Lowassa anasafishwa!

Sweet dreams.I was very disappointed with the interruption of his TVT interview. It looks like EL hasn't got good advisors now and before. His interview gives more questions than answers. If he really did not know who or what is RDC why form the GNT. Yes he was involved in termination of City water contract, surely he would have then made sure that such provisions were included in the contract. Advisors only advice you decide to agree or not.
 
Nahisi kucheka, Maaana hata kama ni ndumba basi jamaa ni mwisho, Asijilinganishe na Mwinyi, wakati ule watu hatukuwa na huduma kama JF wengi hawakujua Who is Mwinyi. Sasa huyu jamaa We know him. Na anapata huo ubabe kwa vile anadhania bado ushoga upo kati yake na Muungwana. Bwana wee wacha hadithi mbele ya Mayai ya Ikulu urafiki na ufe!! I mean not easy. Kikwete kosa analofanya ni kuendelea kumuenzi, Hayo mapesa atakayolipwa kama X PM hastahili, mwizi. This time Badala ya kurukia JF wangekuwa wamemrikia Lowasa na kumweka ndani na kundi lake lote. Inabidi jakaya acheze karata vema, akiona aibu maji yatamzoa maana sumaye yuko Havard! na sasa EL na wengine wengi ndani ya THITHEM. Hiyo mianya itawabomoa wote, sasa hapo ndiyo tutapata serious leaders.
 
Huyu mwache athubutu kurudi kwenye siasa.
Hizo data watu wa jamboforum watakazozitoa kuhusu huyu, bora abaki tu ajenge hoteli na hela za wizi hizo, achunge ng'ombe
maana akileta ubabe, embu cheki clip hii ya Jamboforum vs Lowassa PT1 (Richmond report ilivyotoka)...Lowassa is on the right
 
Huyu mwache athubutu kurudi .... Jamboforum vs Lowassa PT1 (Richmond report ilivyotoka)...Lowassa is on the right

Ehh!,Mkuu hii ni'Kick-Boxing',au 'Wrestling??'maana naona Rafu zote kama zinaruhusiwa humo!!
Kama sikosei Wana-JF tuna Sheria zetu 11 za kuzingatia ktk mapambano...Teh teh..
 

We entirelly know that the "system" wants to clean Mr. Lowassa..that's why the program was cut off-air. It seems the following interview did touch some other people who are "there" sitting on the high table, so the trick had to be applied to defend them. Let him be innocent to the people of his constituency. We can't dare to listen to him. We have been listening to him for about a decade now..It's over now..Let him go
 
watu waliofikiria kuwa Lowasa atajiuzulu kisha atakaa kimya were very wrong!!
get ready to watch an overwhelming power fight! kikwete needs to kill or wait to be killed (politically)
 
watu waliofikiria kuwa Lowasa atajiuzulu kisha atakaa kimya were very wrong!!
get ready to watch an overwhelming power fight! kikwete needs to kill or wait to be killed (politically)
I think he's just trying to play smart with Tanzanians.... he has made a wrong move now. He can only be trusted by his Monduli residents who seems to have put much trust in him or have been misinformed and now believe that this man is their HERO!?
With time all his hopes will vanish and he'll soon be a nobody in this country...
 


I am not sure if Monduli's people still believe on him, but they have to give him support assuming that he will bring some leftover to the area...kama ni kuanguka basi amengukia pua mwache atumie pesa zake alizonazo kujinyanyua, coz "mfa maji haishi kutapatapa"
 
Kasi ya kumsafisha Edward Lowassa ni kubwa kwa sasa na kuna mipesa kibao imemwagwa na yeye mwenyewe na wapambe wake kuwa lazima asafishwe ili awe presida baadaye au mpambe wake wa karibu.

Hivi sasa baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wa habari tena wengine wakijidai kuwa mahiri kabisa na wakongwe, wameibuka kumtetea Lowassa huku vyombo vyao vya habari vikiimba sifa zake za ujasiri, uchapa kazi na kwamba eti hakuhusika ila "anawajibika tu na atarudi madarakani baadaye."

Idadi kubwa ya watu tunakerwa hasa na namna waandishi mahiri kabisa tena wengine tunaambiwa wana ‘madigrii na mastashahada' ya ng'ambo wanavyotumika kucheza ngoma inayowadhalilisha wao, taaluma ya uandishi, vyombo wanavyoviandikia na hata Lowassa wanayempamba.

Mtu ‘graduate' anapoandika habari ndefu ya aya zaidi ya 20 akitumia maneno ya kusifia tu, lazima tutilie shaka habari yenyewe, mwandishi aliyeiandika na chombo anachokiandikia. Msomi anapoandika habari ya ukurasa mmoja akielezea kiatu cha mtuhumiwa na gauni la mkewe, lipustiki na wanja, tunapata shaka kubwa ya lengo hasa la habari yenyewe. Tena habari lidistori- kwamba iko ukurasa wa mbele ikiongoza habari zingine.

Maneno ya kusifia tu kama vile: bashasha ya hali ya juu, furaha ya dhati, mabango yenye ujumbe mzito kwa serikali, kama muujiza vile, kwa mshangao wa wengi na kadhalika na kadhalika, sio maneno ya kiuandishi.

Tunadhani mwandishi huyo kahongwa au kanunuliwa aandike hivyo alivyoandika, anatumiwa na mtu au kundi la watu wenye malengo fulani – angalia kauli kama "amewajibika kama Rais Mstaafu Mwinyi na baadaye atarejea! swali ni je, atarejea lini? Atarejea kuwa nani? Rais wa Jamhuri?

Sisi tulitarajia waandishi hao waliokwenda Arusha ama kwa kujigharimia wenyewe, kwa kugharimiwa na vyombo wanavyoviandikia ama kwa kugharimiwa na wapenzi wa Lowassa, watueleze hao watu 10,000 waliompokea Lowassa na magari 400 waliyokuwa nayo waliandaliwa na nani na lini?

Elfu kumi hao, na wenye magari hao, ni akina nani? Je ni wafanyabiashara ya ng'ombe? Ni wanunuzi wa mawe (madini) au ni wachimbaji wadogo wadogo wa Mirerani? Je, ni wauzaji na wakulima wa maua au ni wamiliki wa magari na kampuni za utalii?

Tungefurahi sana kama wangetuambia kama wapokeaji hao na waandamanaji miongoni mwao ni wahalifu na kama ni wahalifu wametoka jela lini? Au je, ni wana-CCM wenye vyeo fulani. Bila kutufahamisha vyeo, kazi na fani za wapokeaji wa Arusha tunapata kigugumizi cha kuikubali habari hii. Tunaona sio bure, ipo namna. Watu hawamshangilii hivi hivi tu mtuhumiwa!

Swali ambalo tunajiuliza sana ni kwamba ni kwa nini kumekuwa na kampeni kubwa sana ya kumwandika vizuri Lowassa peke yake wakati waliojiuzulu au kupendekezwa wawajibishwe ni wengi. Au wengine kama Karamagi na Msabaha hawahitaji kusafishwa?
 
Ukweli ni kwamba watanzania tumewekwa kama hadhira mfu kwenye mchezo wa kuigiza. Kwa hatua ambayo imefikia kila mtu analake la kuongea bila ya kujihoji mwenyewe kwanza anaongea nini na kwa kwa nini anaongea yale anayoyaongea . Sasa ili tuonekane kwamba tumedhamilia kuwaadibisha tuwapeleke mahakamani ambapo wataongea yote na kukithibitishia chombo hiki cha haki kuwa wao sio wahusika na uma wa watanzania utaelewa. Tuwapelekeni mahakamani wathibitishe wanayopwayuka kila kukicha.
 
subirini siku ya j'tano, kwenye Raia Mwema Bw. mdogo ana ujumbe mzito kuhusu hili...
 
Hili linaweza kuwa jambo la maana, watu wajitokeze kufile kesi. Mtikila yuko wapi, mbona kapotea sana huyu mtaalamu wa kesi za kudandia. Maana hapa ndo palikuwa mahala pake kama kweli anajali maslahi ya nchi na walala hoi dhidi ya walalahai
 
Hili linaweza kuwa jambo la maana, watu wajitokeze kufile kesi. Mtikila yuko wapi, mbona kapotea sana huyu mtaalamu wa kesi za kudandia. Maana hapa ndo palikuwa mahala pake kama kweli anajali maslahi ya nchi na walala hoi dhidi ya walalahai

HahaaHaaa, Mtikila mnamkatisha tamaa waTZ. Akienda mahakamani akishinda mnamsifu akiitisha mkutano wa kampeni kwa ajili ya chama chake hamhudhurii. Akisema saa ya Ukombozi ni sasa hamuitikii.

Nafikiri yuko busy kuangalia vifungu vya sheria na soon ataipeleka kesi hiyo mahakamani. So far anakesi zisizopungua 3 mahakama kuu mapaka sasa hivi

Mahakama ya kadhi,
Kumkashifu Rais Mkapa
Kesi ya uchochezi
n.k
 
Maneno haya ni mazito nami yameniingia .Wakati wewe unangoja kuweka jina mimi naweka kabisa kwamba mwanasheria akianza basi ani andike niwe wa kwanza wewe uwe wa pili kwa kuwa majina yako hayako tayari bado .Mimi ni Joseph Lunyungu Matandula wa Mademla .Niko Mtoni Kijichi na namba zangu za simu ukizitaka sema tafadhali .
 

Lunyungu umenifurahisha, haya huo ndiyo ujasiri wenyewe. hili jambo la kufaili kesi ni jambo la maana sana. lakini tunahitaji wajuvi wa sheria watueleze iwapo inawezekana and me too am ready for that.
 

Mtalaam Lunyungu, naona uzalendo umekukaa sana!! Hongera sana.

Naungana na Advisor na wewe katika hili, nacho omba tulijadili suala hili kisheria, wanasheria wetu watusadie tafadhari ili tupate a good Plan of action!
 
Wazo nzuri,tunalihafiki. Ni kweli kwamba tukitumia muda mwingi kuongelea haya ya kambi ya Lowassa tutapunguza nguvu za kukemea ufisadi na hili sakata litatoweka masikioni mwetu na ndiyo jamaa atarudi tena kwa nguvu za pesa zetu zilezile za richmond na falsafa mpya. Huko mahakamani tutakuwa na kesi gani na vielelezo vipi? maana tutadaiwa ushahidi hatuna,au tumuombe mwakyembe atupe lile file lake ndiyo liwe ushahidi. Vijana wa mwakyembe aka wanasheria tupeni mawazo. Niko tayari kuchangia malipo ya wakili
 

Naunga mkono jina langu ni Neema Solomoni nakaa chang'ombe
 
Mie nikitaja jina langu mioyo ya watu itapasuka!nitaendelea kuwa invisible mpaka pale Mwanakijiji atakapojitokeza mbel;e ya watanzania,nitaendele akumpelekea taarifa Mkuuwa kaya kuhusu yasemwayo hapa,na nitaendelea kumponda kama atafanya yasiyofaa hapa hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…