Njaa zao zitatufikisha mahari pabaya...ebu wahandishi wa habari mlio safi na kama mnawajuwa wenzenu wanaofanya vitendo hivyo wakemee kwa nguvu zote waache kabisa hizo tabia.
Wakumbuke wanayoyafanya leo ni wajukuu wao na wa kwetu watakaopata shida sana...si muda si mrefu sana wote tutakuwa mavumbini na kuacha vyote tulivyopanda hapa hapa duniani...iwe tulivipata kwa jasho letu au kwa ufisadi...
Tujiulize wote nani atakuwepo miaka 30 ijayo....kama si watoto na wajukuu zetu. Sasa waheshimiwa mafisadi tafadhalini sana badili hizo tabia zenu...na nyinyi baadhi ya wahandishi msiokuwa na maadili msikubali njaa zenu ziwafanye kuwa watumwa...
Mungu tuapushe na haya mafisadi yasiyo na aibu....
Lowassa alichafuka zamani kabla ya Richmond
Waandishi Wetu Februari 20, 2008
HATA kama tuhuma za kampuni hewa ya Richmond zingemnusuru, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, asingefika mbali, kwa vile alikwisha kujitengenezea maadui wengi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), bungeni na serikalini, Raia Mwema imefahamishwa.
- Kikwete alijulishwa, akapuuza
Hatua ya Lowassa ya kujiuzulu kiasi cha wiki mbili zilizopita, ilikuwa inahitimisha tu mlolongo wa matukio ndani ya CCM, bungeni na serikalini na hata katika nyanja za kibiashara na kijamii, yanayokwenda nyuma katika wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais ndani ya chama hicho, na baadaye katika utendaji wa kila siku akiwa Waziri Mkuu.
Endelea na story hapa RAIAMWEMA
Nimeisoma Riport Ile...
Ninachosema Kama Hakuewa Fursa Ile Anahaki Ya Kujitetea Kwani Hakuwa Na Pakuongelea Jamani!!
Nimeisoma Riport Ile...
Ninachosema Kama Hakuewa Fursa Ile Anahaki Ya Kujitetea Kwani Hakuwa Na Pakuongelea Jamani!!
[/QUOTE]2. Edo alifanya jambo la ajabu sana kutumia nafasi aliyopewa bungeni achangie mjadala unaomhusu, nafasi ambayo angeweza kujitetea, kuwa alisingiziwa kwa sababu hii na ile, badala yake yeye akatangaza kwa jazba kuwa ana resign. Amefika wapi?
3. Amegundua sasa kuwa uamuzi wake utagharimu maisha yake yote yaliyobaki kisiasa, na ameanza kukuru kakara kuanza kujitetea, tena kwa kuwasingizia wenzake.
5. Edo ameshindwa hata kujitetea jana kwenye TvT. Alichoongea kwa kweli hakina mantiki kwa ku settle dust la Richmond. Huwezi kusema sasa umegundua Edo alionewa na kamati, na ukatupa sababu za maana.
Tu convince kwa hoja tukuelewe, si kwa blah blah tu, Mkuu. Karibu sana.
Tumwamini nani? Tume , Lowasa au watetezi wake? Tafuta riport ya Mwakyembe.
...na ujue kuwa we are watching guys like you who comes up with attractive threads to cleanse the Richmond scandal guys. Tumejadili kwa mapana sana juu ya mambo ya Lowasa et al, kabla hujajiunga hapa...
Ndugu Kishaju,
Karibu sana JF. Una maana gani hapo juu? Kuna kitu kinaitwa plagiarism, unakifahamu?
Ndugu yangu samahani yaani nilikuwa najaribu ku-quote kumbe pale juu nikafuta ndo maana ikaonekana kama vile imetoka kwangu...sikuwa na nia ya kuifanya kama "my original idea" Nilikuwa nataka nichambue baadhi ya vipengele ambavyo nimeviona vinanifurahisha.
Kwa hiyo ndugu yangu usinielewa vibaya...nina masaa chini ya 24 tangu nimeingia hapa...bado niko kwenye kujifunza...
Bila shaka umenielewa...hivyo sikuwa na nia ya kuiweka kama "original idea" yangu...nilikuwa nataka kuonyesha msisitizo...hivyo ni tatizo la kiteknologia si nia yangu kufanya hivyo...
Ndugu Idimi, nashukuru sana kwa maelekezo yako...yatanisaidia sana...bila shaka na Mbalamwezi atakuwa ameelewa kwamba sikuwa na nia mbaya ni katika kujifunza...
Bila shaka ndugu yangu Kishaju!
Hakuna aliyeingia hapa JF na kujua kila kitu kwa siku moja, utagundua kwamba kadri unavyizidi kuwa hapa ndio unajifunza jambo jipya kila siku. Hii ni kawaida kabisa.
Sasa basi ili kuthibitisha kama umenielewa, hebu ninukuu mimi kwa kufuata maelekezo hayo hapo juu
Good luck!.
Pope,
Hata kichaa anaweza kuona kuwa kujitetea kwa Lowassa sio majibu yanayotakiwa na wananchi hata kidogo...
1. Anapodai kusikia minong'ono mitaani kwani hakujua kulikuwa na nyaraka zinazojieleza wazi zaidi ya minong'ono?...soma report ya Mwakyembe.
2. Alipowaita wakuu wa Idara ni maelezo baada ya mkataba kuwa signed, sisi tunachouliza na hata hiyo report inachokizungumzia ni nani walioshinikiza Richmond kupewa Mkataba.
3. Huo mwezi September na October anaodai ktk maelezo yake tayari, Richmond walishakubaliwa kuingiza generators nchini..Nini mchango wake kabla ya hapo?
4. Alipoulizwa bungeni kuhusiana na Mkataba wa Richmond, kwa mdomo wake aliliambia bunge hakuna matatizo yoyote ktk mkataba wa Richmond hata baada ya vyombo vya habari kufichua ukweli kuhusu Richmond...Hivyo basi ni wakati gani alitumia nafasi yake kama Waziri mkuu kupata uhakika wa mkataba ule badala ya minong'ono...
5. Je, siii yeye aliyesema kwamba Kamati imetumia minong'ono kumsulubu walitakiwa kumwita yeye?.. mbona yeye pia ktk utekelezaji wa kazi yake alitumia Minong'ono kutengua Utafiti wa Wataalam kuhusiana na uwezo wa Richmond. Je, aliwaita wataalam hao kupata uhakika kimaandishi?... NO! mbali na Taarifa ya Mwakyembe kudai kuwa barua zaidi ya mara mbili ofisi yake iliandikiwa barua.
He is gualty as hell!.. tena kama PrimeMinister ndio asiseme kabisa maanake anazidi kujichimbia kaburi...