Sipingi hoja zako moja kwa moja hasa msimamo wa Dr. Slaa linapokuja suala la misamamo yake toka kuacha upadre na hasa hasa huyo Lowassa. Kwa kiasi kikubwa sikuridhika na maamuzi ya Slaa kukiacha chama japo niliheshimu sana maamuzi yake. Ila nilichogundua Slaa ni mtu mwenye misimamo mikali ambayo wakati mwingine inaweza isimpate kila anachokitaka. Leo hii tunawaona wanaccm wakatuhumu na kukashifu wapinzani wanaposusia mijadala kwa kusema njia nzuri sio kukimbia bali kubaki na kujadili mpaka mwisho. Iweje leo wanaccm muonyeshe kuunga kitendo cha Slaa kukimbia chama chake badala ya kubaki na kupambana akiwa chamani mpaka kieleweke? Simply huu unaoleta ni unafiki wa kiccm.
Ni kweli kuwapokea wanachama wenye makando kando sio jambo zuri sana, lakini nikuulize, kama kweli ccm huwa inashinda kihalali kwanini hawa hawa wenye makando kando wanashinda wakiwa ccm? Huoni kwamba wapiga kura wanachagua bila kujali makando kando ya wagombea? Kama wapiga kura huwa wanachagua kihalali basi wakulaumiwa ni wao kwani wanaccm wengi wanasifa mbaya za wazi na za kificho lakini bado wanashinda uchaguzi. Kwa hiyo cdm wanaweza wasilaumiwe sana kwani wao huwa wanachagua bila kujali sifa za mgombea. Vinginevyo uniambie kwamba ushindi wa hao wagombea wenye sifa mbaya sio kikwazo cha wapiga kura. Mfano Lowassa alikuwa nia hiyo sifa mbaya kuliko Magufuli. lakini alipata kura milioni 6+ akawashinda akina Mama Mghirwa, Dovutwa, Hashimu Rungwe nk ambao hawakuwa na sifa mbaya za kifisadi.
Wangalau hili la kutowapa uongozi ninakuunga mkono. Hata mimi nimeshapendekeza sana humu jukwaani kwamba cdm iepuke sana kuwapa nafasi za kugombea wanachama toka vyama vingine haswa ccm tena wale wenye makando kando. Sikuishia hapo nikapendekeza pia mtu ili aweze kupata nafasi ya kugombea hasa aliyetoka chama kingine wangalau atumikie chama miaka sio chini ya miwili, kisha ndio apatiwe nafasi ya kugombea kama anataka. Sio lazima chama wafanyie kazi mapendekezo yangu ila wakifanyia kazi mapendekezo haya yanaweza kusadia baadhi ya mambo tofauti na ilivyo sasa.