Lowassa ashangazwa mikutano ya kisiasa kuzuiwa; sasa kutumia mitandao ya kijamii kuhutubia wananchi

Akili za matope shiiida. Hata ilani ya uchaguzi ilikuwa kwa mtandao.
Anajifurahisha asikike
 
Bavichaaa wanahaha kutafuta mbinu za kumfanya Lowasa aanze kuwachangia tena baada ya ukata kuwakumba..

Lkn EDO alishawashitukia , mlimdanganya sana kwamba anakubalika na mna kura million 10, mkamtengenezea hadi picha za mafuriko feki ili kuyaponda mabilioni yake .!;
Lkn sasa Mzee amewagunndua nyinyi majizi ,EDO hatawapa hela tena, tafuteni kazi halali za kufanya ili mpate hela na siyo kushinda kwenye mitandao ya kijamii kujipendekeza kwa mwanaume mwenzenu !!!
mrija wa buku 7 saba umekata nini mbona povu hivyo
 
Naona mleta Uzi umeamuwa kuwa shekhe yahaya,ulicho kileta humu ndani hakiendani kabsa na kichwa cha habari.ila hupaswi kulaumiwa unatetea buku Saba yako
 
Mzee kawasaidia kuongeza wabunge na kuichachafya CCM halafu leo mnaibuka na kusema kaja kuua upinzani? Akyanani hii sasa haivumiliki, ngoja mzee apachimbe
Ckweli ameingia tayari cdm imeshakuwa imara na tarifa tu wangepata wabunge wengi zaidi hata kuchukua dola.kitendo cha kubadili gia angani kilisononosha wengi nawengi walikata tamaa wakashndwa kuelewa tofouti kati ya ccm na cdm
 
Wakati akiwahutubia Madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha, Edward Lowassa alisema kile alichokiita CHADEMA KUHITIMU(TO GRADUATE) harakati na kukitaka chama hicho sasa kufanya siasa za kunuwia kushika dola na kuachana na Uanaharakati.
Naungana kabisa na kauli ya Lowassa kwani historia ya vyama vingi duniani kote inaonesha ni vyama vichache sana (ama hakuna kabisa) vilivyofanya siasa za aina ya CHADEMA vilivyofanikiwa kushika dola.

Inawezekana kabisa Lowassa anajua sababu za chama chake kufanya siasa za kiharakati lakini naye kwa makusudi kabisa akaamua kudhani ni sababu moja tu.

Moja ya sababu kubwa ambayo inaweza kusababisha aina hii ya siasa ni KUKOSA MAHALI pa kudumu pa kuweza kufanyia siasa na kuachana na harakati. Naongelea OFISI ZA CHAMA kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa. Hapana ubishi kwamba CHADEMA kinaelekea kuvuka ngazi ya SACCOS na kuwa taasisi kubwa. Kwa maana hiyo haitegemewi kabisa maamuzi ya Taasisi yakatoka kwa Lowassa, Mbowe, Lissu na Mashinji. Hata kuamua kufanya au kitofanya migomo na maandamano , lazima uamuzi utoke kwa wengi, siyo suala la ama Mbowe, ama Lowassa kuamua.Swali ni WAPI SASA WATU HAWA WATAKUTANA KUFANYA MAAMUZI YA WENGI? Ni kinondoni mtaa wa UFIPA?

Tayari Mbowe ameshatoa tamko la kuwataka vijana wa BAVICHA kusitisha azma yao ya kwenda Dodoma kufanya kile walichokiita kusaidia jeshi la polisi kuzuia MKUTANO WA NDANI wa CCM kwa madai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli alishaikataza kufanyika hadi 2020. Sababu alizozitoa Mbowe ni mufilisi kabisa eti wana taarifa watapigwa na polisi, mbona walisema hawaogopi Polisi? Eti wao hawana nia ya kupambana na polisi ila walitaka tu dunia ijue, kwa hiyo hawakuwa na hoja ila walikuwa wanajionesha tu kama bidhaa kwenye mabanda ya Sabasaba? Nimemdharau Mbowe.

Wajumbe wa CCM katika mkutano huo ni zaidi ya 500 lakini unafanyika ndani ya majengo yanayomilikiwa na CCM( Ni mali ya CCM). Leo Chadema wakifanya mkutano wao wa aina hiyo nao wauite MKUTANO WA NDANI? NDANI wapi wakati wanafanyia Mlimani City na Serena Hoteli huku kumbi hizo zikiwa zimezungukwa na wafuasi wakiwa na mabango na nyimbo za kukabiliana na vyombo vya dola.
Ndiyo maana wanalazimika kutumia viwanja vya Mashujaa, SOWETO, TANGANYIKA PAKERS n.k kufanya mambo yote kwa pamoja(mikutano ya ndani, harakati na chaguzi za chama chao).
Ni wakati Muafaka sasa Lowassa kujikuna zaidi ili kufanikisha Chama chake kuachana na siasa za Kiharakati kwa sababu ndogo tu ya kukosa ofisi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom