Dr Slaa aliisoma tu aliyeiandika T Lisu, muulizeni kwa nn alitunga uongoSlaa ndo alikuja na ile listi ya mafisadi Mwembe Yanga. Kama Lowassa alikuwemo humo, muondoe halafu ndo tuanze kujadiliana kuhusu ukweli wa Slaa kuwa Lowassa ni fisadi. Slaa naye anaweza kuwa victim kama mimi tu. Kwasababu nilijiapiza sitoweza kumpigia kura fisadi. Slaa alikuwa na fikra kama hizo. Kwasababu wana Jf asili humu karibia wote tulilishwa sumu kuhusu Lowassa. Slaa tulikuwa naye humu, wote tukiamini kuwa Lowassa ndo fisadi kuu. Kumbe hata wapi bhana.
Itabakia hivi FULLstopWishful thinking, lkn haikuwa sasa after all, kila mtu anaweza kusema chochote hata mimi nawezaa kusema Lowasa could have been worse, hizo zote ni wishful thinking, Watanzania tumemkataa Fisadi Lowasa na itabakia kuwa hivyo!
Mkuu Kwani hata akiisoma yeye kuna utofauti gani? Taarifa zenyewe si zilitoka ndani ya serikali? Wewe unadhani kwanini walizitoa? Pengine chadema na kina Lissu walilishwa kasa na wao wakaja kutulisha sisi. Tumia akili, na pia utulie unapofikiri kuhusu hii issue. Usiende kiushabiki utapotea.Acha ujinga Dr Slaa aliisoma tu aliyeiandika TLizu, muulizeni kea nn alitunga uongo
Dah hapo watu hawafaiMkuu nimekuwekea maelezo ya Sumaye kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali na bado unamuita Magu fisadi bila kuweka ushahidi wa kueleweka ila unakataa Lowassa asiitwe fisadi pamoja na ushahidi wa bunge. Au umekumbuka tu nyumbani leo bwn mushi?
Mkuu mbona yako wazi hayo? Hata ndugu yake aliyepewa kazi fasta fasta ili aweze kuqualify kama mfanyakaz wa serikali na kuuziwa hiyo nyumba anafahamika?
Mimi binafsi nililifumbia macho hilo kwasababu nilidhani Lowassa ni fisadi kuu lilouza nchi yetu na rasilimali zetu. Kumbe wapi bhana.
Utalindwa vipi ukiwa nje ya ccm? Ndo maana navyofahamu hasira na nyongo za mkulu, Lowassa angekuwa fisadi sahii ungekuta ananyea debe.
Hasa pale Slaa alipoamua kususa na kuachana na siasa ndiyo iliwaumiza sana wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumlaHuu ni ukweli mchungu. CHADEMA wana makosa yao pia. Inawezekana waligunduwa wameingizwa chaka, lakini shida iko upande wa wananchi. Tulichanganywa siyo siri.
Mpaka sasa tutajieuyu asie nagege kakamata gege gani na lime lipa nini na taifa limefaidikaje nauchumi wako wewe umebadilikaje?Magufuli ni rais bora kabisa kuwai kutokea. Acheni akili fupi za kiafrika, huyo lowassa kwa mfano angefanya nini ambacho magu hafanyi zaidi ya wizi yeye na genge lake la kina rostam karamagi
Heshima gani aliyo rudisha, kupungua kwa pato la mtanzania na mfumuko wa bei kupaa ndio heshima?Nilimpigia Magufuli na nitampigia tena na tena, rais aliyekomesha rushwa aina ya richmond na kirudisha heshima mtaani.
Aliye sema nchi imekaa tengeiwekwe sawa nani?? Walio iweka tenge akina nani? Yeye wakuiweka sawa hakushiriki kwenye awamu za kuiweka tenge??Mpinzani aliyekuwa serious ni Slaa pekee, ndio mtu aliyekuwa na uwezo wa kusafisha nchi kwa 100% awa kina Lowassa ni bora ata Hashm rungwe.. Magu anafanya kile mlichokililia miaka yote lazima mkubali gharama ya kila mnachoitaji. Mnataka nchi ikae sawa uku mnachekelea tu bila kuwajibika sheinz kabisa.
kwahapo siamini ingawa nilikuwa nipo naye.waliomzunguka sijui angefanyajeJK inawezekana alikuwa ana wivu kuona besti yake naye akiingia kwenye listi ya mapresdaa. Ili kwenye group lao EL asimfunike. Maana kiukweli walikuwa marafiki. Lakini urafiki wa JK ulikuwa wa kinafiki zaidi.
JK akaleta siasa za "kuvua gamba", akiwa target walio kuwa wakipigiwa kelele za ufisadi. JK alijuwa EL si fisadi lakini alinyamaza na kuendeleza politics za kiswalihina. Ufisadi wote wa kuuza nchi EL hajatokea.
JK yuko responsible kwasababu hata mimi nilimpigia kura Maghufuli badala ya Lowassa kwa kuamini ni fisadi ambaye JK anaogopa kumtimua waziwazi ili chama kisimegeke. But I was wrong.
JK pia alitaka wananchi wamkumbuke uongozi wake ndo maana akaona JPM anafaa zaidi kwasababu anamfahamu vyema(alishawahi kupindua maamuzi yake mengi tu JPM alipokuwa waziri na JK rais), JK alijuwa kuna namna mambo yatakuwa ndivyo sivyo na wananchi kulalamika zaidi, hence kumkumbuka.
However nimekaa nikafikiria, sababu kubwa ya kumpigia kura JPM badala ya Lowassa ni ufisadi. Nikasubiri ccm wamshitaki EL, wapi. Subiri wataje kashfa ambaye kiukweli amehusika yeye, hakuna.
Yani ina maana kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa ndugu zake, inaonyesha wazi uncle Magu ni fisadi na wala siyo EL.
Kwahiyo hapa kusema JPM ni msafi kuliko EL ni upotoshaji mkubwa kabisa.
Hivyo basi hapo ndo tofauti kubwa ya kwanza kabisa kati ya hao viongozi wawili. Pia kingine ni busara. Mzee EL ana busara sana, na pia huchaguwa maneno ya kuzungumza nk.
Watu hao lakini pia wana similarities. Yani kuna mambo wanafanana. Na hilo ni ufuatiliaji, utekelezaji na uwajibikaji.
Hizo ndo nguzo kuu za sifa za Lowassa. Sasa wale ambao hatukuwa na uhakika kuhusu EL, tukaona kuwa Maghufuli pia anaweza kufanya tu kama yeye.
Lakini tofauti ni ukosefu wa busara kwenye maamuzi hayo. Busara ikikosekana kwenye jambo lolote la msingi, basi matokeo yake ni sawa "kujipiga risasi ya mguuni" ukiwa kwenye safari inayoitegemea miguu hiyo.
EL pia ni msikilizaji. Hiyo sifa rais wetu wa sasa hana. Nina imani kuna anaowasikiliza wachache, ambao hao kwake hawana makosa.
Pamoja na sifa ya ujasiri na uchukuaji wa maamuzi magumu alizonazo EL, bado ni mtu mwenye UPENDO na HURUMA.
Rais anaonekana ana ujasiri. Wengi wanapiga wanasema ni uoga. Mimi ninaamini ana ujasiri, lakini hana upendo wala huruma hata chembe.
Binafsi ninaamini rais lazima awe na empathy, yani uwezo wa kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine na kuona anayopitia. Mtu wa namna hawezi kukosa huruma na upendo, ingredients ambazo ni muhimu sana kwenye jamii ya kitanzania. Aliposhindwa kujiweka kwenye nafasi ya wafiwa, aliamuru rambi rambi zisikabidhiwe kwa wafiwa/waathirika. Hapo ndipo utaona umuhimu wa empathy kwa kiongozi mkuu wa nchi.
Pia EL siyo mtu wa visasi wala vinyongo. Kwa kuwa nilikuwa nimeshamchukia sana kwasababu za uongo kuwa ni fisadi namba moja nchini, nilishindwa kuamini kama hana hizo characteristics.
Nikawa nadhani anajifanyisha tu pale ambapo akitukanwa wala hajibu. Na wanaomuita fisadi hawamyimi usingizi. Yani wala hakutumia nguvu kubwa kupingana na hao wanaomuita fisadi na matusi mengine.
Binafsi ninaamini kuwa JPM amepiga marufuku siasa kwasababu ya Lowassa. Kiukweli, wengi wangeona makosa makubwa tuliyofanya.
Hapo mwanzoni nilikubaliana na JPM kuwa serikali inatakiwa ipewe muda wa kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake badala ya kuendeleza siasa. However sasa nimegunduwa kuwa sababu kubwa ni yeye binafsi. Wasiwasi kuwa wananchi watagunduwa mapema makosa waliyoyafanya.
Kama Mungu akimpa uzima, na afya ikawa inaruhusu, nina imani kuwa Lowassa bado ana nafasi ya kuongoza Taifa letu. Pengine akayafanya yale mazuri yaliyoko kwenye uongozi huu wa sasa, na kuachana na negativity zote za utawala huu.
La mwisho kabisa, ni uzalendo wa kweli.
Hii nchi imefikishwa hapa ilipo na chadema,???? Uwo wizi, semina za ovyo ovyo, rushwa wame fanya chadema?? Uyo rais unae mdifine kuwa ndio alitakiwa alikuwa kwenye serikali gani kama sio hii hii anayo ilalamikia? Acheni unafki ccm uongo umewzidi!! Mtu ansimama anasema hili baadae lile eti ndio tuliye muhitaji!Hii nchi imefika hapa tulipo si kwasababu ya viongozi tu bali wananchi wengi ambao ni mazuzu kama mleta mada.
Mleta unawakilisha aina ya mazuzu wasiojua nchi ilifika wapi na ilihitaji kiongozi wa aina gani kutuchongea njia tuliyopotea.
Mtu anazunguka misikitini, makanisani vyama mbalimbali vya kijamii kote anamwaga hela,,, akiulizwa anasema eti pesa za marafiki zangu,,,hujiulizi hizo ela angezirudisha vipi!???
Pia yote kwa yote, walioasisi vita ya ufisadi na kupelekea Lowassa kujiuzulu ni CHADEMA. Labda mleta mada ungeuliza je Chadema waliudanganya na kuulaghai umma!????
Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
Bob,katukomoa wote sasaWengi hamjui kilichomponza Lowasa kwa JK.
Tatizo lilikuwa Lowasa kumdharau JK akiwa waziri mkuu kiasi cha kuwa akisafiri nje ya nchi bila kumjulisha JK wakati huo naye akiwa nje. Sasa jamaa alitaka kumuonyesha tu kuwa yeye yupo juu hata kama wao (Lowasa na marafiki zake) ndiyo waliomfikisha hapo juu.
Dogo mradi wa maji ziwa Victoria Lowasa kaukuta uko mezani kwa utekelezaji.
City water Lowasa alikuwa akivuta 200m kwa mwezi kama commission alipoingia mwandozya wizarani akmjulisha mkapa akampiga marufuku Lowasa kupokea commission ndo chuki yake Lowasa ikaanza kwa city water alipoupata Waziri mkuu ikaanza nao.akawatimua.
forget about this highly corrupt man Lowasa.
Wale majaa watata wa 777 wote wangekuwa mabalozi na wakuu wa mikoa na wengine wezi wa mfukoni kwa kutumia dola. Hafai baba yule bora amekaa mbali...ila namuheshimu sana maana ametulia tuliiiNilifanya uamuzi wa ajabu sana kumpigia kura Lowasa.
Mtu aliyeishia kusoma theatre arts (usanii) utamlinganisha na mwenye PhD ya sayansi? Utakuwa na akili kweli?
Sumaye na Lowassa.Aliye sema nchi imekaa tengeiwekwe sawa nani?? Walio iweka tenge akina nani? Yeye wakuiweka sawa hakushiriki kwenye awamu za kuiweka tenge??