Lowassa anaudhoofisha upinzani

Lowassa anaudhoofisha upinzani

Ili ufutiwe dhambi zako kwa mungu kiri lowassa ni fisadi!

Mkuu Lowassa na Magufuli hawachekani inapokuja suala la uadilifu. Labda tuongelee sifa nyingine zinazowatengenisha sasa lakini sio maadili. Hawa kwangu wote ni watu waliotumia madaraka yao kuwahujumu watanzania kila mmoja kwa nafasi yake. Ukipenda labda tuwaongelee kwa sasa lakini sio kabla ya uchaguzi wa 2015.
 
Slaa alisema nini? alichokifanya Slaa ni kuzira baada ya nafasi ya kugombea urais kupewa Lowassa. Hiyo tabia ya kuzira ya Slaa inaeleweka muda mrefu na hata wanaccm huwa mnamsifia kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani sasa hivi haikosoi serekali ya ccm. Sipingi mchango wa Slaa kwa cdm nauheshimu sana, lakini kilichomtoa cdm sio kufukuzwa bali ni nafasi ya urais kupewa Lowassa.
Hapo umepotoshwa, nawe kama wengine wengi, ukakubali kupotoka kirahisi. Lowasa aliteuliwa kugombea urais baada ya kuhamia chadema, na slaa alijiondoa chadema wakati wa mchakato wa lowasa kuhamia baada ya kushindwa kuafikiana katika mambo kadhaa ya msingi, hivyo slaa aliondoka kabla lowasa hajawa mwanachama wa chadema.

Hayo mengine in propaganda zilizoenezwa na mbowe na gwajima kumchafua slaa ikiwemo kutudanganya wanachama kwamba slaa alikuwa likizo wakati alikwisha kabidhi barua ya kujivua uongozi na uanachama.
 
Ujio wa Nyalandu kwangu sioni jipya kwani kwangu yeye ni mwanaccm kama walivyo wanaccm wengi. Sio Nyalandu tu, hata akija Nape huku cdm bado siwezi kushangilia kwani najua kabisa ataondoka ccm kuja cdm sio kwa kuipenda bali sehemu ya kupoozea machungu yake lakini sio kupenda sera zake. Wangalau Nyalandu, ukiacha sifa mbaya ya ufujaji wa mali ya umma aliyonayo mbele ya jamii kama alivyo Magu, yeye anamejitoa muhanga kwa kuhama ccm huku akiacha wadhifa wake bila kufukuzwa na kutokuogopa vitisho vya mwenyekiti asiyetaka kupingwa wala kukosolewa. Yeye namsifu kwa kuchukua maamuzi magumu kwa wakati huu na mazingira yalivyo, huu nauona ni ushujaa na si msifu kwa kutaka kujiunga cdm.
Mpendwa siyo kweli kwamba Dr slaa alizira eti kwa sababu alikosa nafasi ya kugombea uraisi, bali alikataa kula matapishi yake. Au kwa msemo wa Mwl Nyerere alikataa kugeuka nyuma kwani angekuwa jiwe.

Kumbuka kwa miaka miingi Dr Slaa amekuwa akimtaja Lowasa kuwa ni fisadi papa, je kwa mtu mwenye kusimamia msimamo wake, ingekuwa sahihi kubadili kauli hiyo na kumnadi Lowasa kama clean man!!!

Si hivyo tu bali pia Kumbuka umaarufu wa cdm umetokana na kuwashambulia mafisadi mojawapo akiwa ni Lowasa, je Dr Slaa angekuwa na kauli ipi kuhusu swala zima la ufisadi katika mikutano ya kumnadi Lowasa?

Kubali kataa cdm ingepata umaarufu sana na ingeendelea kupata umaarufu kama ingewakataa kuwapokea watu wowote wanye makandokando kama Liwasa na Nyalandu.

Kumbuka cdm walivyokuwa wakimsema Nyalandu kuhusiana na ubadhilifu wa mali za umma ikiwa ni pamoja na kusafirisha Twiga hai. Leo hii cdm wanadiliki kusema ya kuwa kumpata Nyalandu wamelamba dume!! Je kwa wenye akili waitafasili vipi kauli hiyo!!

Huoni kama kwa sasa cdm ni kama inaunda kundi maarumu la mafisadi? Kuna kila sababu kwa cdm kujitafakali upya kuhusu watu wanaowapokea. Si ajabu kesho tukasikia wakimpokea kwa shangwe pro Maghembe, nyoka wa makengeza, Zitto mliyemwita msaliti nk

Hata Sumayi hakuwa mtu sahihi kupokelewa cdm. Na kama mngempa uanachama basi mngeepuka kumpa uongozi. Kumbukeni huyu mlimwita mr zero je hiyo akili ameipata wapi baada ya kuja cdm?

Cdm mnaonyeshe wazi kuwa hamsimamii mnachokiamini kuwa si sahihi. Bali mko tayari kuchukua hata mizoga ili mradi tu mwingie ikilu. Kumbukeni kila binadamu ana ubongo hivyo kila binadamu ana kumbukumbu.
 
Labda hujui sifa ya cdm kwa kuwa uko hapa kutaka kuona wanacdm wanafarakana, tulio wengi tunajitambua na tunatumia haki yetu ya kusema ukweli bila kujali wanacdm wengine watajisikiaje kwani tunajua ukweli unaumiza kiasi gani. Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze cdm haijawahi kurudia mgombea uchaguzi wa urais. Mpaka sasa Dr. Slaa ndie alikuwa mgombea maarufu na aliyekubalika zaidi, lakini aliikosa nafasi hiyo aliyoitegemea itakuwa Lowassa? Lowassa yeye ni kama aliokota embe chini ya mnazi 2015. Hivyo usitarajie hiyo 2020 yeye kupata nafasi hiyo kwa namna yoyote.
Tuombe uzima.
 
Hapo umepotoshwa, nawe kama wengine wengi, ukakubali kupotoka kirahisi. Lowasa aliteuliwa kugombea urais baada ya kuhamia chadema, na slaa alijiondoa chadema wakati wa mchakato wa lowasa kuhamia baada ya kushindwa kuafikiana katika mambo kadhaa ya msingi, hivyo slaa aliondoka kabla lowasa hajawa mwanachama wa chadema.

Hayo mengine in propaganda zilizoenezwa na mbowe na gwajima kumchafua slaa ikiwemo kutudanganya wanachama kwamba slaa alikuwa likizo wakati alikwisha kabidhi barua ya kujivua uongozi na uanachama.

Kimsingi siko hapa kutafuta mshindi na huwa naamini hoja zangu bila kulazimisha yoyote kuzikubali, pia mimi hupima hoja za upande mwingine na kuzichambua kwa kadiri niwezavyo. Haya mambo hayakuwa wazi kwa asilimia mia moja. Hivyo ninamini nina ukweli kwa asilimia fulani na wewe pia una ukweli wa asilimia fulani. Nililifuatilia sana hili jambo la ujio wa Lowassa kuja cdm kwani lilinikwaza kutokana na madhara ya muda mrefu kwa chama iwapo kingeshika dola au mbaya zaidi kama kingekosa dola kama ilivyo sasa.

Nilijua ujio wake usingekuwa na afya kwa muda mrefu haswa iwapo asingeshinda urais. Nilimsikia Slaa kwa masikio yangu akikiri kukubali ujio wa Lowassa ila kwa masharti fulani. Moja wapo ilikuwa ni hilo la yeye kuusema ukweli wote kuhusu ushiriki wake kwenye kashfa ya richmond nk. Kwa sababu ya muda kuwa finyu zoezi hili halikwenda vizuri kwani viongozi wengi walikuwa pia kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu ikiwemo udiwani na ubunge. Hivyo pressure ya muda ilichangia jambo hili kutokuendeshwa kwa uwazi, na maridhiano yaliyo wazi moja kwa moja. Kwa ujumla ujio ule wa ghafla ulichangia zoezi lile kutokuratibiwa vizuri hasa ukizingatia kulikuwa na suala la Ukawa. Pupa ya jambo lile ndio iliyozua sijui niite changamoto au madhara ya kilichotokea. Itoshe kusema haya yote ni historia, ila kama tunajadili kwa sasa Lowassa hana faida ya wazi kwa chama kama ambavyo ingetarajiwa iwe. Labda kama viongozi walio karibu na yeye wanajua nini wanapata lakini sio mchango wa chama kitaifa.
 
...Cdm mnaonyeshe wazi kuwa hamsimamii mnachokiamini kuwa si sahihi. Bali mko tayari kuchukua hata mizoga ili mradi tu mwingie ikilu. Kumbukeni kila binadamu ana ubongo hivyo kila binadamu ana kumbukumbu.
Wenyewe wameshasema wapo tayari kuingia mkataba na shetani ili waingie ikulu. Ukishaingia mkataba na shetani nini kinafuata? Ushetani.
 
58.46% alizopata JPM 2015 zitashuka 2020 baada ya maboko anayopiga...wajiandae kuiba kisomi..wakikosea kama 2015 kitanuka
 
Mpendwa siyo kweli kwamba Dr slaa alizira eti kwa sababu alikosa nafasi ya kugombea uraisi, bali alikataa kula matapishi yake. Au kwa msemo wa Mwl Nyerere alikataa kugeuka nyuma kwani angekuwa jiwe.

Kumbuka kwa miaka miingi Dr Slaa amekuwa akimtaja Lowasa kuwa ni fisadi papa, je kwa mtu mwenye kusimamia msimamo wake, ingekuwa sahihi kubadili kauli hiyo na kumnadi Lowasa kama clean man!!!

Si hivyo tu bali pia Kumbuka umaarufu wa cdm umetokana na kuwashambulia mafisadi mojawapo akiwa ni Lowasa, je Dr Slaa angekuwa na kauli ipi kuhusu swala zima la ufisadi katika mikutano ya kumnadi Lowasa?

Kubali kataa cdm ingepata umaarufu sana na ingeendelea kupata umaarufu kama ingewakataa kuwapokea watu wowote wanye makandokando kama Liwasa na Nyalandu.

Kumbuka cdm walivyokuwa wakimsema Nyalandu kuhusiana na ubadhilifu wa mali za umma ikiwa ni pamoja na kusafirisha Twiga hai. Leo hii cdm wanadiliki kusema ya kuwa kumpata Nyalandu wamelamba dume!! Je kwa wenye akili waitafasili vipi kauli hiyo!!

Huoni kama kwa sasa cdm ni kama inaunda kundi maarumu la mafisadi? Kuna kila sababu kwa cdm kujitafakali upya kuhusu watu wanaowapokea. Si ajabu kesho tukasikia wakimpokea kwa shangwe pro Maghembe, nyoka wa makengeza, Zitto mliyemwita msaliti nk

Hata Sumayi hakuwa mtu sahihi kupokelewa cdm. Na kama mngempa uanachama basi mngeepuka kumpa uongozi. Kumbukeni huyu mlimwita mr zero je hiyo akili ameipata wapi baada ya kuja cdm?

Cdm mnaonyeshe wazi kuwa hamsimamii mnachokiamini kuwa si sahihi. Bali mko tayari kuchukua hata mizoga ili mradi tu mwingie ikilu. Kumbukeni kila binadamu ana ubongo hivyo kila binadamu ana kumbukumbu.

Sipingi hoja zako moja kwa moja hasa msimamo wa Dr. Slaa linapokuja suala la misamamo yake toka kuacha upadre na hasa hasa huyo Lowassa. Kwa kiasi kikubwa sikuridhika na maamuzi ya Slaa kukiacha chama japo niliheshimu sana maamuzi yake. Ila nilichogundua Slaa ni mtu mwenye misimamo mikali ambayo wakati mwingine inaweza isimpate kila anachokitaka. Leo hii tunawaona wanaccm wakatuhumu na kukashifu wapinzani wanaposusia mijadala kwa kusema njia nzuri sio kukimbia bali kubaki na kujadili mpaka mwisho. Iweje leo wanaccm muonyeshe kuunga kitendo cha Slaa kukimbia chama chake badala ya kubaki na kupambana akiwa chamani mpaka kieleweke? Simply huu unaoleta ni unafiki wa kiccm.

Ni kweli kuwapokea wanachama wenye makando kando sio jambo zuri sana, lakini nikuulize, kama kweli ccm huwa inashinda kihalali kwanini hawa hawa wenye makando kando wanashinda wakiwa ccm? Huoni kwamba wapiga kura wanachagua bila kujali makando kando ya wagombea? Kama wapiga kura huwa wanachagua kihalali basi wakulaumiwa ni wao kwani wanaccm wengi wanasifa mbaya za wazi na za kificho lakini bado wanashinda uchaguzi. Kwa hiyo cdm wanaweza wasilaumiwe sana kwani wao huwa wanachagua bila kujali sifa za mgombea. Vinginevyo uniambie kwamba ushindi wa hao wagombea wenye sifa mbaya sio kikwazo cha wapiga kura. Mfano Lowassa alikuwa nia hiyo sifa mbaya kuliko Magufuli. lakini alipata kura milioni 6+ akawashinda akina Mama Mghirwa, Dovutwa, Hashimu Rungwe nk ambao hawakuwa na sifa mbaya za kifisadi.

Wangalau hili la kutowapa uongozi ninakuunga mkono. Hata mimi nimeshapendekeza sana humu jukwaani kwamba cdm iepuke sana kuwapa nafasi za kugombea wanachama toka vyama vingine haswa ccm tena wale wenye makando kando. Sikuishia hapo nikapendekeza pia mtu ili aweze kupata nafasi ya kugombea hasa aliyetoka chama kingine wangalau atumikie chama miaka sio chini ya miwili, kisha ndio apatiwe nafasi ya kugombea kama anataka. Sio lazima chama wafanyie kazi mapendekezo yangu ila wakifanyia kazi mapendekezo haya yanaweza kusadia baadhi ya mambo tofauti na ilivyo sasa.
 
Tambua kuwa ufisadi ni nguzo pekee inayoifanya hadi leo CCM inapumua na unapomtuhumu kuwa mchafu yakupasa utambue kuwa ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja ...
sasa hivi hakuna msafi na mchafu kuna Ilimradi na Afadhali..
 
Ila Magufuli kwa kukamata kamata na kunyima uhuru ndio anastawisha upinzani huku akitoa maagizo kuwa spika awashungulikie bungeni nae wakitoka huku nje atawashughulikia!!!

Hivi yule aliyekuwa akiripoti Central kila week kwa kosa la uchunguzi wa uchochezi baada ya kusema masheikh wa UAMSHO toka zanzibar walioshikiliwa Ukonga kwa miaka minne sasa huku kesi tunambiwa uchunguzi bado ni Baba yako ama baba watoto?!!!
Gheresha hizo angekuwa mwingine angelikuwa Nairobi....
 
Hahahaha ameamua awaache tu mkiwa na amani maana angeanza kudai haki kama alivyodai cjui Tanzania tungekuwa wap sasa so pengine kuna kitu amekiona mbele akaamua kutupilia mbali na kutulia
Kwa hiyo, ni zigo
 
3) Mbona hajawahi kuomba msamaha kwa kuwapotosha wapigakura alipowaahidi suala la kulinda kura ni lake aachiwe na baada ya kushindwa akadai aliibiwa?

Lowassa ni msanii na alikiingiza chama na upinzani chaka kwa kuwalaghai wananchi waondoke vituoni baada ya kupiga kura, huku akijua fika njia pekee ya kuindoa CCM madarakani ilikuwa ni kupiga kura na kuzilinda..

Lowassa & Katibu mkuu Mashinji hawana jipya la kuweza kuusaidia upinzani na chama kwa ujumla..
Ni kwa maombi tu tutoke hapa tulipo
 
Ni hivi mimi ni mshabiki wa upinzani na hasa cdm, sikuwahi kuumuunga mkono Lowassa na nililalamika kwamba lile ni kosa kubwa haswa baada ya ule upuuzi aliokuwa akiufanya Shibuda. Nilitarajia upinzani na hasa cdm watakuwa walijifunza kuhusu kupokea makapi toka ccm na kuyapa nafasi, cha kushangaza ndio wakafanya kosa kubwa kuliko yote ya kumpokea Lowassa na kumpa nafasi namba moja katika chama ya kugombea urais.

Matokeo yake baada ya Lowassa kuingia cdm, cdm kimegeuka kuwa chama cha kikondoo, hakuna lolote jipya aliloleta Lowassa ndani ya cdm zaidi ya kuwinda nafasi ya kugombea urais tena kwa faida ya CCM. Mambo yaliyoipa cdm nguvu huko nyuma yote yamemezwa na ujio wa Lowassa, kiasi kwamba wanaposema Mbowe na uongozi wa juu walihongwa kutoa nafasi ya kugombea urais kwa Lowassa inakuwa ni ukweli. Leo hii Magufuli na ubovu wake katika uongozi anaonekana ni bora kwani analinganishwa na Lowassa. Lowassa hajawahi kuwa mwanasiasa wa aina ya siasa za cdm, ubora wake wote huwa unaimbwa na wapambe lakini sio yeye.

Nashangaa wapenzi washabiki na wanachama wa cdm kuwa kimya wakati chama kimeendelea kufubaa kwa sababu ya uwepo wa Lowassa. Hili tukubali la kuendelea kuwa na Lowassa ndani y ya cdm ni kuimaliza cdm, ni wakati wa wote wanaoitakia mema cdm kupinga Lowassa kukaa nafasi za mbelembele kwenye mambo ya chama kwani hana mapenzi na chama zaidi ya kuhakikisha cdm inampa nafasi ya kufikia matakwa yake. Huyo Mbowe sio wa kumuacha tena aamue lolote kwani amekiharibu chama kwa faida yake ya muda mfupi.
Upinzani wetu wengi wao ni mkono uko mdomoni...tumbo street
 
Back
Top Bottom