Lowassa aweka mambo hadharani: Nitatoa uamuzi

Lowassa aweka mambo hadharani: Nitatoa uamuzi

Mbona kila kiongozi wa Juu wa CCM kama Akina nape na wengine ambao walikuwa mstari wa mbele kutaka magamba yaondoke CCM wamenyewa.
Vikao havishi vya kumjadili mzee wa Igunga, wanatakaa kuzungumzia swala hilo kwa vyombo va habari au kwnaini pia wanachukua muda mkubwa Kukubali ombi lake?
Jee sio ndio huyu aleatikiwa kujivua gamba? jee sio ndio huyu asietakiwa ccm? kwanini wasijitokeze haraka haraka akina nape kujipongeza kwa kazi waliofanya?
 
Hoja hii ni nzuri...nimeipenda.... Ila ishu moja tu ambayo ninadhani wakati unaandika hoja hii hukuifikiria. Je, muda mrefu ni muda mrefu kiasi gani? Je, umefikiria: PALE WEWE BINAFSI UNAPOKUWA UMEFANYA UAMUZI, kuwa huwezi kubadilisha hata kama iwevipi. Bila shaka mara maamuzi yanapokuwa yamefanyika hayawezi kufanywa tena (One a decision has been made it can never be remade). Rostam ameshaamua... CCM hata wakichukua Mwaka, Rostam ameshaamua kama ingekuwa vinginevyo asingetokea na kutoa UAMUZI wake. Ishu hapa siyo chama kutokea na kusema jambo fulani. Ishu ni sisi WATANZANIA kuuchukua uamuzi wa ROSTAM kama ulivyo na kuheshimu uamuzi wake.
 
Ni muhimu awasilishe kwa maandishi uamuzi wake kwa ajili ya kumbukumbu ingawa Naona RA ameamua kuwatosa kimya kimya maana hakupenda kujiuzuru ila kwa kauli yake siasa uchwara za kupakana matope ndizo zilizo mfukuza Kwenye chama chetu dah
 
Lowasa kuachia si rahisi na hana mpango huo .CCM wanaye tu mamvi .Huyu ni shoka lao ana ngozi ngumu na Mukama pale hagusi .Unafiki huu Jamaa kajiondoa na CCM wanasema hawana habari ? Ama kweli CCM ya maajabu .

Mkuu kwa kauli hiyo ya Lowasa nadhani atajiondoa kwenye NEC lakini si Ubunge.
 
Lowassa ubunge ni mali yake haweza kufanya kama Rostam! Hesabu zake ni kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu! anaweza kujitoa tu kwenye NEC
 
CCM hawajui kama RA kajiuzulu alafu pengine wanasema wao ndio wamesababisha ajiuzulu! Ili uwe CCM unatakiwa kuwa taahira kidogo au uvute bangi.
Nakubaliana nawe. Unajua CCM wanafikra potofu sana kuwa hii nchi ni ya wana CCM. Kinachoendelea sasa ni kauli za kinafki kupita maelezo...yuko wapi Nape na Chiligati? Eti mwenyekiti CCM amestushwa na move ya Rostam je aliyekuwa anachair vikao ni nani? Non sense tupu.
 
Chenge yupo safarini kaenda Wingereza, kuangalia kama vijisenti vyake vimeongezeka kwa riba hajawahi kuvigusa taingia mwaka 2000
 
EL kama kweli wewe unataka kujisafisha..hebu tueleze richmond ni dili la nani?..vinginevyo wewe ni fisadi tu..
 
Nadhan ishu si kujiuzulu issue ni kuwa nje ya chama........sasa kama hirizi anayo basi chama kitaendelea kumuitaji
 
Kwani kasema kafukuzwa kwenye chama??????
Ni muhimu awasilishe kwa maandishi uamuzi wake kwa ajili ya kumbukumbu ingawa Naona RA ameamua kuwatosa kimya kimya maana hakupenda kujiuzuru ila kwa kauli yake siasa uchwara za kupakana matope ndizo zilizo mfukuza Kwenye chama chetu dah
 
Niwe mwana JF wa kwanza kumpongeza rasmi RA kujiuzulu katika nyadhifa zote ndani ya CCM , ikiwamo ubunge wa jimbo la Igunga.
Alicho fanya ni kitendo cha kistaarabu kwake binafsi na mwitikio wa wanachama wa CCM pamoja na wapinzani pia.
Ameamua kuondoka badala ya kusukumwa-jumped, not shoved.
Kumpongeza huku hakuna maana ya kupuuza tuhuma zilizopo na zinazomhusu yeye binafsi na kampuni zake za biashara.
Wahenga walisema biashara na siasa ni vitu viwili tofauti kabisa, na imemchukua Rostam muda mrefu sana kulielewa hilo.
Hii ni pamoja na ukweli kuwa kampuni za RA zipo katika karibu kila sekta ya uchumi nchini, iwe mawasiliano(vodacom), usafirishaji(kwa sasa sijayataji), ujenzi(caspian) nk.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mtu masikini akizidiwa, nguvu yake kubwa ni kuzomea tu.
Na ndicho kilichofanyika.
Rostama amekiri kuwa zomea hii inaathiri biashara zake-zingine za kimataifa, kwa hiyo kwa vile biashara ndiyo inamuweka mjini- na siyo siasa , ameamua kuning'iniza joho la siasa.
Kujiuzulu kutapunguza makali ya mashambulizi kwake na kuingia katika phase ya kurekebisha mambo yake kisiasa na kiuchumi.
Kwa hakika Lowassa na Chenge wana mfano mzuri wa kujifunza hapa kabla bahati zao hazijabadilika.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Lowassa: Nimeshtushwa [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 14 July 2011 22:42 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

lowassa%20nimest.jpg
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana, walipotaka kujuwa maoni yake juu ya uwamuzi wa Rostam Aziz kujiuzuru nyazifa zake za Ubunge wa Igunga na Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM. Picha na Edwin Mjwahuzi

Leon Bahati, Dodoma, Ramadhan Semtawa, Dar
WAKATI uamuzi wa Rostam Aziz kung'atuka ubunge wa Igunga na ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ndani ya chama chake cha CCM ukiibua gumzo kubwa karibu kila kona nchini, mshirika wake mkubwa kisiasa, Edward Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli ameeleza kushtushwa na tukio hilo.Juzi, Rostam, mmoja wa watu muhimu ndani ya CCM aliyeshiriki vyema katika mtandao uliomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005, alitangaza uamuzi mzito wa kung'atuka siasa akipinga kile alichokiita siasa uchwara za baadhi ya viongozi wake.Uamuzi huo mzito wa Rostam uliibua kwikwi na vilio kutoka kwa wapigakura jimboni kwake Igunga, wakiwamo wale waliomchagua kwa vipindi vitatu mfululizo tangu mwaka 1994 ulipofanyika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Charles Kabeho. Jana, Lowassa alisema: "Kwa kweli nimeshtushwa, nimesikitishwa...kilichonishtua zaidi ni vilio. Namna wananchi wa Igunga walivyokuwa wanalia na kusikitika."

Hata hivyo, Lowassa ambaye naye amekuwa akitajwa katika orodha ya watu watatu wanaopaswa kuachia nafasi zao za uongozi CCM katika kile kinachoitwa chama kujivua gamba, alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kufuata njia ya mshirika wake huyo alijibu: "Siku ikifika nitatoa uamuzi na nitajibu wakati ukifika."

Lowassa alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kuhusu alivyopokea uamuzi huo wa Rostam na kama yuko tayari kufuata mfano na njia hiyo ya kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya CCM.
Lakini, juzi Rostam aliweka bayana kwamba uamuzi wake wa kujiuzulu hautokani na shinikizo lolote ikiwamo kile kinachoitwa mpango wa kujivua gamba, bali aliufanya uamuzi huo kuepuka kuathiri biashara zake kutokana na kuchafuliwa na siasa uchwara akieleza kuwa yeye ni mfanyabiashara wa kimataifa, lakini akaahidi kuendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM.

Hata hivyo, Lowassa jana hakutaka kufafanua kuhusu kauli yake hiyo ya "Nitajibu wakati ukifika," ingawa alionyesha tabasamu wakati akiulizwa na kujibu swali hilo la iwapo atafuata nyayo za Rostam au la.
Mshirika wao mwingine, Andrew Chenge, jana alivumishiwa kuandaa mkutano na waandishi wa habari ili naye atangaze uamuzi wa kujiuzulu nafasi zake zote kama hatua ya kutekeleza azimio la Nec la kujivua gamba.

Lakini, alipotafutwa kwa simu na kuulizwa kuhusu taarifa za yeye kutaka kujiuzulu, Chenge alijibu kwa kifupi kuwa alikuwa Uingereza, kitu kilichothibitisha kuwa hakukuwa na mpango huo wa kujiuzulu huku akisisitiza: "Mimi niko nje ya nchi, nipo Uingereza."

Hivi karibuni, Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi, maarufu kama Mzee wa Vijisenti, aliwahi kuliambia gazeti hili: "Sijui kama mimi ni gamba CCM," huku akisisitiza kwamba anaheshimu taratibu za chama na asingeweza kukurupuka na kuanza kuzungumza mambo ya chama nje ya utaratibu.
Chenge alisema chama kina utaratibu wake wa kufanya maamuzi, hivyo kuanza kutoka nje ya taratibu na kuzungumzia mambo ya ndani ya chama isingekuwa rahisi kwake kwani anaheshimu taratibu zilizopo.

..Sendeka asifu ujasiri wa Rostam
Kwa upande wake, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole-Sendeka, ambaye amekuwa akijipambanua kama mpambanaji wa ufisadi, alisema kujivua kofia zote alizokuwa nazo Rostam ni kitendo cha kuletea afya chama tawala.Sendeka alifafanua kwamba kuwapo kwa vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa ndani ya CCM ni sawa na mtu anayeugua na ili apone lazima waondoke ili chama kipate afya njema.

Alisema kutokana na sababu hiyo, anamuunga mkono Rostam kwa uamuzi wake aliochukua wa kutii uamuzi wa chama wa kujivua gamba, kwani ni hatua moja ya kukiboresha chama na kuongeza: "Unaposhauriwa kwa afya ya chama chako na ukakubali ni uamuzi wa kijasiri."
Hata hivyo, alionya kwamba mkakati huo wa kujivua gamba ni zaidi ya vigogo watatu ambao wamekuwa wakitajwa mara kwa mara.Sendeka alisema wote wakifuata mkondo wa Rostam, chama kitajijengea taswira nzuri ya kupendwa na watu ambao tayari wameanza kukata tamaa kutokana na kuona haya kutokana na tuhuma zinazowahusu.

Kuhusu wale ambao bado hawajatekeleza hilo, ole-Sendeka alisema: "Cheo ni dhamana, uongozi ni utumishi, kama wale waliokupa dhamana wanakushauri uondoke, huna haja ya kubishana, tekeleza."Naye Ally Mohamed (Nkasi Kaskazini-CCM), alisema amefurahishwa na hatua ambayo Rostam ameichukua kwa lengo la kusafisha chama.
Lakini, akasema ni wakati mwafaka wa kuhakikisha CCM inasafishika mbele ya Watanzania kwa sababu, kuwapo kwa watuhumiwa hao wa ufisadi wanaozungumzwa mara kwa mara, kulionekana kuchafua chama chote."Sasa ni wakati wengine nao wachukue uamuzi kama huo. Tunajua wako wengi, waondoke chama kiimarike," alisema Mohamed.

Tundu Lisu azungumzia uamuzi wa Rostam
Tundu Lissu (Singida Mashariki-Chadema), alisema bado gamba la CCM halijavulika kwa sababu Rostam ni mmoja wa watuhumiwa 11, ambao walitajwa na Chadema kwenye orodha ya mafisadi, Mwembeyanga, Temeke mwaka 2007.

"Bado kumi," alisema Lissu huku akijigamba kuwa mafanikio hayo ni juhudi zilizofanywa na Chadema ili kulinda rasilimali za Watanzania ili zitumike vizuri.

Kuhusu kauli ya Rostam kuwa amejing'oa kwenye nyadhifa zake kutokana na "siasa uchwara", Lissu alijibu: "Kama kweli siasa uchwara ndizo zimemwondoa Rostam, basi ndizo zinazofaa kuendelezwa hapa nchini."

 Ingawa Rostam alikataa kuhusisha uamuzi wake na kujivua gamba, tangu kikao cha Nec cha Aprili, Sekretarieti mpya ya CCM imekuwa ikitangazia umma orodha ya makada wake watatu ambao wanapaswa kujiuzulu ili kuleta kile inachokiita heshima kwa chama na kukisafisha.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Hapo ndio ujue wanasiasa wetu ni wasanii tu anastuka na nini wakati yeye juzi kasema tufanye maamuzi magumu
Nilitegemea Lowassa aseme kitendo cha kujiuzulu kwa RA ndiyo maamuzi magumu anayotaka serikali ifanye badala yake anastushwa.
 
CCM hawajui kama RA kajiuzulu alafu pengine wanasema wao ndio wamesababisha ajiuzulu! Ili uwe CCM unatakiwa kuwa taahira kidogo au uvute bangi.
OOh unamaana ccm wote ni mataahira au wavuta bangi????
 
Kwa hiyo inavyoonekana yeye binafsi hana mpango wa kujiuzulu!!
 
Lowasa wewe ni mzawa usikubali kabisa kuachia ngazi kwani hao wanaokuambia uachie ndiyo wamekuchagua? Wewe komaa nao hivyo hivyo tu usikubali kuyumbishwa na watoto wadogo kina Nape, kwanza hawajui wewe umewekeza kiasi gani katika siasa za nchi hii, ulijitosa katika dili chafu kukwapua mihela ili mkale kuku leo baba Rizwan anakuchenjia usikubali baba.Hawa wepesi tu wasikubabaishe kama kung'oka basi aanze baba Riz.
 
Lowassa is politically more matured as compared to a neophyte Rostam. He has been in public service for more than three decades, enough time to make a reputable leader. Therefore he will, obviously, not hastily make a resignation move. And as he prepares to contend for 2015 elections, he needs an ample time to gather the essentials a canvasser is supposed to have.

May be one thing which mkight not be aware is that Lowassa, with all his maturity in politics, has been 'made' by RA
 
Back
Top Bottom