Lowassa aweka mambo hadharani: Nitatoa uamuzi

Lowassa aweka mambo hadharani: Nitatoa uamuzi

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Thursday, 14 July 2011


* Lowassa aweka mambo hadharani

JANE MIHANJI, DODOMA na Hamis Shimye, Dar

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amesema atatangaza uamuzi kuhusu nyadhifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati muafaka ukifika. Amesema ameshitushwa na kitendo cha aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, kutangaza kuachia nafasi hiyo na ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.

Lowassa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Muungano, alisema hayo jana mjini hapa, baada ya kutakiwa kutoa maoni kuhusu uamuzi wa Rostam kujiuzulu nyadhifa hizo. "Ninachoweza kusema ni kuwa, Rostam kujiuzulu ni haki yake lakini nimeshituka kuona amejiuzulu na ubunge. Nimeguswa pia na wananchi wake walivyopokea uamuzi huo," alisema.

Rostam akitangaza uamuzi wa kuachia ngazi juzi, alisema amefikia uamuzi huo ili kulinda maslahi ya Chama. Kwa upande wake, Lowassa alipoulizwa ana mpango gani wa yeye kujiuzulu alisema: "Nitazungumza wakati muafaka ukifika." Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kwa upande wake alisema kwa kufuata utaratibu wa kawaida ndani ya Chama, hakina taarifa za kujiuzulu Rostam. Hata hivyo, alisema jambo hilo litazungumzwa katika vikao vya juu vya Chama na baadaye taarifa zitatolewa.

"Chama hakina taarifa yoyote, tumeona kwenye vyombo vya habari ametangaza kujiuzulu kwake akiwa Igunga," alisema Mukama na kuongeza kuwa, CCM bado inalihitaji jimbo la Igunga. Naye mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), jana aliibuka bungeni na kuomba muongozo wa Spika Anne Makinda, akitaka atangaze kuwa jimbo la Igunga lipo wazi. Spika Anne alisema hana taarifa rasmi kuhusu kujiuzulu kwa Rostam, na kama ilivyo kwa wengine ameona habari hizo kwenye mitandao.


"Sisi tuna taratibu zetu, Rostam hajaniandikia barua, tutatoa taarifa wakati muafaka utakapowadia," alisema. Katika hatua nyingine, wanasiasa na wasomi nchini wameendelea kuwa na maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Rostam, wengine wakipongeza hatua hiyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema uamuzi huo ni mzuri ingawa umechelewa.

Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema, alisema Rostam amechukua uamuzi mzuri. "Ni uamuzi mzuri ingawa amechelewa, hasa kutokana na tuhuma zake kuwa za muda mrefu,'' alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hajji Semboja, alisema Rostam anapaswa kupigiwa mfano na wafanyabiashara wengine.


"Ni sawa tu kuondoka, nina hakika CCM haiwezi kuyumba, ikizingatiwa kuwa wameondoka wakongwe kama hayati Julius Nyerere na Mzee Rashidi Kawawa na CCM bado ipo,'' alisema. Alisema CCM ni chama chenye wanachama wengi, hivyo kinachopaswa kufanyika ni kwa wafanyabiashara wengine kujitoa na kuwaachia watu wa siasa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mohamed Bakari, alisema CCM inapaswa kuwa makini kutokana na Rostam kushika nafasi kubwa, hivyo ni lazima alikuwa na wafuasi. "Suala hili ni kubwa na lina faida na hasara, hivyo kinachotakiwa ni kujipanga vyema ili kuepusha matatizo yatakayoweza kujitokeza baadaye,'' alisema.
 
Ameshtushwa na Rostam kuachia Ubunge... Wow
 
Mgombea urais ajaye ajipange mnnoo ku raise 42bil au zaidi maanna mfadhili out gharama zipo pale
 
Lowasa kuachia si rahisi na hana mpango huo .CCM wanaye tu mamvi .Huyu ni shoka lao ana ngozi ngumu na Mukama pale hagusi .Unafiki huu Jamaa kajiondoa na CCM wanasema hawana habari ? Ama kweli CCM ya maajabu .
 
Mgombea wa CCM 2015 ajiandae kupiga kampeni za BMW.
 
Lowassa pia anapaswa kuchukua maamuzi magumu.
Watanzania wanajua,dunia inajua.
 
Huyu mfanyakazi wa hili gazeti mbona maadili sifuli.!!?? Unaiwekaje habari hewani hivi kabla ya kampuni yenye hii habari kufanya hivyo.!!
 
Now who is going to play the game to raise monies for the 2015 election? Manji? Mohamed dewji? Shubhash Patel or 'Ridhiwani'???
 
Lowassa is politically more matured as compared to a neophyte Rostam. He has been in public service for more than three decades, enough time to make a reputable leader. Therefore he will, obviously, not hastily make a resignation move. And as he prepares to contend for 2015 elections, he needs an ample time to gather the essentials a canvasser is supposed to have.
 
Huyu mfanyakazi wa hili gazeti mbona maadili sifuli.!!?? Unaiwekaje habari hewani hivi kabla ya kampuni yenye hii habari kufanya hivyo.!!
Nini Maana ya sifuli??
 
Nasubiri na kikwete ajiuzuru nyadhifa zote alizonazo chini ya ccm hapo ndio nitaamini ccm imedhamiria mabadiliko!!!
 
  • Msishangae Rosta katikisa kiberiti.
  • Msishangae CCM wakamzuia Rostam kuandika baarua ya kuachia ubunge ndani ya mwaka huu
Kujivua magamba ni zoezi linaenda taratibu sana
 
Mzee Ngoyai Lowassa na Kuaminia!Usijiuzulu kwa Chochote mpaka muda wa Cheo Ulichoshika Umekwisha!
Tumia muda wako kuangalia Wapiga Kura wako wanahitaji nini namna ya Kuendeleza Maasae Girlz na Moringe n.k n.k
Wapiga kura wasome na wajikomboe!
Swala la Richmond Halina Mashiko tena!Kwanza ulishatekeleza wajibu wako kwa Kujiuzulu kutokana na Mchezo wa Richmond!
Na toka Umejiuzulu hakuna Umeme wa Uhakika hadi leo!
Komaa Laigwanani Usikubali Kuchezewa,Sifa ya Kiongozi Shupavu na Waziri Mkuu wa Vitendo ipo pale pale!
 
Ni taarifa nzuri,inafanya JF kuwa chanzo kizuri...Walatini wanasema "hic et Nunc"="Here and Now" ....we get the informatn!Lakn in Moral Phlosophy ths z Unethical!hultendei vema gazet na kampuni yako!ungepost ata kuanzia usiku wa kati!kwa namna hii unapngza heshma ya Kampuni,gazeti na Mwandsh husika!...ni mtazamano tu
 
CCM hawajui kama RA kajiuzulu alafu pengine wanasema wao ndio wamesababisha ajiuzulu! Ili uwe CCM unatakiwa kuwa taahira kidogo au uvute bangi.
Futa kauli mkuu kwasababu umemtukana mpaka Rais wa hii nchi
 
Lowasa kuachia si rahisi na hana mpango huo .CCM wanaye tu mamvi .Huyu ni shoka lao ana ngozi ngumu na Mukama pale hagusi .Unafiki huu Jamaa kajiondoa na CCM wanasema hawana habari ? Ama kweli CCM ya maajabu .

CCM hawajui kama RA kajiuzulu alafu pengine wanasema wao ndio wamesababisha ajiuzulu! Ili uwe CCM unatakiwa kuwa taahira kidogo au uvute bangi.
CCM hawajapata barua rasmi kutoka kwa Rostam kama Spika nae hajapata barua ya kujiuzulu kwake haya ni mambo ya kiofisi hata nyie hamwezi simama nje ya mnapofanyia kazi mkasema mmejiuzulu inabidi muandike barua sasa hamjaelewa nini hapo ?
 
Kumbe nae yupo mbioni kujiachia!!haya drama kama kawa!!
 
haya na mkuu wetu aliye mapumziko serengeti amelipokeaje au ndio linamfanya aongeze siku za kupumzika?
 
Back
Top Bottom