Pole umepotea njia bila kujua mimi najua ukweli ulivyo kuliko wewe unayejua ukweli wa propaganda. Baadhi ya watu waliofanya mpango wa Lowassa kuja cdm, Slaa ndio alikuwa kinara. Ila hakutaka akija apewe nafasi ya kugombea urais kwani hiyo aliona ni haki yake na kweli alistahili. Tatizo lililojitokeza mpaka ikawa ilivyokuwa ni muungano wa Ukawa. Muungano huu ulitawaliwa na mitazamo ya nani haswa alipaswa kubeba jukumu la kugombea urais. Ushindani ukawa ni baina ya Lipumba na Slaa. Cuf waliona Lipumba anafaa na cdm waliona Slaa anafaa.
Kumbuka huu ulikuwa ni ushindani baina ya ccm dhaifu iliyokuwa inaogopa kupoteza dola lakini ikiwa na dola mkononi, na Ukawa yenye nguvu. Kwa mtazamo wao Cuf wakaona Slaa atapata shida kuungwa mkono na waisilamu kwani ilifahamika ccm wamejipanga kutumia siasa chafu kama kawaida yao ya kuongozwa na padri. Na cdm wakawa wanaona Lipumba hana ushawishi kama alivyokuwa huko nyuma. Hivyo bahati ikamuangukia Lowassa kwani naye alikuja na mzigo wake nyuma ya pazia, na pia kuuaminisha umoja huo kwamba yeye anaungwa mkono mpaka na wanaccm. Hivyo ili kuondoa mvutano wa Slaa na Lipumba, karata ikamuangukia Lowassa, huku Slaa na Lipumba wakiwa hawajaridhika na maamuzi hayo. CCM kwa kugundua tatizo hilo ndio wakawaribuni Slaa na Lipumba, na mengine kwa sasa ni historia. Kwa hiyo sio Slaa wala Lipumba waliondoka kwa ajili ya kuona eti Lowassa aliitwa fisadi, bali ushindani wao ndio uliosababisha Lowassa kuchukua nafasi waliyoitegemea wao. Na maadamu ccm hawakuwafuata mikono mitupu ulitegemea nini? Hivyo hilo la ufisadi ilikuwa ndio kete pekee ya kuaminisha watanzania. Matokea ya chochote kitu toka ccm ndio leo unamuona Lipumba anapata support ya wapi, na Slaa huko alipo hathubutu kuchangia dhidi ya ccm enzi zake.