Bepari
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 904
- 329
Ni kweli si vizuri kufanya utani na maradhi ya mtu maana si ujinga wake kupata hayo maradhi na wala mtu si ujanja wake kuwa na afya. Lakini linapokuja suala kama hili la urais, lazima watu tulitizama suala la afya yake maana anataka kuwa kiongozi wetu hivyo lazima tuhoji je,ataweza kuongoza kwa hali aliyokuwa nayo? Laiti Lowasa asingejishughlisha na suala hili hakuna ambaye angekuwa anazungumzia afya yake leo,lakini kwa kuwa anataka awe kingozi mkuu wa nchi hivyo suala la afya yake si la kwake yeye na familia yake tu.
Hivyo si sahihi kutisha watu kuhoji afya yake maana anataka kuwa kiongozi mkuu.
Hata angegombe uenyekiti serikali ya mtaa, kura yangu asingeipata. Afya kigezo muhimu sana kwenye kazi, achilia mbali wizi na ufisadi.