Lowassa could've done better...

Lowassa could've done better...

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,375
Reaction score
25,453
JK inawezekana alikuwa ana wivu kuona besti yake naye akiingia kwenye listi ya mapresdaa. Ili kwenye group lao EL asimfunike. Maana kiukweli walikuwa marafiki. Lakini urafiki wa JK ulikuwa wa kinafiki zaidi.

JK akaleta siasa za "kuvua gamba", akiwa target walio kuwa wakipigiwa kelele za ufisadi. JK alijuwa EL si fisadi lakini alinyamaza na kuendeleza politics za kiswalihina. Ufisadi wote wa kuuza nchi EL hajatokea.

JK yuko responsible kwasababu hata mimi nilimpigia kura Maghufuli badala ya Lowassa kwa kuamini ni fisadi ambaye JK anaogopa kumtimua waziwazi ili chama kisimegeke. But I was wrong.

JK pia alitaka wananchi wamkumbuke uongozi wake ndo maana akaona JPM anafaa zaidi kwasababu anamfahamu vyema(alishawahi kupindua maamuzi yake mengi tu JPM alipokuwa waziri na JK rais), JK alijuwa kuna namna mambo yatakuwa ndivyo sivyo na wananchi kulalamika zaidi, hence kumkumbuka.

However nimekaa nikafikiria, sababu kubwa ya kumpigia kura JPM badala ya Lowassa ni ufisadi. Nikasubiri ccm wamshitaki EL, wapi. Subiri wataje kashfa ambayo kiukweli amehusika yeye, hakuna.

Yani ina maana kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa ndugu zake, inaonyesha wazi uncle Magu ni fisadi na wala siyo EL.

Kwahiyo hapa kusema JPM ni msafi kuliko EL ni upotoshaji mkubwa kabisa.

Hivyo basi hapo ndo tofauti kubwa ya kwanza kabisa kati ya hao viongozi wawili. Pia kingine ni busara. Mzee EL ana busara sana, na pia huchaguwa maneno ya kuzungumza nk.

Watu hao lakini pia wana similarities. Yani kuna mambo wanafanana. Na hilo ni ufuatiliaji, utekelezaji na uwajibikaji.

Hizo ndo nguzo kuu za sifa za Lowassa. Sasa wale ambao hatukuwa na uhakika kuhusu EL, tukaona kuwa Maghufuli pia anaweza kufanya tu kama yeye.

Lakini tofauti ni ukosefu wa busara kwenye maamuzi hayo. Busara ikikosekana kwenye jambo lolote la msingi, basi matokeo yake ni sawa na "kujipiga risasi ya mguuni" ukiwa kwenye safari inayoitegemea miguu hiyo.

EL pia ni msikilizaji. Hiyo sifa rais wetu wa sasa hana. Nina imani kuna anaowasikiliza ni wachache, ambao hao kwake hawana makosa.

Pamoja na sifa ya ujasiri na uchukuaji wa maamuzi magumu alizonazo EL, bado ni mtu mwenye UPENDO na HURUMA.

Rais anaonekana ana ujasiri. Wengi wanapinga, wanasema ni uoga. Mimi ninaamini ana ujasiri, lakini hana upendo wala huruma hata chembe.

Binafsi ninaamini rais lazima awe na empathy, yani uwezo wa kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine na kuona anayoyapitia. Mtu wa namna hiyo hawezi kukosa huruma na upendo, ingredients ambazo ni muhimu sana kwenye jamii ya kitanzania.

Aliposhindwa kujiweka kwenye nafasi ya wafiwa, aliamuru rambi rambi zisikabidhiwe kwa wafiwa/waathirika. Hapo ndipo utaona umuhimu wa empathy kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Pia EL siyo mtu wa visasi wala vinyongo. Kwa kuwa nilikuwa nimeshamchukia sana kwasababu za uongo kuwa ni fisadi namba moja nchini, nilishindwa kuamini kama hana hizo characteristics.

Nikawa nadhani anajifanyisha tu pale ambapo akitukanwa wala hajibu. Na wanaomuita fisadi hawamnyimi usingizi. Yani wala hakutumia nguvu kubwa kupingana na hao wanaomuita fisadi na matusi mengine.

Binafsi ninaamini kuwa JPM amepiga marufuku siasa kwasababu ya Lowassa. Kiukweli, wengi wangeona makosa makubwa tuliyofanya.

Hapo mwanzoni nilikubaliana na JPM kuwa serikali inatakiwa ipewe muda wa kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake badala ya kuendeleza siasa. However sasa nimegunduwa kuwa sababu kubwa ni yeye binafsi. Wasiwasi kuwa wananchi watagunduwa mapema makosa waliyoyafanya.

Kama Mungu akimpa uzima, na afya ikawa inaruhusu, nina imani kuwa Lowassa bado ana nafasi ya kuongoza Taifa letu. Pengine akayafanya yale mazuri yaliyoko kwenye uongozi huu wa sasa, na kuachana na negativity zote za utawala huu.

La mwisho kabisa, ni uzalendo wa kweli.
 
Wengi hamjui kilichomponza Lowasa kwa JK.
Tatizo lilikuwa Lowasa kumdharau JK akiwa waziri mkuu kiasi cha kuwa akisafiri nje ya nchi bila kumjulisha JK wakati huo naye akiwa nje. Sasa jamaa alitaka kumuonyesha tu kuwa yeye yupo juu hata kama wao (Lowasa na marafiki zake) ndiyo waliomfikisha hapo juu.
 
Uchambuzi mzuri. Ila kumbuka Lowassa hana maono kabisa ya uongozi. Rejea vision yake wakati wa uchaguzi: "education, education, education". Aliiga kwa Tony Blair (Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza) hii vision; na pia hakuwa na record nzuri ya kuendeleza elimu nchini. Legacy yake ilikuwa ni shule za kata. Ambazo karibu zote ni majanga. Kimaamuzi pia Lowassa ni bomu. Rejea memo alizokuwa akiandika kuharakisha suala la Richmond wakati wa uongozi wake ambazo zilikuja kuibuliwa na kamati ya Mwakyembe.

Sema yote lakini usiniambie Lowassa ni Kiongozi mzuri aisee. In fact, ukilinganisha na Magufuli, Magufuli is better, japokuwa mimi mwenyewe simkubali Magufuli sana.
 
Sema yote lakini usiniambie Lowassa ni Kiongozi mzuri aisee. In fact, ukilinganisha na Magufuli, Magufuli is better, japokuwa mimi mwenyewe simkubali Magufuli.

Mpinzani aliyekuwa serious ni Slaa pekee, ndio mtu aliyekuwa na uwezo wa kusafisha nchi kwa 100% awa kina Lowassa ni bora ata Hashm rungwe.. Magu anafanya kile mlichokililia miaka yote lazima mkubali gharama ya kila mnachoitaji. Mnataka nchi ikae sawa uku mnachekelea tu bila kuwajibika sheinz kabisa.
 
Angepita lowasa...today pasingekuwepo haya ambayo magufuli amefaulu kuyaleta...napoiangalia TZ ya 2030 sio TZ ya 2005 .
Sasa kuhusu yapi magufuli kafanya ,,Mimi naanza nahili :-

Kukuakikisha Vyombo vyetu vya ulinzi kua vya kisasa navinavyolinda Amani yanchi ivo Basi saizi tunaendelea kucheka kwa amani.
b1b341907f48e786120a2a3e4843e82d.jpg
 
Mpinzani aliyekuwa serious ni Slaa pekee, ndio mtu aliyekuwa na uwezo wa kusafisha nchi kwa 100% awa kina Lowassa ni bora ata Hashm rungwe.. Magu anafanya kile mlichokililia miaka yote lazima mkubali gharama ya kila mnachoitaji. Mnataka nchi ikae sawa uku mnachekelea tu bila kuwajibika sheinz kabisa.

Magufuli anaumiza watu haohao anaojaribu kuwaponya. That's my problem with him. Huwezi kuniambia serikali inapiga vita ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi. Halafu serikali hiyohiyo ina pesa ya kukamata watu wake na kuwatisha kwa silaha za kivita pale hao watu wanapotaka kukusanyika kutoa maoni yao peacefully kuhusu mwelekeo wa nchi. Acha ujinga.
 
Hii nchi imefika hapa tulipo si kwasababu ya viongozi tu bali wananchi wengi ambao ni mazuzu kama mleta mada.
Mleta unawakilisha aina ya mazuzu wasiojua nchi ilifika wapi na ilihitaji kiongozi wa aina gani kutuchongea njia tuliyopotea.

Mtu anazunguka misikitini, makanisani vyama mbalimbali vya kijamii kote anamwaga hela,,, akiulizwa anasema eti pesa za marafiki zangu,,,hujiulizi hizo ela angezirudisha vipi!???

Pia yote kwa yote, walioasisi vita ya ufisadi na kupelekea Lowassa kujiuzulu ni CHADEMA. Labda mleta mada ungeuliza je Chadema waliudanganya na kuulaghai umma!????

Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
 
Nilimpigia Magufuli na nitampigia tena na tena, rais aliyekomesha rushwa aina ya richmond na kirudisha heshima mtaani.
Mkuu hata mimi nilikuwa ukurasa mmoja na wewe. Kwani Lowassa ndo Richmond? Usidanganyike mkuu. Issue ya Richmond ilianzia humu JF, lakini ingekuwa amehusika lazima angeshitakiwa, ama hata ushahidi kuwekwa wazi. Hadi usawa huu, kashfa ya Magu kuuza nyumba za serikali ni kubwa kuliko hizo tetesi kuwa EL ni fisadi.

Pia unaposema amekomesha kashfa aina ya Richmond unakosea. Nadhani kipindi hiki kuna nidhamu ya woga tu. Tena unaweza kuta kuna kashfa mbaya kuliko zote zilizopita.

Hata escrow chini ya utawala huu ingefunikwa tu kama kina Lugumi nk. Na wala isingejulikana.

Serikali ya awamu hii huwa ukitoa kashfa hata kama ni kweli inakula kwako, ndo maana whistle blowers kama Tundu Lissu wanaonekana ni maadui wa Taifa. Sasa unategemea nini hapo?

Serikali hii, cha muhimu ni rais akupende tu basi. It's not about the nation, it's about the president and his cronies.
 
..mleta mada umesahau hili la jpm kuitia hasara nchi wakati wa u waziri wake...ambapo hadi leo nchi imeathirika mno na mzigo wa faini za kimataifa kwa makosa ya maamuzi ya JPM...

...ukiondoa uuzaji wa nyumba za serikali....kuna issue ya kubomoa kile kituo cha mafuta mwanza bila kuskia ushauri....jambo lililopeleleka hasara kwa nchi baada ya muhanga kulipwa fidia...

..kipo lile la kutaifisha meli ya wachina yenye samaki...napo tukashindwa kesi...
...likaja la kuwakatia mkatba ile kampuni ya ujenzi ya Canada...iliyowapelekea kishinda kesi tribune ...na ndege yetu kushikwa rehani...
...lipo pia la kuwatimua konoike Japan.... Ambapo sasa kuna kesi ya kujibu kwa kukataa kuwalipa tuzo ya fidia tribune...
.

My take..hivi ukiyajumlisha haya yote nani Kati ya lowassa na JPM ameitia nchi hasara zaidi ya mwingine?????

......ikumbukwe kuwa lowassa Ana credit kwenye issue ya Ujenzi wa Maji ya Victoria Kule shinyanga...pia alivunja mkataba na city water na tukashinda kesi...jambo ambalo JPM ameshindwa....kwa haya tu nani mwenye maamuzi sahihi????
...haya ndio mambo yanamfanya JPM azuie mikutano ya kisiasa..maana watu wakijua Hana chake.....
 
Uchambuzi mzuri. Ila kumbuka Lowassa hana maono kabisa ya uongozi. Rejea vision yake wakati wa uchaguzi: "education, education, education". Aliiga kwa Tony Blair (Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza) hii vision; na pia hakuwa na record nzuri ya kuendeleza elimu nchini. Legacy yake ilikuwa ni shule za kata. Ambazo karibu zote ni majanga. Kimaamuzi pia Lowassa ni bomu. Rejea memo alizokuwa akiandika kuharakisha suala la Richmond wakati wa uongozi wake ambazo zilikuja kuibuliwa na kamati ya Mwakyembe.

Sema yote lakini usiniambie Lowassa ni Kiongozi mzuri aisee. In fact, ukilinganisha na Magufuli, Magufuli is better, japokuwa mimi mwenyewe simkubali Magufuli sana.
Yani hizo memo za Mwakyembe ndo zinakufanya uconclude kwamba "siyo mtu wa maamuzi magumu"? Kamati ya Mwakyembe ilitaka kumfanya scape goat au mbuzi kafara tu. Angekuwa respinsible tena na sasa ni mpinzani, msingemuacha, kama mnavyomfanyia waziri mkuu mstaafu mwingine aliyeenda upinzani(Sumaye)

Maghufuli is better in what sense? Kama ni ufisadi, yeye ndo aliuza nyumba za serikali kwa bei chee na nyingine akagawia vimada na ndugu.

Kuhusu elimu kwanza pia sidhani kama alikosea. Pengine utekelezaji haukuwa mzuri. Lakini nani asiyefahamu kuwa ccm haitaki wananchi waelimike? Maana wakielimika wataiondoa ccm madarakani asubuhi na mapema. Kwahiyo hapo at least naweza kuona nia njema ya Lowassa.

Sasa hayo siyo maono?
 
Mkuu hata mimi nilikuwa ukurasa mmoja na wewe. Kwani Lowassa ndo Richmond? Usidanganyike mkuu. Issue ya Richmond ilianzia humu JF, lakini ingekuwa amehusika lazima angeshitakiwa, ama hata ushahidi kuwekwa wazi. Hadi usawa huu, kashfa ya Magu kuuza nyumba za serikali ni kubwa kuliko hizo tetesi kuwa EL ni fisadi.

Pia unaposema amekomesha kashfa aina ya Richmond unakosea. Nadhani kipindi hiki kuna nidhamu ya woga tu. Tena unaweza kuta kuna kashfa mbaya kuliko zote zilizopita.

Hata escrow chini ya utawala huu ingefunikwa tu kama kina Lugumi nk. Na wala isingejulikana.

Serikali ya awamu hii huwa ukitoa kashfa hata kama ni kweli inakula kwako, ndo maana whistle blowers kama Tundu Lissu wanaonekana ni maadui wa Taifa. Sasa unategemea nini hapo?

Serikali hii, cha muhimu ni rais akupende tu basi. It's not about the nation, it's about the president and his cronies.

kuhusu nyumba za serikali msikilize mwenyekiti wa chadema kanda ya pwani Mr Sumaye hapo juu anatoa ufafanuzi mzuri tu.

Richmond ni ya Lowassa ilo awezi chomoka, ukitaka ushaidi waulize lissu, mnyika na lema walishasema.ushahidi wanao.

Yani huyo Lowassa ni afadhari mtafute mwingine huyo ni mwizi ata nafsi yako inajua kutopandishwa kizimbani hakumfanyi kutokuwa mwizi wapo wezi wengi tu wa nchi hii awajafikishwa kortini sababu walituibia kwa akili nyingi lakini haiwafanyi kutokuwa wezi.

Magufuli ni kiongozi ni jasiri atatufikisha sehemu nzuri, amethubutu mpaka kugusa eneo la madini pamoja na kumbeza wengi tunaamini kuna matunda tutayaona huko.

Pengine sio mzuri kwenye siasa ndio maana vilio vyenu wengi haswa ni kwenye demokrasia.
 
Mpinzani aliyekuwa serious ni Slaa pekee, ndio mtu aliyekuwa na uwezo wa kusafisha nchi kwa 100% awa kina Lowassa ni bora ata Hashm rungwe.. Magu anafanya kile mlichokililia miaka yote lazima mkubali gharama ya kila mnachoitaji. Mnataka nchi ikae sawa uku mnachekelea tu bila kuwajibika sheinz kabisa.
Slaa ndo alikuja na ile listi ya mafisadi Mwembe Yanga. Kama Lowassa alikuwemo humo, muondoe halafu ndo tuanze kujadiliana kuhusu ukweli wa Slaa kuwa Lowassa ni fisadi. Slaa naye anaweza kuwa victim kama mimi tu. Kwasababu nilijiapiza sitoweza kumpigia kura fisadi. Slaa alikuwa na fikra kama hizo. Kwasababu wana Jf asili humu karibia wote tulilishwa sumu kuhusu Lowassa. Slaa tulikuwa naye humu, wote tukiamini kuwa Lowassa ndo fisadi kuu. Kumbe hata wapi bhana.
 
Hii nchi imefika hapa tulipo si kwasababu ya viongozi tu bali wananchi wengi ambao ni mazuzu kama mleta mada.
Mleta unawakilisha aina ya mazuzu wasiojua nchi ilifika wapi na ilihitaji kiongozi wa aina gani kutuchongea njia tuliyopotea.

Mtu anazunguka misikitini, makanisani vyama mbalimbali vya kijamii kote anamwaga hela,,, akiulizwa anasema eti pesa za marafiki zangu,,,hujiulizi hizo ela angezirudisha vipi!???

Pia yote kwa yote, walioasisi vita ya ufisadi na kupelekea Lowassa kujiuzulu ni CHADEMA. Labda mleta mada ungeuliza je Chadema waliudanganya na kuulaghai umma!????

Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
Usiwe narrow minded na kuwa mtu wa kukariri. Zamani tulidhani rais ambaye ni masikini ndo atatufaa. Wrong, wengi ndo wanatumia nafasi hizo kujitajirisha wao na watu wao. Sasa hivi kuna watu wa Maghufuli ambao hawaguswi na ndo wanafaidi nchi.

Hilo la kumwaga pesa, hata mimi nililifikiri the same like you. Na binafsi ni kwasababu wale marafiki zake waliokuwa wakichangia ni wale ambao pia walitajwa kwenye kashfa. Lakini nimegunduwa tatizo ni ccm, mfumo.

Kwamba tulihitaji kiongozi wa aina gani kututoa tulipokuwa, wengi tulitaka kiongozi mwenye msimamo, mzalendo, asiye muoga wa kuchukua maamuzi magumu , mwenye kuuchukia ufisadi nk. Lakini wengine walijikuta wakiombea laana ya udikteta. Pengine hawa kujuwa wanachotaka.
 
Back
Top Bottom