Lowassa anaudhoofisha upinzani

Lowassa anaudhoofisha upinzani

Jibu swali kama jinalake halitapitishwa ataendelea kusalia hapo?
Sioni kama kuna mtu wa kuzuia jina la lowasa ndani ya chadema, labda mwenyewe aamue kutogombea. 2020 mtajuta kwanini mlimpokea.
 
Slaa alishasema lakini mkampuuza,vp kuhusu ujio wa nyalandu mnadhani nae ni kama lowassa!

Slaa alisema nini? alichokifanya Slaa ni kuzira baada ya nafasi ya kugombea urais kupewa Lowassa. Hiyo tabia ya kuzira ya Slaa inaeleweka muda mrefu na hata wanaccm huwa mnamsifia kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani sasa hivi haikosoi serekali ya ccm. Sipingi mchango wa Slaa kwa cdm nauheshimu sana, lakini kilichomtoa cdm sio kufukuzwa bali ni nafasi ya urais kupewa Lowassa.

Ujio wa Nyalandu kwangu sioni jipya kwani kwangu yeye ni mwanaccm kama walivyo wanaccm wengi. Sio Nyalandu tu, hata akija Nape huku cdm bado siwezi kushangilia kwani najua kabisa ataondoka ccm kuja cdm sio kwa kuipenda bali sehemu ya kupoozea machungu yake lakini sio kupenda sera zake. Wangalau Nyalandu, ukiacha sifa mbaya ya ufujaji wa mali ya umma aliyonayo mbele ya jamii kama alivyo Magu, yeye anamejitoa muhanga kwa kuhama ccm huku akiacha wadhifa wake bila kufukuzwa na kutokuogopa vitisho vya mwenyekiti asiyetaka kupingwa wala kukosolewa. Yeye namsifu kwa kuchukua maamuzi magumu kwa wakati huu na mazingira yalivyo, huu nauona ni ushujaa na si msifu kwa kutaka kujiunga cdm.
 
Umesema kweli kama kweli Lowassa angekuwa ni mwanasiasa mwenye intergrity angejiuzulu baada ya kushindwa uraisi.Kilichompeleka ukawa ni uraisi.
 
...Hakuna chochote alicholeta kipya hata asingekuja bado cdm ingepata ushindi mkubwa kuliko yeye alivyokuja, huo ni ukweli uliodhahiri. Lowassa angeenda UDP au TLP apate kura zile ningeamini na sio kupitia cdm.
Kwa lugha nyepesi, ujio wake ilikuwa loss kwa chama.
 
Kwani nani amewahi kukuhesabu among the human beings ?

Kwa bahati mbaya nafanya siasa kwa kujitambua bila kumuiga yoyote, msimamo wangu sio lazima ukufurahishe ndio maana sikushawishi kunikubali wala kushawishi wengine mnaomuona Lowassa anafaa awe hafai. Niko cdm muda mrefu na sijawahi kuvutiwa na cdm kwa ajili ya kusubiri ujio wa Lowassa. Nitaendelea kuipenda cdm bila Lowassa kuwa ndani ya hayo mapenzi yangu. Cdm imepata nguvu na kukubalika na wengi bila mchango wa Lowassa, hivyo kwangu cdm bila Lowassa ndio cdm original.
 
Lumumba mbona mna muogopa sana EL ? Au bado mna weweseka na kichapo cha uchaguzi wa 2015, kile kulikuwa cha mtoto subirini sasa 2020.
 
Kwa lugha nyepesi, ujio wake ilikuwa loss kwa chama.

Kwa mtazamo wangu ujio wake ni loss kwa chama na itaendelea kuwa hivyo. Simsemei mwanachama yoyote kwani kila mtu ana mtazamo wake kwenye hili. Ila mimi kama mimi sioni faida wala jambo jipya lenye kukuza chama zaidi ya aliyovyokikuta chama.
 
Slaa alisema nini? alichokifanya Slaa ni kuzira baada ya nafasi ya kugombea urais kupewa Lowassa. Hiyo tabia ya kuzira ya Slaa inaeleweka muda mrefu na hata wanaccm huwa mnamsifia kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani sasa hivi haikosoi serekali ya ccm. Sipingi mchango wa Slaa kwa cdm nauheshimu sana, lakini kilichomtoa cdm sio kufukuzwa bali ni nafasi ya urais kupewa Lowassa.

Ujio wa Nyalandu kwangu sioni jipya kwani kwangu yeye ni mwanaccm kama walivyo wanaccm wengi. Sio Nyalandu tu, hata akija Nape huku cdm bado siwezi kushangilia kwani najua kabisa ataondoka ccm kuja cdm sio kwa kuipenda bali sehemu ya kupoozea machungu yake lakini sio kupenda sera zake. Wangalau Nyalandu, ukiacha sifa mbaya ya ufujaji wa mali ya umma aliyonayo mbele ya jamii kama alivyo Magu, yeye anamejitoa muhanga kwa kuhama ccm huku akiacha wadhifa wake bila kufukuzwa na kutokuogopa vitisho vya mwenyekiti asiyetaka kupingwa wala kukosolewa. Yeye namsifu kwa kuchukua maamuzi magumu kwa wakati huu na mazingira yalivyo, huu nauona ni ushujaa na si msifu kwa kutaka kujiunga cdm.
Ok pole dogo naona unaandika kwa uchungu na ghazabu nyingi ila slaa aliondoka baada ya kuona mtu waliemuimba fisadi amepokelewa na ameambiwa aikane ccm ameshindwa kuikana,mmechelewa kansa imeshamtafuna mgonjwa haiwezekani kuchomwa kwa mionzj wala kukatwa viungo!
 
7b3c3bba6d9c0891d8841f53a3d6814f.jpg
Raisi amepiga marufuku kufukua makaburi mkuu
 
Kwa mtazamo wangu ujio wake ni loss kwa chama na itaendelea kuwa hivyo. Simsemei mwanachama yoyote kwani kila mtu ana mtazamo wake kwenye hili. Ila mimi kama mimi sioni faida wala jambo jipya lenye kukuza chama zaidi ya aliyovyokikuta chama.
Mkuu, huo ndio ukweli wenyewe japo kuusema hadharani inakuwa ngumu kwa wengi. Najiuliza watu kama mnyika wamekutwa na nini kiasi cha kuwa kimya hivi, sipati jibu.
 
Sioni kama kuna mtu wa kuzuia jina la lowasa ndani ya chadema, labda mwenyewe aamue kutogombea. 2020 mtajuta kwanini mlimpokea.

Labda hujui sifa ya cdm kwa kuwa uko hapa kutaka kuona wanacdm wanafarakana, tulio wengi tunajitambua na tunatumia haki yetu ya kusema ukweli bila kujali wanacdm wengine watajisikiaje kwani tunajua ukweli unaumiza kiasi gani. Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze cdm haijawahi kurudia mgombea uchaguzi wa urais. Mpaka sasa Dr. Slaa ndie alikuwa mgombea maarufu na aliyekubalika zaidi, lakini aliikosa nafasi hiyo aliyoitegemea itakuwa Lowassa? Lowassa yeye ni kama aliokota embe chini ya mnazi 2015. Hivyo usitarajie hiyo 2020 yeye kupata nafasi hiyo kwa namna yoyote.
 
Kwa bahati mbaya nafanya siasa kwa kujitambua bila kumuiga yoyote, msimamo wangu sio lazima ukufurahishe ndio maana sikushawishi kunikubali wala kushawishi wengine mnaomuona Lowassa anafaa awe hafai. Niko cdm muda mrefu na sijawahi kuvutiwa na cdm kwa ajili ya kusubiri ujio wa Lowassa. Nitaendelea kuipenda cdm bila Lowassa kuwa ndani ya hayo mapenzi yangu. Cdm imepata nguvu na kukubalika na wengi bila mchango wa Lowassa, hivyo kwangu cdm bila Lowassa ndio cdm original.
Ili ufutiwe dhambi zako kwa mungu kiri lowassa ni fisadi!
 
Makamanda akili zimeanza kurudi ....tunaitaka CDM ile .....ile isiyoogopa chochote ....ile iliyokesha viwanja vya NMC ....ile iliyopigwa bomu .....ile iliyofanya Mwangosi akauawa ...ile si hii ....
Watu tulinyeshewa na mvua pale, watu tulikuwa tupo tayari kukesha mkesha wa amani kwa ajili ya Lema aliyekuwa amesekwa ndani kwa hila za CCM ..
Nakumbuka baada ya mvua kuanza watu walianza kuondoka ndipo Lissu akapanda jukwani na kutamka "Wana-Arusha mnaogopa mvua badala ya kuuogopa umaskini"?

Kiukweli Chadema ya kipindi kile ilikuwa na nguvu na hatari kwa maslahi ya CCM, kinyume chake kwa sasa ni Lowassa amekuwa hatari kwa maslahi ya Chadema..
 
Ok pole dogo naona unaandika kwa uchungu na ghazabu nyingi ila slaa aliondoka baada ya kuona mtu waliemuimba fisadi amepokelewa na ameambiwa aikane ccm ameshindwa kuikana,mmechelewa kansa imeshamtafuna mgonjwa haiwezekani kuchomwa kwa mionzj wala kukatwa viungo!

Pole umepotea njia bila kujua mimi najua ukweli ulivyo kuliko wewe unayejua ukweli wa propaganda. Baadhi ya watu waliofanya mpango wa Lowassa kuja cdm, Slaa ndio alikuwa kinara. Ila hakutaka akija apewe nafasi ya kugombea urais kwani hiyo aliona ni haki yake na kweli alistahili. Tatizo lililojitokeza mpaka ikawa ilivyokuwa ni muungano wa Ukawa. Muungano huu ulitawaliwa na mitazamo ya nani haswa alipaswa kubeba jukumu la kugombea urais. Ushindani ukawa ni baina ya Lipumba na Slaa. Cuf waliona Lipumba anafaa na cdm waliona Slaa anafaa.

Kumbuka huu ulikuwa ni ushindani baina ya ccm dhaifu iliyokuwa inaogopa kupoteza dola lakini ikiwa na dola mkononi, na Ukawa yenye nguvu. Kwa mtazamo wao Cuf wakaona Slaa atapata shida kuungwa mkono na waisilamu kwani ilifahamika ccm wamejipanga kutumia siasa chafu kama kawaida yao ya kuongozwa na padri. Na cdm wakawa wanaona Lipumba hana ushawishi kama alivyokuwa huko nyuma. Hivyo bahati ikamuangukia Lowassa kwani naye alikuja na mzigo wake nyuma ya pazia, na pia kuuaminisha umoja huo kwamba yeye anaungwa mkono mpaka na wanaccm. Hivyo ili kuondoa mvutano wa Slaa na Lipumba, karata ikamuangukia Lowassa, huku Slaa na Lipumba wakiwa hawajaridhika na maamuzi hayo. CCM kwa kugundua tatizo hilo ndio wakawaribuni Slaa na Lipumba, na mengine kwa sasa ni historia. Kwa hiyo sio Slaa wala Lipumba waliondoka kwa ajili ya kuona eti Lowassa aliitwa fisadi, bali ushindani wao ndio uliosababisha Lowassa kuchukua nafasi waliyoitegemea wao. Na maadamu ccm hawakuwafuata mikono mitupu ulitegemea nini? Hivyo hilo la ufisadi ilikuwa ndio kete pekee ya kuaminisha watanzania. Matokea ya chochote kitu toka ccm ndio leo unamuona Lipumba anapata support ya wapi, na Slaa huko alipo hathubutu kuchangia dhidi ya ccm enzi zake.
 
Back
Top Bottom