Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

NIKWELI HUU NI MTANDAO WA CHADEMA! KAMA VILE ALIYEIPOST ALIKUWA AKILINI MWANGU.Niwatu wasioweza kupima mambo kwa mapana na marefu.Hugombana wao kwa wao,Jaziba ni yakwao,Vujo niyakwao na shari niyakwao.Jana nimesoma Topic moja kuna mwenzao kawapelekea Topic ya zitto.Wakaanza kumshambulia tofauti na maada ilivyotolewa.Niwatu waku offroad kwakweli.
 
Jamaa kiukweli ni jembe, ila too much political timing.
Bora afanye maamuzi magumu ahamie CDM na akatubu kuwa kilichompelekea kuonekana kafanya ufisadi ni mfumo tu na sio dhamira yake, aache kulalama kama mwenzake sumaye.
Manake inaonekana mawaziri wakuu wastaafu wa tz kwa kulalamika hawajambo.

Afadhali a dead hero kuliko a living hero!!
 
Ccm muda uliobaki ni mdogo mno kuelekea uchaguzi,hawana mikakati yoyote ya kushinda uchaguzi wao wako bize kumkata kichwa nyoka wao ,isije ikawa ni technic imetengenezwa ili iwakeep bize wakati wenzao wanachanja mbuga,au wanajiamini ya kuwa ushindi ni wao 2015?.
 
Kubwajinga zama za kutishana na kudanganyana zimepitwa na wakati sasa hivi hadanganyiki mtu mabadiliko ni lazima kuwaita wenzio matapeli huwatendei haki hao wanaowadanganya watanzania kwa miaka 50 sasa lakini hali ya maisha bado ngumu wananchi wategemee lini watapata nafuu ya maisha? Sasa ndio viongozi wa CCM wanahamisha pembe za ndovu wakati Mtanzania bado hana uhakika wa milo mitatu kwa siku hata huo mmoja anbahatisha madidi wamegawana yote,gesi wameanza kuhujumu,mtanzania maskini ategemee nini kutoka kwenye uongozi huu? Nafikiri na wewe ni mmoja wao ndio maana unawakatisha tamaa wenzako kwa tamaa zako za kufikiria neema ambayo hutaipata, Watanzania wameamka sio kama wenye mawazo hasi kama yako
eowange,
Karibu mtandaoni. Lakini ningekushauri uwe mwangalifu na wanasiasa kwani wapo wengi ambao wanatumia hizo shida ulizonazo kukupumbaza kuwa wana nia njema ya kukusaidia. Ukiona mtu (Mbowe) anang'ang'ania madaraka kwenye chama licha ya kutokuwa na sifa, na waliomzunguka wanakubaliana naye, basi ujue maslahi binafsi ndio yanayotawala na sio utatuzi wa shida za nchi.
 
MKUU Mtoi!

Heshima kwako!

Ki ukweli WANA-MAGAMBA wanaucheza MDUMANGE wa CHADEMA kwa kasi kubwa sana. Tatizo hawa jamaa ni vilaza wa kutupwa. Yaani hata mtu kama ni Prof. Anapoingia MAGAMBANI hata akili yake yote inapotea kabisa.

Haya yote walisema hayawezekani wakati ule wa uchaguzi. Leo hii kila MWANA-MAGOME anaimba musiki wa ELIMU BURE, ambayo ilikuwa sera ya CHAMA KUBWA "CHADEMA".

Si hata unasikia Waziri wao wa Ujenzi anavyo aminisha Wadanganyika kwamba CCM imejenga barabara mpya sijui zenye urefu wa zaidi ya KM 11,000 wakati ukweli hawajajenga barabara bali wamekarabati barabara za zamani.

chuki bwana inapumbaza kabisa, bara bara za zamani nani alijenga? CDM? nyerere anachukua nchi kulikua hamna hata mile 500 za lami, yeye akajenga zaidi ya mile 2000, mwinyi ndiyo alikarabati tu muda wake, mkapa akaongeza na Jk sasa amejenga zaidi ya mile 4000 za lami. fikiria kabla ya kuropoka
 
Ni bora watangaze shule ni hela, kuliko tunavyokamuliwa kwa michango isiyoisha!
 
chuki bwana inapumbaza kabisa, bara bara za zamani nani alijenga? CDM? nyerere anachukua nchi kulikua hamna hata mile 500 za lami, yeye akajenga zaidi ya mile 2000, mwinyi ndiyo alikarabati tu muda wake, mkapa akaongeza na Jk sasa amejenga zaidi ya mile 4000 za lami. fikiria kabla ya kuropoka

Mharakati,

siasa za jumla jumla sio nzuri kabisa. Vipaji walivyo navyo watanzania pamoja na rasmali zao na amani yetu hatutegemei kuwa na miundombinu tuliyonayo. It's shame. usiwafanye watanzania kulidhika ktk umaskini huu. we need much that we would have had already. Ebu wambie hao unaoonekana kuwatetea warudishe fedha zetu toka Uswissi. kama unataka kujua hizo barabara kuwa ni danganya toto zitembelee uone. mashimo matupu! hivi mtatudaganya mpaka lini?
 
tuna tofauti kubwa kati yangu na wewe mkuu, ila umeonyesha kua civil tofauti na wengi hapa. I appreciate
Kila serikali ina mapungufu yake, hata marekani wangetumia vizuri sera zao na kujali zaidi wananchi wao, marekani isingekua nchi iliyoendelea huku ikiwa na idadi kubwa ya maskini na hudumna hovyo za afya na elimu kulinganisha na matajiri wenzao.

Sitetei CCM hii ya sasa, lakini bado sioni kama CDM kuondoa matatiizo yetu yote na katika kipindi kifupi, kwani CDM ni nani? mitume? wapinzani gani hapa Afrika wamebadilisha nchi zao kiufanisi namna CDM inavyotaka kutushawishi tena kutushawishi bila mikakati mahsusi ya kuongeza pato la taifa. kwangu hizi ni siasa na wanasiasa wale wale, i appreciate what ccm has done so far ukichukulia miaka 26 ilipotea hivi hivi na experiment za Mwalimu. CDM hawajaniconvice na cheap propaganda bila minofu ya kuelezea watafikia vipi hayo malengo.

hamna nchi imekua kwenye potential yake halisi haswa nchi kubwa kiidadi ya watu na kieneo kama tanzania. mimi siyo mnazi wa siasa za upange wowote, ila siasa za jumla ziko kwa WanaCDM wengi.
 
Mkuu Che Guevara.
Kwa kuijazia minofu hoja yako naomba nitoe na mfano mwingine halisi kwenye hili.

Kampuni ya kufua umeme ya Richmond ilikuwa inalipwa milioni 152 kwa siku, kwa mwezi yaani siku 30 ni sawa 4260 bilioni, ukiipiga hesabu hiyo kwa mwaka unaweza kuchanganyikiwa. Tukirudi kwenye hoja, kama tumeweza kugharamia umeme wa magumashi kwa karibu mwaka mzima, tunakosa vipi udhati wa kugharamia elimu ya vijana wetu?! Hapa kina ndugu yangu chama lazima watueleze tuwaelewe vizuri.

Mkuu, pia tukumbuke kuwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL ambayo toka mwaka 1994 inalipwa sh bilioni 4 kila mwezi kama "Capacity charge", kwa maana kuwa inalipwa kwa kuwepo tu kwa mitambo yao, hii ni mbali na gharama wanazolipwa wakizalisha na kupeleka umeme Tanesco, ambapo hapo inaweza kulipwa mpaka sh bilioni 8 kwa mwezi.
Huu ulikuwa ni mkataba mkubwa wa kwanza wa kifisadi.
Kumbuka kuwa ni miaka 18 imeshapita sasa (miezi 200 na kitu!)
Arghhhhh...

Mara mbili ndani ya mwezi mmoja, pembe za ndovu kutoka huku zimekamatwa bandarini China. Je zimetoka vp huku kwetu kiaina? Ndio maana Maige wakati akiwa waziri wa maliasili alinunua nyumba kwa USD 750,000/-.

Natamani China wanyonge watu, watatusaidia kidogo.

Au tuungane na China kwa "mkataba" ili tutumie sheria zao. Watanyongwa wengi.
 
Yaani watajikanyaga na kubeza sana badaye wanarudi kula matapishi yao kupitia mlango wa nyuma
 
Mkuu, pia tukumbuke kuwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL ambayo toka mwaka 1994 inalipwa sh bilioni 4 kila mwezi kama "Capacity charge", kwa maana kuwa inalipwa kwa kuwepo tu kwa mitambo yao, hii ni mbali na gharama wanazolipwa wakizalisha na kupeleka umeme Tanesco, ambapo hapo inaweza kulipwa mpaka sh bilioni 8 kwa mwezi.
Huu ulikuwa ni mkataba mkubwa wa kwanza wa kifisadi.
Kumbuka kuwa ni miaka 18 imeshapita sasa (miezi 200 na kitu!)
Arghhhhh...

Mara mbili ndani ya mwezi mmoja, pembe za ndovu kutoka huku zimekamatwa bandarini China. Je zimetoka vp huku kwetu kiaina? Ndio maana Maige wakati akiwa waziri wa maliasili alinunua nyumba kwa USD 750,000/-.

Natamani China wanyonge watu, watatusaidia kidogo.

Au tuungane na China kwa "mkataba" ili tutumie sheria zao. Watanyongwa wengi.

Mkuu Che Guevara
Heshima kwako kwa kuendelea kuwa objective kwenye mada,ndugu yangu chama alianza vizuri lakini naona ameungana na Ritz kurukia vioja vya kumjadili Lowasa na urais badala ya hoja iliyooko mezani.

Naomba kwa heshima na taadhima tuendelee kujikita kwenye hoja na hapa ni maelezo ya mwanazuoni Kitila Mkumbo kujazia nyama hoja iliyooko kwenye mjadala.

Maelezo yake ni haya...

KUNA wanaotilia shaka sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoa elimu bure, kuanzia ngazi ya chekechea.

Hao wanaogozwa na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, meneja kampeni wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na spika wa zamani Samwel Sitta.

Wanasema nchi maskini kama Tanzania, haiwezi kutoa elimu bure. Nawambia inawezekana.

Mwaka 1995 wapinzani waliahidi kufuta kodi ya kichwa – CCM waliita kodi ya maendeleo – iliyoleta adha kubwa kwa wananchi hadi wengine kujificha porini wakikimbia kukamatwa na mgambo.

Serikali ilisema haiwezekani kuendesha serikali bila kodi hiyo. Lakini baada ya shinikizo kutoka ndani na nje ya bunge, serikali iliifuta.

Mwaka 2000 wapinzani walikuja na sera ya kufuta ada katika shule za msingi kama njia ya kuwawezesha watoto wengi kuingia shuleni.

Kama kawaida yao, CCM walicharuka tena wakidai kuwa “wapinzani wanaota.” Hata hivyo, baada ya uchaguzi wa 2000 ada katika shule za msingi ilifutwa; wakabakiza kinachoitwa leo: michango.”

Wapinzani wa elimu ya bure wametumia hoja dhaifu, kwamba kwa kufanya hivyo, serikali itashindwa kutekeleza majukumu yake mengine ya msingi.

CHADEMA inapoongelea elimu ya bure inamaanisha kufuta ada zote wanazotozwa wazazi katika shule za sekondari.

Tayari wanafunzi wa shule za msingi hawalipi ada na kwa hivyo kinadharia elimu ya msingi inatolewa bure Tanzania.

Hivyo basi, kila mwanafunzi wa shule ya sekondari anatakiwa kulipa Sh. 20,000 kwa shule za kutwa na Sh. 70,000 kwa shule za bweni.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali mwaka 2010, idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari za serikali walikuwa 1,401,330.

Katika shule zaidi ya 2,000 nchi nzima, shule za bweni zipo 170 zenye wanafunzi wasiozidi 120,000.

Hii inamaanisha kuwa kwa mwaka serikali inakusanya takribani Sh. 25.6 bilioni ikiwa ni ada kutoka kwa wanafunzi wa kutwa na takribani Sh. 8.4 bilioni kutoka kwa wanafunzi wa bweni.

Kwa hivyo, serikali inapata Sh. 34 bilioni ikiwa ni mapato yatokanayo na ada ya wanafunzi katika shule za serikali. Hii ndiyo fedha ambayo serikali itaikosa kwa kutekeleza sera ya elimu bure.

Kama serikali itafuta michango mingine yote ambayo wazazi wenye watoto katika shule za sekondari wanalipa, italazimika kuongeza bajeti yake kwa shule za sekondari kwa kiwango cha Sh. 40 bilioni.

Hii ndiyo kusema kuwa gharama ya kutoa elimu bure, kwa maana ya kumuondelea mzazi mzigo wa ada na michango mingine, ni Sh. 100 bilioni kwa mwaka.

Kuhusu kupanua wigo wa mapato ya kodi, CHADEMA wameweka mkazo katika maeneo mawili:

Moja, kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija na pili kuongeza vyanzo vya kodi ambavyo vimeanishwa vizuri katika bajeti mbadala zilizowasilishwa na kambi ya upinzani bungeni.

Wataalam wa kodi wameshauri kwa miaka mingi kuwa misamaha ya kodi isizidi asilimia moja ya pato la taifa au asilimia 10 ya makusanyo yote ya kodi.

Wanasema punguzo la kodi kwa kiwango hiki halitaathiri mazingira ya uwekezaji nchini. Lakini serikali imepuuza ushauri huu. Matokeo yake mapato mengi ya serikali yamepotea.

Kwa mfano, mwaka 2008/2009 serikali ilisamehe asilimia 2.7 ya pato la taifa – sawa na Sh. 731.3 bilioni.

Kama ingefuata ushauri wa wataalam wa kodi ingesamehe kiasi kisichozidi Sh. 270. 8 bilioni na hivyo kuokoa zaidi ya Sh. 500 bilioni.

Hivyo basi, kupunguza misamaha ya kodi pekee, kutaokoa mara tano (Sh. 500 bilioni) ya fedha ambazo zinatosha kugharamia masomo ya wanafunzi wote nchini.

CHADEMA kitatekeleza ushauri wa wataalam na kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi haizidi kiwango cha asilimia moja ya pato la taifa. Hili limewekwa ndani ya ilani ya chama na dhamira ya viongozi.

Pili, CHADEMA imeahidi kubana matumizi ya serikali kwa kuachana na anasa.

Moja ya maeneo ambayo wamelenga kuokoa fedha ni eneo la posho.

Kwa mujibu wa vitabu vya bajeti, katika mwaka wa fedha wa 2008/09, serikali ilitenga Sh. 506 bilioni ili kulipa posho wafanyakazi wake.

Kiasi hiki cha fedha ni sawa na mishahara ya walimu 109,000, au zaidi ya theluthi mbili ya walimu wote nchini.

Katika mwaka wa fedha wa 2009/10, kiwango kilichotengwa kwa ajili ya posho kilikuwa sawa na asilimia 59 ya mishahara yote ya wafanyakazi wa serikali.

Sehemu kubwa ya posho hizi ni zile zinazolipwa kwa viongozi na maafisa katika taasisi za serikali na haziwahusu watendaji wanaofanya kazi katika mazingira magumu huko vijijini.

Katika ilani yake, CHADEMA imeahidi kupunguza kiwango cha posho hadi kufikia asilimia 15 ya mishahara wanayolipwa wafanyakazi wa serikali.

Msingi wa kukuza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi umejengwa katika kubana matumizi ya serikali na kupanua wigo wa ukusanyaji mapato.

Katika hili, CHADEMA itapunguza ukubwa wa serikali kutoka mawaziri na manaibu mawaziri zaidi ya 40 waliopo sasa hadi 20.

Hii itasaidia kupunguza gharama za kuendesha serikali kwa zaidi ya nusu ya gharama za sasa.

Kwa hatua hii, kiwango cha posho serikalini kitapungua kutoka Sh. 506 bilioni za sasa hadi Sh. 126 bilioni.

Hapa serikali itakuwa imeokoa Sh. 380 bilioni ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwamo uboreshaji wa shule za msingi sekondari na huduma nyingine za jamii.

Kwa hatua mbili tu za kupunguza misamaha ya kodi na kupunguza posho zisizo na tija kwa viongozi na maafisa wa serikali, serikali itaokoa Sh. 880 bilioni.

Hii ni mifano miwili kati ya mingi ambayo serikali makini ya CHADEMA inaahidi katika kutumia vizuri fedha za walipakodi kwa ajili ya maendeleo na kuboresha utoaji huduma za jamii, ikiwemo kutoa elimu bure.

CHADEMA haijakokotoa fedha zitakazookolewa kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kufuta nafasi za wakuu wa wilaya.

Aidha, haijkokotoa fedha zitakazopatikana kwa kutokomeza ufisadi serikalini na zitakazopatikana kwa kuimarisha mikataba ya madini.

Kwa hiyo, utaona kuwa kwa kutumia mifano michache niliyoitoa hapo juu, tatizo sio ukosefu wa fedha katika kutoa elimu bure na huduma nyingine za jamii.

Tatizo ni ukosefu wa utashi wa kisiasa, ukosefu wa upeo, uadilifu na umakini.

Mwandishi wa makala hii ni mhadhiri katika Idara ya Saikolojia ya Elimu na Taaluma za Mitaala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaa. na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA.

*Nimeyachota kwenye gazeti la mwanahalisi la 13 October 2010*.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Che Guevara
Heshima kwako kwa kuendelea kuwa objective kwenye mada,ndugu yangu chama alianza vizuri lakini naona ameungana na Ritz kurukia vioja vya kumjadili Lowasa na urais badala ya hoja iliyooko mezani.

Naomba kwa heshima na taadhima tuendelee kujikita kwenye hoja na hapa ni maelezo ya mwanazuoni Kitila Mkumbo kujazia nyama hoja iliyooko kwenye mjadala.

Maelezo yake ni haya...

KUNA wanaotilia shaka sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoa elimu bure, kuanzia ngazi ya chekechea.

Hao wanaogozwa na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, meneja kampeni wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na spika wa zamani Samwel Sitta.

Wanasema nchi maskini kama Tanzania, haiwezi kutoa elimu bure. Nawambia inawezekana.

Mwaka 1995 wapinzani waliahidi kufuta kodi ya kichwa – CCM waliita kodi ya maendeleo – iliyoleta adha kubwa kwa wananchi hadi wengine kujificha porini wakikimbia kukamatwa na mgambo.

Serikali ilisema haiwezekani kuendesha serikali bila kodi hiyo. Lakini baada ya shinikizo kutoka ndani na nje ya bunge, serikali iliifuta.

Mwaka 2000 wapinzani walikuja na sera ya kufuta ada katika shule za msingi kama njia ya kuwawezesha watoto wengi kuingia shuleni.

Kama kawaida yao, CCM walicharuka tena wakidai kuwa "wapinzani wanaota." Hata hivyo, baada ya uchaguzi wa 2000 ada katika shule za msingi ilifutwa; wakabakiza kinachoitwa leo: michango."

Wapinzani wa elimu ya bure wametumia hoja dhaifu, kwamba kwa kufanya hivyo, serikali itashindwa kutekeleza majukumu yake mengine ya msingi.

CHADEMA inapoongelea elimu ya bure inamaanisha kufuta ada zote wanazotozwa wazazi katika shule za sekondari.

Tayari wanafunzi wa shule za msingi hawalipi ada na kwa hivyo kinadharia elimu ya msingi inatolewa bure Tanzania.

Hivyo basi, kila mwanafunzi wa shule ya sekondari anatakiwa kulipa Sh. 20,000 kwa shule za kutwa na Sh. 70,000 kwa shule za bweni.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali mwaka 2010, idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari za serikali walikuwa 1,401,330.

Katika shule zaidi ya 2,000 nchi nzima, shule za bweni zipo 170 zenye wanafunzi wasiozidi 120,000.

Hii inamaanisha kuwa kwa mwaka serikali inakusanya takribani Sh. 25.6 bilioni ikiwa ni ada kutoka kwa wanafunzi wa kutwa na takribani Sh. 8.4 bilioni kutoka kwa wanafunzi wa bweni.

Kwa hivyo, serikali inapata Sh. 34 bilioni ikiwa ni mapato yatokanayo na ada ya wanafunzi katika shule za serikali. Hii ndiyo fedha ambayo serikali itaikosa kwa kutekeleza sera ya elimu bure.

Kama serikali itafuta michango mingine yote ambayo wazazi wenye watoto katika shule za sekondari wanalipa, italazimika kuongeza bajeti yake kwa shule za sekondari kwa kiwango cha Sh. 40 bilioni.

Hii ndiyo kusema kuwa gharama ya kutoa elimu bure, kwa maana ya kumuondelea mzazi mzigo wa ada na michango mingine, ni Sh. 100 bilioni kwa mwaka.

Kuhusu kupanua wigo wa mapato ya kodi, CHADEMA wameweka mkazo katika maeneo mawili:

Moja, kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija na pili kuongeza vyanzo vya kodi ambavyo vimeanishwa vizuri katika bajeti mbadala zilizowasilishwa na kambi ya upinzani bungeni.

Wataalam wa kodi wameshauri kwa miaka mingi kuwa misamaha ya kodi isizidi asilimia moja ya pato la taifa au asilimia 10 ya makusanyo yote ya kodi.

Wanasema punguzo la kodi kwa kiwango hiki halitaathiri mazingira ya uwekezaji nchini. Lakini serikali imepuuza ushauri huu. Matokeo yake mapato mengi ya serikali yamepotea.

Kwa mfano, mwaka 2008/2009 serikali ilisamehe asilimia 2.7 ya pato la taifa – sawa na Sh. 731.3 bilioni.

Kama ingefuata ushauri wa wataalam wa kodi ingesamehe kiasi kisichozidi Sh. 270. 8 bilioni na hivyo kuokoa zaidi ya Sh. 500 bilioni.

Hivyo basi, kupunguza misamaha ya kodi pekee, kutaokoa mara tano (Sh. 500 bilioni) ya fedha ambazo zinatosha kugharamia masomo ya wanafunzi wote nchini.

CHADEMA kitatekeleza ushauri wa wataalam na kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi haizidi kiwango cha asilimia moja ya pato la taifa. Hili limewekwa ndani ya ilani ya chama na dhamira ya viongozi.

Pili, CHADEMA imeahidi kubana matumizi ya serikali kwa kuachana na anasa.

Moja ya maeneo ambayo wamelenga kuokoa fedha ni eneo la posho.

Kwa mujibu wa vitabu vya bajeti, katika mwaka wa fedha wa 2008/09, serikali ilitenga Sh. 506 bilioni ili kulipa posho wafanyakazi wake.

Kiasi hiki cha fedha ni sawa na mishahara ya walimu 109,000, au zaidi ya theluthi mbili ya walimu wote nchini.

Katika mwaka wa fedha wa 2009/10, kiwango kilichotengwa kwa ajili ya posho kilikuwa sawa na asilimia 59 ya mishahara yote ya wafanyakazi wa serikali.

Sehemu kubwa ya posho hizi ni zile zinazolipwa kwa viongozi na maafisa katika taasisi za serikali na haziwahusu watendaji wanaofanya kazi katika mazingira magumu huko vijijini.

Katika ilani yake, CHADEMA imeahidi kupunguza kiwango cha posho hadi kufikia asilimia 15 ya mishahara wanayolipwa wafanyakazi wa serikali.

Msingi wa kukuza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi umejengwa katika kubana matumizi ya serikali na kupanua wigo wa ukusanyaji mapato.

Katika hili, CHADEMA itapunguza ukubwa wa serikali kutoka mawaziri na manaibu mawaziri zaidi ya 40 waliopo sasa hadi 20.

Hii itasaidia kupunguza gharama za kuendesha serikali kwa zaidi ya nusu ya gharama za sasa.

Kwa hatua hii, kiwango cha posho serikalini kitapungua kutoka Sh. 506 bilioni za sasa hadi Sh. 126 bilioni.

Hapa serikali itakuwa imeokoa Sh. 380 bilioni ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwamo uboreshaji wa shule za msingi sekondari na huduma nyingine za jamii.

Kwa hatua mbili tu za kupunguza misamaha ya kodi na kupunguza posho zisizo na tija kwa viongozi na maafisa wa serikali, serikali itaokoa Sh. 880 bilioni.

Hii ni mifano miwili kati ya mingi ambayo serikali makini ya CHADEMA inaahidi katika kutumia vizuri fedha za walipakodi kwa ajili ya maendeleo na kuboresha utoaji huduma za jamii, ikiwemo kutoa elimu bure.

CHADEMA haijakokotoa fedha zitakazookolewa kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kufuta nafasi za wakuu wa wilaya.

Aidha, haijkokotoa fedha zitakazopatikana kwa kutokomeza ufisadi serikalini na zitakazopatikana kwa kuimarisha mikataba ya madini.

Kwa hiyo, utaona kuwa kwa kutumia mifano michache niliyoitoa hapo juu, tatizo sio ukosefu wa fedha katika kutoa elimu bure na huduma nyingine za jamii.

Tatizo ni ukosefu wa utashi wa kisiasa, ukosefu wa upeo, uadilifu na umakini.

Mwandishi wa makala hii ni mhadhiri katika Idara ya Saikolojia ya Elimu na Taaluma za Mitaala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaa. na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA.

*Nimeyachota kwenye gazeti la mwanahalisi la 13 October 2010*.

R.I.P Mwanahalisi...:rip:
 
R.I.P Mwanahalisi...:rip:

I didn't expect white from charcoal! Yes R. I. P mwanahalisi but what about what is written in Mwanahalisi?! Is it also dead?! Face reality and be objective in the discussion, if shoes can't fit you don't wear them.
 
mkuu na kwataarifa tu na hizo pesa zinaelekea mwishon kutoa hizo capitation grand na sasa ndio wazaz kukamuliwa hadi basi hii ndio ccm yenye kila maajabu.
 
Mkuu IBRAAH.
kuna usanii mkubwa sana kwenye swala la elimu. Mfano angalia kwenye swala la ujenzi wa mashule, wananchi wengi vijijini wamechangishwa fedha, wale walio shindwa wamenyang'wa vitu vyao kwa kushindwa kuchangia ujenzi wa mashule (kwetu lushoto tunaita "kuhambua"),wengi wamepoteza ng'ombe, mbuzi, kondoo, au kuku eti tu kwa kuwa wameshindwa kuchangia ujenzi wa shule za kata. Halafu wana siasa hasa ccm wakisimama majukwaani wanajipiga vifua "Tumejenga shule kila kata" matokeo yake shule nyingi zimejenwa chini ya kiwango na madarasa mengi yako kama mabanda ya kuku.

Hapo hujaja kwenye uwepo wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, huja angalia ubora wa walimu na elimu wanayotoa. Ukijumuisha hayo yote unaona jinsi ndugu yangu chama anapovyo pingana na sera ya chama chake kwa ndani kabisa maana naye ana amini kwenye private zenye mazingira bora na walimu bora huku akipingana na sera ya chama chake.

Kama kuna makosa makubwa ambayo serikali ya ccm imeyafanya ni kuchezea elimu ya Tanzania. Inasikitisha sana ukisoma tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya elimu ya nchi yetu, na ili ujue elimu yetu imefikia wapi subiria matokeo ya kidato cha pili ya mwaka huu ndio utaona jinsi mpango wa shule za kata ulivyo feli kwa kutawaliwa na siasa badala ya utaalamu wa kitaaluma.
 
Last edited by a moderator:
Lowassa ni jembe la ukweli hilo halina ubishi kuliko wale wanaobebwa bebwa na mkulu
 
Mkuu Mtoi
Nadhani mpaka sasa hivi unajiuliza kwa nini napingana na kauli za mh. Lowassa; yeye ndiye muasisi wa shule za kata; mpango mzima ulifeli kwasababu hakukuwa na uwiano kati ya majengo na vitendea hii ikijumuisha na idaidi walimu; mh. Lowassa ni mwanasiasa ambaye upepo wake kisiasa umezimika na anajitahidi kila siku kusema vitu ambavyo havina mpangilio; au inahitilafiana na sera makini za CCM; sisi tunasema kilimo kwanza yeye kadakia elimu kwanza; yote hii ni kuwa kaishiwa kisiasa. Mkuu Mtoi sera ya elimu ya CCM haijatukataza tusipeleke vijana wetu kwenye mashule ya binafsi; mwenyekiti MBOWE amepeleka watoto wake shule ya vichekechea nasikia analipa milioni 7 hivi unategemea Chadema ikiingia madarakani MBOWE atawapeleka wanawe kwenye shule za serikali? Sijafanikiwa kimaisha najihini ili niwapeleke shule wanangu; nimekuambia kuna siku nakula muhogo usio na towezi; mkuu usiwaamini sana hao watu wana ajenda binafsi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom