Lowassa apaishwa BBC,atakiona cha mtema kuni

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mwanangu amekuja mbio kunikurupusha eti nije nione. Nione jinsi Idhaa ya Kiswahili ya BBC London inavyotangaza habari za Lowassa na UKAWA yake kwakuwa ni mtu maarufu! Amenítambia,kwakuwa yeye ni mpinzani wangu,kuwa Lowassa atatulaza macho wazi mwaka huu. Nipo hapa natazama,kwa kushurutishwa,BBC kupitia Star TV.

Nimemwambia kuwa Lowassa atakiona cha mtema kuni. Mwenyekiti wetu wa chama amesema. Mwenyekiti amesema tuna uzoefu,mbinu na sababu za kushinda. Mwanangu hapa ananimiminia maswali ili nimwambie mantiki ya kauli ya Mwenyekiti Kikwete. Nimemjibu kuwa asubiri Octoba 25.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Wizi mtupu na kupendelewa na maaskari ndio mbinu walizo nazo. Uzoefu ndio huo na sababu wanazo kuzuia maovu yao yasifichuliwe na watawala wapya. Nay, Kwishney ccm
 
Hakuna haja ya goli la mkono kwani watapigwa magoli kama wamesimama..Mwenyekiti kwa kujiamini.
 
Hii kauli inaweza kumpeleka the Hague huyu mkwere asipokuwa makini na kauli zake
 
CCM Fanyeni Campaign Hilo Gori La Mkono Msilitegemee na Mara Nyingi Linafanyiwa Team ambazo Hazikujipanga.
 
hahaha., we tupatupa umekula malimao Leo?
 
Mwanangu amekuja mbio kunikurupusha eti nije nione. Nione jinsi Idhaa ya Kiswahili ya BBC London inavyotangaza habari za Lowassa na UKAWA yake kwakuwa ni mtu maarufu! Amenítambia,kwakuwa yeye ni mpinzani wangu,kuwa Lowassa atatulaza macho wazi mwaka huu. Nipo hapa natazama,kwa kushurutishwa,BBC kupitia Star TV.

Nimemwambia kuwa Lowassa atakiona cha mtema kuni. Mwenyekiti wetu wa chama amesema. Mwenyekiti amesema tuna uzoefu,mbinu na sababu za kushinda. Mwanangu hapa ananimiminia maswali ili nimwambie mantiki ya kauli ya Mwenyekiti Kikwete. Nimemjibu kuwa asubiri Octoba 25.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

mwanao ana miaka mingapi mkuu?
 
Hakuna haja ya goli la mkono kwani watapigwa magoli kama wamesimama..Mwenyekiti kwa kujiamini.
Sekunde za mwanzo tu, beki tuliyedhani ndiye wa kutumainiwa dj kesha jifunga magoli mawili. Mwisho wa mechi itakuwa dazeni za magoli.
 
Kama anafkiria bao la mkono aangalie vizuri asijekuwa mgumba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom