Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,628
Reaction score
6,816
TAMKO KULAANI MATENDO YA KIKUNDI VYA WATU KWENYE MITANDAO YA JAMII

Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mh Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.

Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi Mia tano yenye picha ya Mh Lowassa. Kitendo hicho siyo Utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za utaifa na mamlaka ya nchi.

Mh Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mawasiliano kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.

Imetolewa na ofisi ya Mh Lowassa(mb)

Machi 7, 2014
 
Khaaa pole MZEE ila usikute ni wale vijana amabao hawataki shughili zaidi ya kukupigia debe LA 2015
 
Hata mimi nakemea hiyo tabia!

Asubuhi saa tano na nusu kuna mtu kaposti uzushi kuhusu mheshimiwa Lowassa kwa ID ya Filipo, nawashukuru Mods maana baada ya dakika kama tano post hiyo iliondolewa! Lakini ilishaleta mtafaruku hapa ofisini na watu wengine kutaka kuzimia! Mods watu kama hawa wafungiwe milele! Na kwa kweli walaaniwe, kumzulia kifo binadamu mwenzio wala sio tabia njema kabisa, kwamba wewe utaishi milele?Nachukia sana habari za kizushi, wenye tabia hiyo mkome!

Tulieni, kama hamyawezi mapigo yake!
 
Last edited by a moderator:
Wanaomzushia EL walaaniwe wao mpaka panya wa majumbani kwao
 
Lowasa unatumia mno pisa kushawishi viongozi wa ccm iliuteuliwe kugombea urais kwa tiketi ya ccm pia una mwaga hela kwa vijana wenye njaa ili wakuunge mkono.hiyo ndiyo sms yake na bado watato umelalia noti ya elfu kumi kitandani kwako subiri
 
Hiyo siyo STYLE ya Lowassa. Lowassa ni SIMPLE but tough in Action. CCM wanam-feel kwa ukweeli.

Dua la Kuku......
 
Last edited by a moderator:
Lowasa unatumia mno pisa kushawishi viongozi wa ccm iliuteuliwe kugombea urais kwa tiketi ya ccm pia una mwaga hela kwa vijana wenye njaa ili wakuunge mkono.hiyo ndiyo sms yake na bado watato umelalia noti ya elfu kumi kitandani kwako subiri

mbna unalalamika,si ufnye kaz upate hela
naona kama unamlalamikia lowassa mlaumu mzaz wako
 
Huku ni kukanusha au kujipa promo kuwa ametoa noti ya jero.
 
Watrace origin ya hiyo picha culpit atapatikana
 
hao watakuwa friends of...... tz aka el wachunguzwe
 
hii mambo ya kulaani yalimgharimu jamaa wa mwandiga.
 
Back
Top Bottom