Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.

Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo
utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi.

Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)

Kwa hiyo wewe ndiye Msemaji wake au?
 
samahani naomba kukumbushwa noti ya miatano ina rangi gain vileee?
 
Yani watu wameamua kumtabiria hizi mambo mapema sana, msimlazimishe ajihusishe na mambo ya siasa mpaka muda wa adhabu yake uishe.
 
Lowasa unatumia mno pisa kushawishi viongozi wa ccm iliuteuliwe kugombea urais kwa tiketi ya ccm pia una mwaga hela kwa vijana wenye njaa ili wakuunge mkono.hiyo ndiyo sms yake na bado watato umelalia noti ya elfu kumi kitandani kwako subiri
si lazima awe rais wa tanzania kupitia ccm. muhimu ni kura za wananchi.
 
TAMKO KULAANI MATENDO YA KIKUNDI VYA WATU KWENYE MITANDAO YA JAMII........Imetolewa na ofisi ya Mh Lowassa(mb)

Machi 7, 2014

- ha! ha! ha! unajua siku ya kifo cha nyani miti yote hutelezzaaaaaaaa! ha! ha! ha!, sasa mmeanza kuikana mitandao yenu wenyewe kweli makubwa sana haya!! duh!!

Le Mutuz
 
Ajisafishe kwanza!! Hivi hao marafiki zake wa kihindi wanaochanga fedha na kumpatia azigawe makanisani, miskitini na makundi ya vijana na akina mama wana nia gani na nchi hii? Yeye akiwa rahisi atarudishaje kwa hawa watu? Tunahitaji mfia nchi si mfia kundi la watu wenye nia ya kuichuma na kuifilisi nchi hii.
 
Ajisafishe kwanza!! Hivi hao marafiki zake wa kihindi wanaochanga fedha na kumpatia azigawe makanisani, miskitini na makundi ya vijana na akina mama wana nia gani na nchi hii? Yeye akiwa rahisi atarudishaje kwa hawa watu? Tunahitaji mfia nchi si mfia kundi la watu wenye nia ya kuichuma na kuifilisi nchi hii.


Hayo makundi unayoyadharau na kuwaona kwamba ni wajinga wanapoamua kumuita Lowassa atumie ushawishi wake kuhamasisha matamasha yao ya kuinua miradi yao unawakosea ubinadamu. Suala la kama Lowassa atapata urais au atakosa halina uhusiano wa kuchangia au kutochangia shughuli za jamii.Cha msingi ni kwamba wananchi wanahitaji watu wenye uwezo wabust shughuli za maendeleo.
Mimi nashangaa mpaka leo hii mtu anasimama na kusema huyu anayechangia maendeleo akipata urais hizo pesa atazirudishaje? Kwa nini tusiseme akikosa atawadai aliowachangia? Kwani kuna mahali aliweka mkataba wa kupewa kura?
Hata ukienda kuomba kazi kwenye benki mara nyingi wanataka uwe na mdhamini mwenye title fulani kama sio fedha.
Hivi ingekua ni busara Lowassa kikundi fulani kimuombe aje aongoze tamasha halafu yeye aseme sitakuja kwa sababu sitagombea urais. Hata enzi za marehemu mzee wetu Nyerere alikua anapokea misaada toka nchi yoyote kama hapakua na masharti.
 
Kweli mkubwa, hawa wanaoongea wameshindwa hata kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi.
 
Hivi unafikiri mwasisi wa Taifa la Marekani aliwaza au hata kuhisi kwamba mtu mwenye asili ya Afrika atakuja kuwa Rais wa Taifa kubwa na lenye nguvu kama Marekani?
Watu na Wakati ndivyo vinavyoamua nani awe rais kwa wakati husika sio mizimu.
Kwa taarifa yako kundi la Nyerere lilishondwa vibaya sana tangu wakati wa kumtafuta mtu wa kumrithi mwaka 1985 pale alipomtaka Salm A Salm na badala yake wazanzibar makini wakagoma kuburuzwa na mtu alyeshindwa kusimamia uchumi wa tz na kuvuruga uchumi wa Zanzibar baada ya karume kufa.
Ilipofika awamu ya tatu hiyo ndo iliamua kumaliza kabisa kama Alivyotoboa live Vincent Nyerere kwenye kampeni kule Arumeru.
Naamini hata hawa wanaomtaja Nyerere kama mungu wa kuwachagulia viongozi ni wa nafiki tu wanaotafuta madaraka huku wakisahau kua Nyerere hafai kuwa mfano kwenye suala la uchumi.Nyerere alitumia umaarufu wake kuwazimisha viongozi na wazalendo wa kweli ,watu waliokuwa na maono ya mbali ya kuondoa umaskini.Kwa nini tusiwaenzi akina Horace Kolimba, Abrahaman Babu, Abdu Jumbe Mwinyi,Kambona. Walipoteza nyadhfa na maisha yao kwa kukataa unafki na kuwa wakweli.

Tukizungumzia swala la Uzalendo unadhani kuna mtu ameweza kuwa mzalendo kwa vitondo kama Nyerere ukilinganisha na nafasi yake? Labda Sokoine. Ebu angalia sasa hawa watoto wa marais wetu wanafanya biashara za madawa za kulevya na Nyara za Serikali na wazazi wao wanaiweka nchi rehani kwa kuwagawia wageni rasili mali zetu kwa ajili ya kuokoa familia zao kwa upumba.vu wa kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya. Kiukweli inaumiza sana, labda mwenzangu huguswi na hili.
 
Mbun'go nakuaminia! Ww shibwe una ushahid wa unachosema au aljmrad na ww umeandika?
 
Kweli mkubwa, hawa wanaoongea wameshindwa hata kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi.



Na hii mitazamo hasi dhidi ya kuchangia maendeleo ya wananchi ndio itakaosabsbisha hivi vyama vya upinzani kikosa ridhaa ya wananchi ya kuongoza nchi.
Hivi kweli unaenda na helkopta kuomba kazi ya ubunge yenye mshahara na posho za kumwaga halafu unaona wananchi wanakunywa maji machafu pamoja na ng'ombe ,wewe unashindwa kuwachimbia kisima cha kudumu cha milion kumi kisaidie kinamama na watoto wanaoteseka kutafuta maji kila siku cha kusikitisha unawaambia kwamba wewe hauhusiki hiyo ni kazi ya serikali halafu unawomba hiyo ajira nono ya ubunge au urais.
Kwa nini usiende na bajaji kama mtikila kuonyesha kwmb wewe ni mlala hoi mwenzao.?
Hata nabii Issah au Bwana Yesu alipoona watu kule kana wameishiwa Divai aliwapa nyingine ili kunuduru sherehe isiharibike.
 
na walaaniwe kabisa we mpaka uwe rais bwana hata mungu analijua hilo.
 
Ofisi ya Mbunge mheshimiwa Edward Lowasa imelaani kitendo cha baadhi ya watu ktk mitandao kuchapisha noti ya Tsh 500 yenye picha ya Lowasa.

Mimi naita hizi ni fujo za ushabiki na zinaweza kumuharibia Lowasa SAFARI YAKE YA MATUMAINI aliotangaza kuianza miezi michache iliyopita.
 
Ndio hivyo amejionesha mapema, nami nimeiona hiyo utazani noti ya kweli.

Kuna mdada nilimsoma kwa blog moja, anasema alikuwa na shida ya kumsomesha mdogo wake, so akamuomba msaada Lowassa nadhani simuni, akajibiwa kuwa "mimi nasomesha watoto wa Monduli tu".

Kwa hiyo ni kweli anapoenda huku na kule ni kutaka uraisi tu. Haya mie nisie na chama yangu macho.
 
Back
Top Bottom