Lowassa azungumza na wafanyabiashara Dumila leo

Lowassa azungumza na wafanyabiashara Dumila leo

Teeeeeeeeh teeeeeeeeh, watanzania hasa wa kipato cha chini tayari wamesha rejea enzi za miaka ya 80 ya kunywa chai kwa kutumia sukari guru
wakati wa mpito mambo yatakua mazuri tu msikate moyo. nadhani kuna wengine walikua hata hawanywi chai mpaka mwaka jana. Ila uzuri kwasasa wengi wanaonja shubiri ambayo ilikua kwa wachache tu ndipo watanzania wajifunze kufanya kazi kwa uadilifu badala ya blah blah maofisini kwa kutegemea mishahara ya bure bila kazi.
 
Wewe unazungumzia mishahara bila kazi wakati sisi wakulima tunazungumzia kupanda kwa bei ya sukari?tumesha anza kunywa chai ya kutumia sukari guru na asali
 
Hahaha...watu mna madharau!!Aya bhana,ila bila shaka huyu mzee kakuzidi sana..

Kweli amenizidi kwani nchi imekuwa na mawaziri wakuu wangapi toka nchi ipate uhuru? Katuzidi watu wengi pia. Maswali ya kujiuliza je ataondoka duniani akiwa bado katuzidi kama ambavyo Mrema Augustino alivyotuzidi leo hii? Napigana kabla sijafa niwe namzdi kwa kuviacha vipawa vyangu viendelee kuishi kama ambavyo Plato anaishi leo. Kuzidi kwa mtu nako ni superlative kwani Garang, Ghadafi na Sadam Hussein wamekufa wakiwa wanawazidi hata wale 'akina machinga' wanaofukuzwa na mgambo wa jiji kila siku katikati ya jiji? Tafakari.
 
Wewe utaishia kumsema vibaya rais wetu,lkn mwenye macho anaona jinsi huyo rais wenu anavyo fanya kazi kama mtumwa kisa moto wa lowasa alio uona kwenye uchaguzi wa mwaka jana
Wewe punguani kweli rais wa Tanzania ni mmoja tu huyo Lowassa labda rais kivuli.
 
Lowassa is finished!

Huko nyuma Watu walikuwa wanamfuata kila anakoenda lakini kwa sasa yeye ndiye ameanza kuwafuata watu katika maeneo ya kazi zao!

Hakuna cha kudeki barabara wala kushangilia.

Hata Augustino Mrema alipitia njia hii kuelekea kwenye kaburi la kisiasa.

Huko mbele ya safari, kuna uwezekano hata udiwani utakuwa ni shida kushinda.

Ogopa sana Watanzania.
 
Wewe punguani kweli rais wa Tanzania ni mmoja tu huyo Lowassa labda rais kivuli.
Naona hujui hesabu wewe,walio mchagua magu ni 8m,na walio mchagua lowasa wa mujibu wa lubuva ni 6m.sasa tuwache tulio mchagua lowasa tufurahie maamuzi yetu
 
lowassa ni shujaa na ndio rais wangu kura yangu haikupotea bure namkubari sana huyu mzee.
 
Wewe unazungumzia mishahara bila kazi wakati sisi wakulima tunazungumzia kupanda kwa bei ya sukari?tumesha anza kunywa chai ya kutumia sukari guru na asali

Asali na sukari kipi chenye afya bora, kipi chenye gharama kubwa? Wakulima wa Tanzania hawanufaiki na wala hawajanufaika na kushuka kwa bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, ndio maana watetezi wa wanyonge hawa nao wamekomaa tu na bei ya sukari,. Angalau wana jambo la kuongelea kwa sasa, likiisha la sukari ajenda mpya itakuwa imepatikana.
 
Wewe unazungumzia mishahara bila kazi wakati sisi wakulima tunazungumzia kupanda kwa bei ya sukari?tumesha anza kunywa chai ya kutumia sukari guru na asali
Saafi kwa kuanzia, angalau sukari guru inapatikana mkuu. Mvumilivu hula mbivu ila kuna watu hata hiyo sukar guru hawajawahi kuipata. Tatizo letu ni kubwa sana hatueleweki nini tunataka ndiyo maana hata hao tunaowaita viongozi wanatumia udhaifu wetu kututesa.
 
Naona hujui hesabu wewe,walio mchagua magu ni 8m,na walio mchagua lowasa wa mujibu wa lubuva ni 6m.sasa tuwache tulio mchagua lowasa tufurahie maamuzi yetu

Si rahisi mtu kujua vyote duniani, ndio maana wengine hawajui hesabu na wengine hawajui utaratibu wa kidemokrasia.
 
Huyo utakuta hata mlo wa siku kwake ni issue!

ImageUploadedByJamiiForums1462014173.696386.jpg

Si ndio hawa jamaa wenyewe! Halafu huyo ndio anasema "namwonea huruma sana Lowasa" bilalifulu!
 
Back
Top Bottom