Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Lowassa awalaani wanaomzushia mambo kupitia Mitandao ya Kijamii!

Kwa Mujibu wa Mtangajazi wa Kipindi cha power breakfast cha Clouds FM bwana Gerald hando, kahabarisha tutamsikia EL akijitete muda si mrefu ujao noti ya jero sio yake

tune in, tumsikie
 
Kwa Mujibu wa Mtangajazi wa Kipindi cha power breakfast cha Clouds FM bwana Gerald hando, kahabarisha tutamsikia EL akijitete muda si mrefu ujao noti ya jero sio yake

tune in, tumsikie

noti ya jero?
 
That is very low for him! Jamaa amechoka sana!
 
Chadema wanajilagai wenywewe check hii receipt wanajiandikia tu wanakuja mitandaoni, hawajui hata kudanganya mpaka tarehe wanashindwa kuandika, hii ni ofisi kweli??? Na tukiwapa nchi, hizi reciept si zitachakachuliwa namna hii
 
Post deleted
Paw

- ha! ha! ha! ha! umbeya kama huu wako si ndio tabia ya wakuna nazi naona umeamua kujisema mwenyewe who you are, ha! ha! ha! ha! sasa mmeanza kuikana mitandao yenu wenyewe yamewafika shingoni sasa! ha1 ha! ha!

Le Mutuz
 
TAMKO KULAANI MATENDO YA KIKUNDI VYA WATU KWENYE MITANDAO YA JAMII

Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mh Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.

Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi Mia tano yenye picha ya Mh Lowassa. Kitendo hicho siyo Utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za utaifa na mamlaka ya nchi.

Mh Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mawasiliano kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.

Imetolewa na ofisi ya Mh Lowassa(mb)

Machi 7, 2014
Huyu mmasai haki ya nani watamzushia kila kitu daah mpk huruma achane na siasa uchwara kama Rostam.Mwenzake kaelekeza nguvu kuwa bilionea namba 1 Tanzania.
 
Chadema wanajilagai wenywewe check hii receipt wanajiandikia tu wanakuja mitandaoni, hawajui hata kudanganya mpaka tarehe wanashindwa kuandika, hii ni ofisi kweli??? Na tukiwapa nchi, hizi reciept si zitachakachuliwa namna hii
Wizi wa Chadema ni Zaid ya CCM
 
hata issue ya Lowasa lazima CDm waingizwe ili iwa hata wao..ndio kuikoa CCM.akili za mizoga hizi
 
Hayo makundi unayoyadharau na kuwaona kwamba ni wajinga wanapoamua kumuita Lowassa atumie ushawishi wake kuhamasisha matamasha yao ya kuinua miradi yao unawakosea ubinadamu. Suala la kama Lowassa atapata urais au atakosa halina uhusiano wa kuchangia au kutochangia shughuli za jamii.Cha msingi ni kwamba wananchi wanahitaji watu wenye uwezo wabust shughuli za maendeleo.
Mimi nashangaa mpaka leo hii mtu anasimama na kusema huyu anayechangia maendeleo akipata urais hizo pesa atazirudishaje? Kwa nini tusiseme akikosa atawadai aliowachangia? Kwani kuna mahali aliweka mkataba wa kupewa kura?
Hata ukienda kuomba kazi kwenye benki mara nyingi wanataka uwe na mdhamini mwenye title fulani kama sio fedha.
Hivi ingekua ni busara Lowassa kikundi fulani kimuombe aje aongoze tamasha halafu yeye aseme sitakuja kwa sababu sitagombea urais. Hata enzi za marehemu mzee wetu Nyerere alikua anapokea misaada toka nchi yoyote kama hapakua na masharti.

Very poor analysis na mbaya zaidi hujui kilichopo ndani ya chungu. Nyerere alikuwa tofuti sana na viongozi wa sasa na huezi kumliganisha na kiongozi kama Lowassa hata chembe. Hakuna kitu kibaya kama ukiwa unafikiri uko kwenye mwanga wakati giza ni nene. Kama hujui wahindi wanachagua mpaka mawaziri nchi hii kutokana tu na walichotoa kwenye uchaguzi usingeandika haya. Fuatilia mambo kwa makini.
 
Kwani aliyechaguliwa na wahindi ni nani?
Mwinyi alichaguliwa na Nyerere.
Mana Mkapa alichaguliwa na Nyerere
Kikwete pia ni kutokana na uchaguzi wa mwalimu kwani alimwambia asubiri awamu nyingine kwa hiyo yeye ndiye aliyemfanya kikwete apite kwa urahisi kwa sababu alikua ameshakaa kwenye vichwa vya watu kwa ile imani ya zidumu fikra za mwalimu.Hakushindwa kumwambia kwamba wewe hufai.
Mpaka hapo hamna muhindi anayechagua rais hivyo hata mawaziri watatokana na matakwa ya rais na waziri wake mkuu.Dunia nzima wahindi wapo na ni wa oga sana wanapokuwa nje ya India.
Mimi sio mwanasiasa na sioni sababu ya kuwa mtumwa wa kusifia tuuuu mzimu wa Nyerere.Ndio unafiki mnaofanya nyie wanasiasa kila mtu anamtumia Nyerere kama daraja lake kwa kumtakasa na kumuweka mbali na sababu ya umaskini wa nchi hii.Matatizo ya nchi hii sio wahindi wala wanasiasa peke yao ni jamii nzima ina roho na pepo mchafu wa ufisadi kuanzia kwenye familia.
Mtu anamwagia shehe tindikali,padri anapigwa risasi,wakulima na wafugaji wanakatana mapanga,watu wanabambikiwa kesi,CDM na CCM wanaunda vikundi vya kukatana mapanga, wanataka kuleta yale ya Zanzibar kwa sababu ya njaa ya madaraka na wala sio umaskini wa wananchi.Haya sio matatizo yanayoletwa na wahindi.
Najua mazuri mengi sana ya Nyerere lakini sitaki kuamini kwamba yeye hakufanya mabaya kama wanasiasa wengine. Na eti waliomfuata wooote walifanya mabaya tuuu hivyo tunahitaji mtu mwenye mawazo na fikra kama za mwalimu ili tusonge mbele;siamini katika hilo.
 
Back
Top Bottom