Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Jinga wewe....watu wasifanye siasa kuhofia wewe kuwachukia?

Ulitaka ajitangaze kwa station ipi?

anza kuwachukia wazazi wako kwa kukuleta duniani...
 
Hivi unavyoropoka una ushahidi, mbona Akili Za watu wengine Ni Kama wamepakaziwa?! Mtu anaropoka una ushahidi gani, Mara kahonga wadhamini 870,000 we umetoa wapi ushahidi ..!

Kama na yeye ni mmoja wa waliohongwa ni ngumu sana kutoka hadharani maana sheria inasema wote wana makosa, ila kama anakisia tu siyo haki, ingawa bodaboda walikuwa wakitoka kwenye mikutano yake walikuwa wanasema kuwa wamepata kitu sasa sijui na wao wanaweza kuwa wana chuki binafsi maana moyo wa mwanadamu hakuna anayeweza kuufahamu
 
Ukiona manyoa ujue kaliwa. SOMA HAYA:-

Wapambe wakuu wa Lowassa kitanzini

Posted by: Mwandishi Wetu
MAKADA wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walio pia vinara wakubwa wa kumuunga mkono waziri mkuu aliyejiuzulu kwa shinikizo la bunge mwaka 2008, Edward Lowassa, katika kampeni ya kusaka urais wa Tanzania, wamehojiwa kwa saa kadhaa na Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho mjini Dodoma. Anaandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kamati hiyo tangu jana ilikuwa katika vikao vyake ikichambua majina ya makada wa CCM walioomba uteuzi wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. Upepo ulibadilika kuanzia asubuhi leo baada ya wapambe wa Lowassa kukutwa wanaitwa kuripoti mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.
Kamati hiyo pia inamjumuisha Katibu Mkuu Kanali Abdulrahman Kinana, mwanasiasa ambaye amekuwa wazi katika kupinga mwenendo wa ukiukaji wa taratibu za kuendesha mambo ndani ya chama ikiwemo suala la harakati za kutafuta uteuzi wa kugombea urais.
Mmoja wa makada-wapambe wa Lowassa waliohojiwa na kamati hiyo kuhusu masuala ambayo hayakuwekwa wazi na uongozi wa CCM, ni Kingunge Ngombale-Mwiru, kiongozi mstaafu aliyepata kuwa waziri wa serikalini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Taarifa kutoka mjini Dodoma zimesema kwamba Kingunge ambaye amebadilika safari hii na kuwa muungaji mkono maarufu na wa waziwazi wa Lowassa, alihojiwa kwa saa mbili, akianzia saa 8 mchana.
Kingunge alijitokeza hadharani akimtetea Lowassa dhidi ya tuhuma za ufisadi na matumizi ya fedha katika harakati za kutafuta urais na juzi alisema wazi kuwa angependa kuona chama kinatenda haki kwa wagombea wakati huu kinapofanya vikao vya maamuzi mjini Dodoma.
Maelezo yake yamejenga taswira kwamba huenda Lowassa akaenguliwa mapema kabla ya kufika kwenye NEC, matokeo anayoamini yatakuwa ni kumuonea kwani “hana ubaya wowote na kama ni fedha basi na wenzake pia wanatumia fedha.”
Makada wengine waliohojiwa na Kamati ya Usalama na Maadili ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ambaye aliingia kikaoni baada ya Kingunge kutoka kuhojiwa.
Hao wamekuwa wakisikika mara kwa mara wakishambulia wenzao walio katika makundi mengine ya wasaka urais ndani ya chama hicho, kiasi cha baadhi yao kumfungulia kesi Paul Makonda, kijana wa CCM ambaye amejipatia umaarufu kwa kumshambulia Lowassa, akisema ni kiongozi asiyefaa kutokana na kupenda kutumia pesa kutafuta uongozi.
Lowassa ni mmoja wa makada sita waliofikishwa mbele ya Kamati ya Usalama na Maadili ya Mangula kwa tuhuma za kukiuka taratibu za kutafuta urais na wakapewa adhabu ya kutogombea uongozi kwa miezi 12, lakini adhabu hiyo ilikwenda mpaka hivi karibuni ilipotangazwa kuwa imeondolewa.
Lowassa ambaye alilazimishwa kujiuzulu kufuatia kashfa ya kuingilia utaratibu wa zabuni ya mkataba wa kufua umeme iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond, iliyothibitika kutokuwa na uwezo wa kifedha, vifaa na utaalamu, amekuwa akilaumiwa na wakuu wa chama kwa kutumia fedha kugawa chama akikusanya makundi ya wanachama.
Mbali na Lowassa, wengine waliowekwa kitimoto na Chama ni Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri wa Kilimo, Steven Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Wote hao wameomba kuteuliwa kugombea urais.
 
Hapo mtoa mada umeonyesha kuwa wewe ni Bendera hufata upepo huna hoja bali umepandikiziwa chuki tu,

Nimepandikiziwa chuki na vitendo vinavyoendelea. Kawaida watu wanaoshindwa huwa wanatafuta sympathy ya watu ndio maana anahangaika kuonyesha anaonewa wakati hata maamuzi hayajafanywa
 
Hivi unavyoropoka una ushahidi, mbona Akili Za watu wengine Ni Kama wamepakaziwa?! Mtu anaropoka una ushahidi gani, Mara kahonga wadhamini 870,000 we umetoa wapi ushahidi ..!
Ukitaka kujisafisha kutoka kwenye uchafu fulani si lazima ushike kila mkono wa mtanzania, we jisafishe tu kwa kununua vyombo kadhaa vya habari na watu flani wenye ushawishi katika jamii basi unakuwa umemaliza wengine watafuata mkumbo kama wewe, hiyo hoja eti kahonga watu 870000 wamehongwa? Ni mjinga tu ndiyo hatajua nini kimefanyika
 
akatwe nchi ipate kupumua maana mijitu yenye uroho inakula weee,inajichokonoa inatapika halafu inakula teeenaaa,inakuja kwa wananchi na kutoa mapovuuu weee,kelele luuundooooo.
 
Nimekuwa nikiona nguvu kubwa inayotumika hasa na vyombo vya habari kumfagilia lakini katika siku hizi mbili naona kama kanunua haka ka channel kanaitwa Channel Ten. Kwanini anatumia nguvu kubwa hivi? Jana usiku kukawa na kipindi maalum cha yule mzee fisadi wa stand ya Ubungo, leo from nowhere eti kukatwa kwa Lowassa kumekuwa mjadala! Shame on You Lowassa

Mwanzoni ulikuwa unampenda?
 
Weye nawe, maandalizi yote haya aliyofanya huyu mzee unataka akatwe ili iweje, a RIP kwa Shell na BP

Kufuru ya Lowassa.jpg
 
Nimekuwa nikiona nguvu kubwa inayotumika hasa na vyombo vya habari kumfagilia lakini katika siku hizi mbili naona kama kanunua haka ka channel kanaitwa Channel Ten. Kwanini anatumia nguvu kubwa hivi? Jana usiku kukawa na kipindi maalum cha yule mzee fisadi wa stand ya Ubungo, leo from nowhere eti kukatwa kwa Lowassa kumekuwa mjadala! Shame on You Lowassa

Yani thread yako kwa mtu makini akiisoma tu anajua una wivu wa kike.
 
Yani thread yako kwa mtu makini akiisoma tu anajua una wivu wa kike.
Mi nadhani we ndio una tabia za kike coz wanaume hushindana kwa hoja ila hawa mama zetu huwa wanajenga hoja baada ya kutukanana
 
Nimekuwa nikiona nguvu kubwa inayotumika hasa na vyombo vya habari kumfagilia lakini katika siku hizi mbili naona kama kanunua haka ka channel kanaitwa Channel Ten. Kwanini anatumia nguvu kubwa hivi? Jana usiku kukawa na kipindi maalum cha yule mzee fisadi wa stand ya Ubungo, leo from nowhere eti kukatwa kwa Lowassa kumekuwa mjadala! Shame on You Lowassa

Mh. Membe wacha papara zako, kama unataka njia mdebwedo ya urais basi haiwi hivi, watu tunataka rais mkali na si mbabaishaji kama wewe na wenzako.
 
Hizi nyimbo za Lowassa sijui nani ndani ya CCM karibu zitakoma,ifikapo 25 mwezi wa kumi UKAWA wanakuja kuua kabisaa.
 
Uende naye wapi wakati ni mume wa Mtu kwanini wewe usiende na mumeo?

daaah aiseee,kumbe rushwa iz harmful kwa kweli, i never knew kuwa lowassa ni mumeo? sisi tuna issue nae kisiasa mambo yenu ya unyumba uko peke yako mrembo!
 
Mh. Membe wacha papara zako, kama unataka njia mdebwedo ya urais basi haiwi hivi, watu tunataka rais mkali na si mbabaishaji kama wewe na wenzako.

Kama una uhakika wa kushind, unasema unakubalika kwanini utumie nguvu nyingi namna hii kununua media?
 
Nimekuwa nikiona nguvu kubwa inayotumika hasa na vyombo vya habari kumfagilia lakini katika siku hizi mbili naona kama kanunua haka ka channel kanaitwa Channel Ten. Kwanini anatumia nguvu kubwa hivi? Jana usiku kukawa na kipindi maalum cha yule mzee fisadi wa stand ya Ubungo, leo from nowhere eti kukatwa kwa Lowassa kumekuwa mjadala! Shame on You Lowassa

Hujui kama LA channel kenyewe ka rostam siku hizi?ameshakanunua kwa hiyo lazima wakatumie sawasawa kumpamba nyangumi mwenzao.huyu mzee msameheni maana amesharudi utotoni.
 
Mi nadhani we ndio una tabia za kike coz wanaume hushindana kwa hoja ila hawa mama zetu huwa wanajenga hoja baada ya kutukanana

Anza kutafuta ndimu za kulamba maana bwana Ngoyai ndio rais wako wa awamu ya tano.
 
Anza kutafuta ndimu za kulamba maana bwana Ngoyai ndio rais wako wa awamu ya tano.
Mimi sina tatizo na Lowassa kushinda au kutoshinda, tatizo langu ni haya malalamiko yake anayoyatoa kabla hata maamuzi hayajafikiwa. Ana tatizo gani?
 
Back
Top Bottom