Ni hivi mimi ni mshabiki wa upinzani na hasa cdm, sikuwahi kuumuunga mkono Lowassa na nililalamika kwamba lile ni kosa kubwa haswa baada ya ule upuuzi aliokuwa akiufanya Shibuda. Nilitarajia upinzani na hasa cdm watakuwa walijifunza kuhusu kupokea makapi toka ccm na kuyapa nafasi, cha kushangaza ndio wakafanya kosa kubwa kuliko yote ya kumpokea Lowassa na kumpa nafasi namba moja katika chama ya kugombea urais.
Matokeo yake baada ya Lowassa kuingia cdm, cdm kimegeuka kuwa chama cha kikondoo, hakuna lolote jipya aliloleta Lowassa ndani ya cdm zaidi ya kuwinda nafasi ya kugombea urais tena kwa faida ya CCM. Mambo yaliyoipa cdm nguvu huko nyuma yote yamemezwa na ujio wa Lowassa, kiasi kwamba wanaposema Mbowe na uongozi wa juu walihongwa kutoa nafasi ya kugombea urais kwa Lowassa inakuwa ni ukweli. Leo hii Magufuli na ubovu wake katika uongozi anaonekana ni bora kwani analinganishwa na Lowassa. Lowassa hajawahi kuwa mwanasiasa wa aina ya siasa za cdm, ubora wake wote huwa unaimbwa na wapambe lakini sio yeye.
Nashangaa wapenzi washabiki na wanachama wa cdm kuwa kimya wakati chama kimeendelea kufubaa kwa sababu ya uwepo wa Lowassa. Hili tukubali la kuendelea kuwa na Lowassa ndani y ya cdm ni kuimaliza cdm, ni wakati wa wote wanaoitakia mema cdm kupinga Lowassa kukaa nafasi za mbelembele kwenye mambo ya chama kwani hana mapenzi na chama zaidi ya kuhakikisha cdm inampa nafasi ya kufikia matakwa yake. Huyo Mbowe sio wa kumuacha tena aamue lolote kwani amekiharibu chama kwa faida yake ya muda mfupi.