Lowassa: CHADEMA tutatoa chakula kwa wenye njaa

Lowassa: CHADEMA tutatoa chakula kwa wenye njaa

Chombo cha habari kitakachorusha habari hii ya kichochezi sitosita kukitumbua!
 
Ndio kashaahidi hivyo, kama imekuuma saga chupa unywe
Kuahidi tu sio tatizo kwa sababu hata wewe unaweza kuahidi utawapeleka wanadamu wote mbinguni kama Mungu asipowapeleka. Huwezi kukosa watu wajinga watakaoamini ahadi yako.

Hata ahadi ya Lowassa haiwezi kukosa wajinga watakaoamini.
 
Kama kuna sehemu yenye njaa namuunga mkono lowasa kupeleka chakula hilo tamko alilolitoa kanisani linaendana na Biblia Yesu alisema nilikuwa na njaa mkanilisha kazi ya chama cha siasa ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo halisia ya wananchi. KWA KUTOA UFUMBUZI HALISIA KWA MATATIZO HALISIA ONEKANA KIHALISIA CHADEMA NA LOWASSA HONGERENI Ila MTIMIZE AHADI ZENU TUMIENI HATA RUZUKU KUHUDUMIA WENYE NJAA HALISIA MIMI KAMA MLIPA KODI AMBAYO NI RUZUKU MNAYOPEWA NIKO PAMOJA NA NINYI KWA HILI. TUNATAKA VYAMA VYOTE VITOE UFUMBUZI KWENYE MATATIZO HALISIA. NILIWAPONGEZA HATA ACT WAZALENDO KWA KUSOMESHA BURE BURE WATOTO WOTE KIDATO CHA TANO NA SITA KWENYE HALMASHAURI YAO. HONGERA CHADEMA HONGERA LOWASSA MKIWEZA TAFUTENI HATA PESA ZA KUKOPESHA WANAFUNZI ELIMU YA JUU. MTAUNGWA MKONO NA KILA MTU MIMI NIKIWEMO. TUNATAKA CHAMA CHOCHOTE KITATUE MATATIZO HALISIA YA WANANCHI KEEP UP LOWASSA AND CHADEMA
Kumbuka anayejua kuwa Tanzania kuna njaa au hakuna ni raisi pekee, akitangaza kuwa ipo basi chadema watagawa lakini kama hajatangaza labda chakula mkipitishe chini ya ardhi otherwise huo utakuwa na uchochezi live
 
Kumbuka anayejua kuwa Tanzania kuna njaa au hakuna ni raisi pekee, akitangaza kuwa ipo basi chadema watagawa hicho chakula chao lakini kama haijatangazwa labda chakula mkipitishe chini ya ardhi otherwise huo utakuwa ni uchochezi live
 
Mjumbe wa kamati kuu Chadema, Mhe Edward Lowassa akiwa na mbunge wa Bukoba mjini wameudhuria ibada katika kanisa la KKKT. Akiwa kanisani Mhe Lowassa ametoa kauli.

''Mh rais amesema hatatoa chakula. Mimi nimewasiliana na chama changu tumeona tuwape chakula watanzania. Naamini dunia itasikia'', alisema Lowassa.
Yaani watu wanakufa kwa njaa lakini Makufuri anawakejeli. Ni bora CHADEMA waokoe jahazi.
 
Naunga mkono,huyu mzee alichelewa sana kuingia upinzani,sijui kwanini 2010 wapinzani hawakufikiria kumchukua agombee,anafaa kubakia kama mpinzani na si kuingia magogoni ili kufanya serikali isijisahau.
 
yaaani lowasa akiitisha akaunti ya mchango kwa wana ukawa(cz ukisema watanzania atakabwa koo) kwa ajili ya kununua chakula, walahi ntachangia kwasababu naaamini walengwa watapata chakula...
 
Mjumbe wa kamati kuu Chadema, Mhe Edward Lowassa akiwa na mbunge wa Bukoba mjini wameudhuria ibada katika kanisa la KKKT. Akiwa kanisani Mhe Lowassa ametoa kauli.

''Mh rais amesema hatatoa chakula. Mimi nimewasiliana na chama changu tumeona tuwape chakula watanzania. Naamini dunia itasikia'', alisema Lowassa.
Aaamen ila huo mchakato utafanyiwa fitina mpaka ushindikane
 
Hapa ndipo patamuuuu Waaaoh waaaoh nasikia hadi mwili kusisimka sasa hapa mwendokasi umeingizwa kwenye mtego NA dhubutu yako umropokee Kipenzi cha watu kama ulivizoea kwa maccm wenzako
 
Back
Top Bottom