Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Ina maana printing unit ni ileile iliprint t shirts?
 
POLE SANA MZEE......Lakini wewe si fisadi tu kwa hiyo hatuwezi tukakushangaa tukiona umeamua kutengeneza notihiyo. Jirekebishe mzee na urais hutaupata ng'o kupitia CCM labda uende chama kingine. CCM tunataka wanachama safi ndio wagombee urais
Safi kama Ridhiwan Kikwete muuza madawa
 
Nyerere alimulani Lowasa na hatakuwa raisi wa nchi hii hata atubu yerusalem mwambieni auze mali zake zote na zile nyingi alizowaibia watanzania awagawie masikini ili apate kufunguliwa mbinguni ila hapa duniani akiwa raisi wa tz nahama nchi siongozwi na mwizi mimi!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu mbona hata huyu mwenye kudondoka majukwaani,kichwa nazi naye alikataliwa? Nchi hii tuna laana tu kwa kukiuka maneno ya wafia nchi kama J.K.NYERERE.Na kibaya zaidi hatutaki kubadilika.
 
Mkuu mbona hata huyu mwenye kudondoka majukwaani,kichwa nazi naye alikataliwa? Nchi hii tuna laana tu kwa kukiuka maneno ya wafia nchi kama J.K.NYERERE.Na kibaya zaidi hatutaki kubadilika.



Hivi unafikiri mwasisi wa Taifa la Marekani aliwaza au hata kuhisi kwamba mtu mwenye asili ya Afrika atakuja kuwa Rais wa Taifa kubwa na lenye nguvu kama Marekani?
Watu na Wakati ndivyo vinavyoamua nani awe rais kwa wakati husika sio mizimu.
Kwa taarifa yako kundi la Nyerere lilishondwa vibaya sana tangu wakati wa kumtafuta mtu wa kumrithi mwaka 1985 pale alipomtaka Salm A Salm na badala yake wazanzibar makini wakagoma kuburuzwa na mtu alyeshindwa kusimamia uchumi wa tz na kuvuruga uchumi wa Zanzibar baada ya karume kufa.
Ilipofika awamu ya tatu hiyo ndo iliamua kumaliza kabisa kama Alivyotoboa live Vincent Nyerere kwenye kampeni kule Arumeru.
Naamini hata hawa wanaomtaja Nyerere kama mungu wa kuwachagulia viongozi ni wa nafiki tu wanaotafuta madaraka huku wakisahau kua Nyerere hafai kuwa mfano kwenye suala la uchumi.Nyerere alitumia umaarufu wake kuwazimisha viongozi na wazalendo wa kweli ,watu waliokuwa na maono ya mbali ya kuondoa umaskini.Kwa nini tusiwaenzi akina Horace Kolimba, Abrahaman Babu, Abdu Jumbe Mwinyi,Kambona. Walipoteza nyadhfa na maisha yao kwa kukataa unafki na kuwa wakweli.
 
Sitaki kuamini kuwa mzee EL ni msahaulifu sana!
Ni siku chache tu alisema hahusiki na wanao post kwa jina lake,lakini anafurahi kuwa anakubalika.
Leo wanafanya mengine,anaanza mayowe,..
Debe tupu,haliachi kutika!
 
IKumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.

Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo
utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi.

Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa ( MB )


source : http://www.wavuti.com/2014/03/taarifa-ya-ofisi-ya-lowassa-kuhusu-noti.html?m=1
 

Attachments

  • 1394396563897.jpg
    1394396563897.jpg
    12.5 KB · Views: 420
Pamoja sana. Mbona hajatangaza dau kwa mtu aliyetengeneza noti hiyo?
 
Dah... angejiweka hata kwenye buku 5 bas... lakin jero!!!
 
Hii note haifai hata kununualia sumu ya panya!
 
Naona mnaendelea KUKITEMBEZA KIBAYA,wakati siye tunaendelea KUUZA KIZURI!

Peopleeeees Poweeeeeeer!
 
Back
Top Bottom