Lowassa ashangazwa mikutano ya kisiasa kuzuiwa; sasa kutumia mitandao ya kijamii kuhutubia wananchi

Kiwango chako cha upumbavu kimepitiliza,yaani utumwa wa fikra sababu ya tumbo umekufanya uwe kama ndondocha!kachukue buku 7
 
Buku7 mmeamua kuwa wasemaji wa cdm....
Baada ya kuukosa UDC.....
Safi sanaaa keap it up
 
Hapo ni ukweli mtupu, acha utahaira wewe
Hv unajua unachoshabikia?Toka lini vikao vya CDM vya ndani vikanyika hadharani?
Hamuelewi maana ya upinzani!Siku Ccm mkiwa wapinzani ndio mtaelewa!
 
Hawa jamaa janja janja sana, wakipewa ruzuku wanaongeza wanawake kwa kutegemea wakikamata DOLA Ofisi za Chama cha CCM zitakua zao. Ni Sawa na FISI anasindkiza Mlevi akitegemea mkono Utadondoka.
Ha ha ha ha!
 
CDM wasipokuwa makini na kauli za viongozi wao waandamizi, kile kilichotokea USSR 1990's kwa kauli Mikael Gorbachev kitaikumba CDM.
CDM wakubali kubadilika wao kwanza kwa kusuka upya safu za uongozi kuanzia tawi hadi Taifa ,ikiwezekana wafanye hivyo mapema ili kuendana na kasi iliyopo.
 
Tuliyokuwa tunayasikia toka kule Rwanda sasa yamehamia Tanzania. Chama tawala kinaruhusiwa kufanya mikutano, wapinzani NO! Kudadadeki, mkiitwa madikteta mnachukia. Serikali hii ina utofauti gani na ile ya Rwanda?
 
Wakati akiwahutubia Madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha, Edward Lowassa alisema kile alichokiita CHADEMA KUHITIMU(TO GRADUATE) harakati na kukitaka chama hicho sasa kufanya siasa za kunuwia kushika dola na kuachana na Uanaharakati.
Naungana kabisa na kauli ya Lowassa kwani historia ya vyama vingi duniani kote inaonesha ni vyama vichache sana (ama hakuna kabisa) vilivyofanya siasa za aina ya CHADEMA vilivyofanikiwa kushika dola.

Inawezekana kabisa Lowassa anajua sababu za chama chake kufanya siasa za kiharakati lakini naye kwa makusudi kabisa akaamua kudhani ni sababu moja tu.

Moja ya sababu kubwa ambayo inaweza kusababisha aina hii ya siasa ni KUKOSA MAHALI pa kudumu pa kuweza kufanyia siasa na kuachana na harakati. Naongelea OFISI ZA CHAMA kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa. Hapana ubishi kwamba CHADEMA kinaelekea kuvuka ngazi ya SACCOS na kuwa taasisi kubwa. Kwa maana hiyo haitegemewi kabisa maamuzi ya Taasisi yakatoka kwa Lowassa, Mbowe, Lissu na Mashinji. Hata kuamua kufanya au kitofanya migomo na maandamano , lazima uamuzi utoke kwa wengi, siyo suala la ama Mbowe, ama Lowassa kuamua.Swali ni WAPI SASA WATU HAWA WATAKUTANA KUFANYA MAAMUZI YA WENGI? Ni kinondoni mtaa wa UFIPA?

Tayari Mbowe ameshatoa tamko la kuwataka vijana wa BAVICHA kusitisha azma yao ya kwenda Dodoma kufanya kile walichokiita kusaidia jeshi la polisi kuzuia MKUTANO WA NDANI wa CCM kwa madai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli alishaikataza kufanyika hadi 2020. Sababu alizozitoa Mbowe ni mufilisi kabisa eti wana taarifa watapigwa na polisi, mbona walisema hawaogopi Polisi? Eti wao hawana nia ya kupambana na polisi ila walitaka tu dunia ijue, kwa hiyo hawakuwa na hoja ila walikuwa wanajionesha tu kama bidhaa kwenye mabanda ya Sabasaba? Nimemdharau Mbowe.

Wajumbe wa CCM katika mkutano huo ni zaidi ya 500 lakini unafanyika ndani ya majengo yanayomilikiwa na CCM( Ni mali ya CCM). Leo Chadema wakifanya mkutano wao wa aina hiyo nao wauite MKUTANO WA NDANI? NDANI wapi wakati wanafanyia Mlimani City na Serena Hoteli huku kumbi hizo zikiwa zimezungukwa na wafuasi wakiwa na mabango na nyimbo za kukabiliana na vyombo vya dola.
Ndiyo maana wanalazimika kutumia viwanja vya Mashujaa, SOWETO, TANGANYIKA PAKERS n.k kufanya mambo yote kwa pamoja(mikutano ya ndani, harakati na chaguzi za chama chao).
Ni wakati Muafaka sasa Lowassa kujikuna zaidi ili kufanikisha Chama chake kuachana na siasa za Kiharakati kwa sababu ndogo tu ya kukosa ofisi
Vijana wa CDM kutishia kwenda Dodoma ilikuwa ni strategy tu ya kuufanya umma utambue maamuzi ya upendeleo ambayo Polisi wao wanayafanya, hivyo kumdharau Mbowe kwa kauli yake hiyo si sahihi labda kwa maoni yako tu. Mengine uliyoandika uko sahihi kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom