Lowassa amkosoa Kikwete

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,541
2,000
Gazeti la Tanzania Daima limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Monduli ametofautiana na JK kuwa yeye anaamini nchi itangulize elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.....

Lowassa amkosoa Kikwete

• Asema elimu kwanza, kilimo baadaye

na Salehe Mohamed, Dodoma

ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema serikali inapaswa kutanguliza Elimu Kwanza badala ya Kilimo Kwanza, ili kuwawezesha wakulima na wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu shughuli wanazofanya.

Lowassa alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, mjini hapa baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kuongeza kama elimu itapewa kipaumbele zaidi kuna kila dalili Tanzana ikapiga hatua katika nyanja za kilimo, uvuvi, ufugaji na nyinginezo.

Alisema mkulima mwenye elimu ya kutosha hataweza kulima kilimo cha kisasa pamoja na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao yake.

“Mimi naona tungetoa nafasi kwa Elimu Kwanza halafu ndiyo ije hiyo ya Kilimo Kwanza; kuna nchi zimeendelea zaidi kwa sababu walianza kuwekeza kwenye elimu, naiomba serikali kuliangalia suala hili kwa umakini zaidi,” alisema Lowassa.

Aliongeza kuwa serikali ya sasa inapaswa itafute mbinu madhubuti ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambalo linawafanya vijana wengi kukimbilia mjini kwa lengo la kutafuta kazi.

Alisema tatizo hilo linaweza kutatuliwa iwapo huduma muhimu za kijamii, pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi zitapelekwa vijijini.

Wakati akizindia mpango wa Kilimo Kwanza, Rais Jakaya Kikwete alizitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza na kufanikisha mpango huo akisema awali ushiriki wa sekta hiyo ulikuwa dhaifu hali iliyopelekea kudhoofika kwa mipango mbalimbali ya kilimo iliyowahi kutangazwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, ambaye alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Pinda, alisema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lisipoandaliwa mikakati madhubuti litakuja kuiyumbisha nchi na kuleta mvurugano.

Alisema nguvu kazi kubwa ya sasa ni vijana na hawana kazi hivyo ni vema serikali ikajenga mazingira bora ya kuwawezesha kiuchumi pamoja na kujenga viwanda vitakavyosaidia kutoa ajira.

“Ukosefu wa ajira ni bomu la muda, tusipokuwa makini likija kulipuka nchi haitoweza kukalika, tuandae mazingira mazuri yatakayosaidia kuwepo kwa viwanda au kuwawezesha kiuchumi,” alisema Lipumba.

Alibainisha kuwa Waziri Mkuu ana wajibu mkubwa kuhakikisha kunaundwa Tume huru ya Uchaguzi ili kuepusha mizengwe inayotokea mara kwa mara kwenye chaguzi.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema, alisema Pinda ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hivyo ni vema akautumia kurekebisha masuala mbalimbali ambayo ni kero kwa wananchi ikiwemo umaskini.

Sherehe za kuapishwa kwa Pinda, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na viongozi mbalimbali.

Wakati huo huo, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesusia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikiwa ni msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ambaye wanadai alipata ushindi kwa sababu ya kuchakachua (kuiba) kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Mheshimiwa Lowassa amesema bila ya raia kuwa na uelewa wa kutosha hata hicho kilimo kwanza utekelezaji wake utakuwa mgumu..............

Maono yangu yananiongoza kuamini ya kuwa JK hana mpango wa kumweka Lowassa kwenye baraza la mawaziri kwa sababu siyo za uadilifu au uchapaji kazi - JK hajali sifa hizo katika uteuzi zake na huzitaja tu ili kumwaga changa kwa wapigakura tu- lakini JK anamwona Lowassa atavuruga hesabu zake za kumrithisha Uraisi mzanzibari ambaye JK atamwandaa hivi sasa kwa madai ya kuimarisha muungano huku anaendeleza ajenda ya siri ya kuhakikisha maamuzi ya uanzishwaji wa mahakama za kadhi na nchi hii kujiunga na OIC hayatahojiwa na serikali inayoongozwa na mkristu...........bila ya kujali chama anachotoka................

Ninauhakika ya kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo nchi hii itakuwa imejiunga na OIC na mahakama za kadhi kuanzishwa .......................mbali ya JK jana kudai ya kuwa kuna nyufa za udini na serikali yake itafanya juu chini kuzishughulikia.................lakini ukweli ni kuwa kazi kubwa atakayoifanya kwa miaka mitano ijayo ni kuzikuza nyufa hizo kwa kutoa upendeleo kwa dini yake...............

Lowassa haya yote amekwisha kuyaelewa na ndiyo maana anaonyesha ghadhabu zake kwa kutofautiana na JK hadharani.................
 
Lorah

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
1,193
0
Sijui bora zimu likujualo......

Huyu Kikwete nilivyomwamini ndo anafanya madudu yote haya...

Nilitoa jasho 2005 kumpigia kampeni na t-shirt na kanga (sikupewa bure nilinunua kwa ofisi zao Dodoma) leo hii kumbe nililamba garasha...

Jamani mungu unihurumie...... Kweli sikuwatendea watu wako haki kwani nilikimbia kijiji hiki na hiki kuwaambia watu walioniamini na kuniheshimu kuwa kikwete anafaa na ndie chaguo la mungu...

Nakumbuka babu mmoja aliniuliza unadhana atakuwa mzuri kama mchonga meno??

Nilimjibu kabisaaaa na kweli yeye alikuwa hana lengo la kupiga kura alienda kupiga kura kwa ushawishi wangu...

Leo hii naona haya kwa kweli nafsi inanisuta mnoo... Naombeni watanzania wenzangu mnisamehe.... Shetani nae anapindu za kujivunia watu wake.....
 
Ngangasyonga

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
455
0
Naomba kuungana na JK na Mzee wangu Kayanza, mtu akishiba ni rahisi kufanya maendeleo mengine, uwezi kukaa darasani na njaa asilani. NI lazima tuwe na uhakika kuwa kesho tutakula nini!! hivyo ni rahisi kukaa darasani na masomo fomula, definitions, calculas, yoote yaho yaka gota kichwani kwa makini. NJAA HAINA ADABU, watu washibe kwanza ndio akili itafanyakazi. So what I conclude, JK na Kayanza keep it up!! KILMO KWANZA MAZEEE!!
 
Jamani huu ujumbe umezingua roho...............................But you will never walk alone...........
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,541
2,000
Naomba kuungana na JK na Mzee wangu Kayanza, mtu akishiba ni rahisi kufanya maendeleo mengine, uwezi kukaa darasani na njaa asilani. NI lazima tuwe na uhakika kuwa kesho tutakula nini!! hivyo ni rahisi kukaa darasani na masomo fomula, definitions, calculas, yoote yaho yaka gota kichwani kwa makini. NJAA HAINA ADABU, watu washibe kwanza ndio akili itafanyakazi. So what I conclude, JK na Kayanza keep it up!! KILMO KWANZA MAZEEE!!

Tatizo la hii hoja yako ni kuwa imekosa mashiko ya aina yoyote ile..............................

Kabla ya 2005 JK kuingia Ikulu alikuwa Ni waziri kwa miaka 22 kwa hiyo alikuwa ameshiba sana na hata kuvimbiwa..................kumbuka ufisadi wa Majenerata ya Tanesco pale Ubungo.................yeye ndiye aliyekuwa mwasisi wake mkuu...................

Ukija kayanza mwaka 2005 tayari alikuwa naibu Waziri kwa miaka 5 na kabla ya hapo alikuwa Ikulu akilamba asali na kunyonya maziwa.................kwa hiyo na yeye alikuwa kashiba sana na pengine kavimbiwa ile mbaya........................

Sasa miaka 5 ya kwanza ya JK mbona umasikini umeongezeka kwa kasi na kashfa nazo zimetanda kila kona ya nchi?

Kwwa hiyo tunalojifunza hapo ni kuwa hata hawa mabwanyenye wakishiba vipi huwa hawadondoshi kwenye meza zao ili mimi na wewe tuweze kuokota hata zile punje punje za hapa na pale..........................kwa hiyo kwa kifupi sana hawana msaada...................
 
kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,022
1,500
kwa upande mmoja naweza kuungana na Lowasa katika hili elimu ya darasani na elimu ya street ni muhimu ili tuweze kufanikiwa. pamoja na hayo tutafanikiwa tukiwa na uadilifu na wachapa kazi.!!
 
kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,715
2,000
Acha waanze kutofautiana wao kwa wao baadae watatuambia uozo wote ulioko ndani
 
tunalazimika

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,099
1,195
Rutashubanyuma wewe ndo mdini mkubwa maana umeamua kutuwekea na bible kwenye picha yako-ni kweli JK ana mapungufu kibao, lakini wewe ni mbaya zaidi kwani-unataka kutupandikizia maslahi yako wana JF-hufai kabisa, mimi pia najutia kuwa sehemu ya JK mwaka 2005 na nilishiriki ipasavyo kuweka madarakani na sasa najuta-lakini si unganishi habari hizo na udini unao uleta wewe wa kijinga kabisa
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
Tatizo la hii hoja yako ni kuwa imekosa mashiko ya aina yoyote ile..............................

Kabla ya 2005 JK kuingia Ikulu alikuwa Ni waziri kwa miaka 22 kwa hiyo alikuwa ameshiba sana na hata kuvimbiwa..................kumbuka ufisadi wa Majenerata ya Tanesco pale Ubungo.................yeye ndiye aliyekuwa mwasisi wake mkuu...................

Ukija kayanza mwaka 2005 tayari alikuwa naibu Waziri kwa miaka 5 na kabla ya hapo alikuwa Ikulu akilamba asali na kunyonya maziwa.................kwa hiyo na yeye alikuwa kashiba sana na pengine kavimbiwa ile mbaya........................

Sasa miaka 5 ya kwanza ya JK mbona umasikini umeongezeka kwa kasi na kashfa nazo zimetanda kila kona ya nchi?

Kwwa hiyo tunalojifunza hapo ni kuwa hata hawa mabwanyenye wakishiba vipi huwa hawadondoshi kwenye meza zao ili mimi na wewe tuweze kuokota hata zile punje punje za hapa na pale..........................kwa hiyo kwa kifupi sana hawana msaada...................

Tatizo la pinda naona alikaa sana ikulu hakuwahi tumbelea Tanzania, sasa ndio anaona hali halisi ya watanzani
 
HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
0
Waungwana hutoa sifa panapositahili na kutoa sifa pasipositahili. Kwa habari hii mimi naungana na Lowassa.

Ila kwa kuwa serikali ni ya CCM na yeye ni kiongozi ndani ya CCM kwani nini asitumie vikao vya CCM kueleza hii maada ambao mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana nayo.

Mhe Lowassa nakushauri peleka hoja hii kwenye vikao ile sera za chama chenu ziende na zile za chama mbadala. CCM isione aibu kuchukua hii sera na kuitekeleza kwa vitendo. Kwani nia na madhuni ni kuendeleza taifa. Nadhani kwenye uchaguzi kuna chama kilichokuwa kinasema sera yake ingekuwa na pamoja elimu tena ya bure.

Bila elimu ufahamu wa binadamu katika kutenda kazi zikiwemo za kilimo ni hafifu.
 
Kaisikii

Member
Nov 10, 2010
74
0
Njama yao hiyo mumuone anafaa uraisi 2015 kalagha baoo hiyo inaitwa ccm wajanja na wanambinu ajabu....kampeni ndo zishaanza hizo.kwanza gazeti linamilikiwa na nani hilo...kama sio ....
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
Hapo naungana mkono na fisadi lowasa! Huyu jamaa ni mzuri isipokuwa anatamaa sana!
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,520
1,225
Kwenye vikao vya chama hawezi kutoa hoja hiyo kwa kuwa huwa kuna ajenda muhimu za kujadili,akiingiza hoja kama hii katika vikao vyao wanaweza kumnyang'anya kadi ya chama ndio maana alipopata nafasi ya kuongea kaamua kulisemea.
Kwa mara ya kwanza tangu auache uwaziri mkuu ndio kauli yake ya kwanza ya maana kuitoa hata kama inaonekana inapingana na mipango ya wengine
 
Ki tochi

Member
Oct 19, 2010
49
0
kila penye kutofautiana kuna ukweli ndani yake.
Elimu kwanza ndo mpango,
Kilimo kwanza inabidi mtu uwe risk taker kutokana na hali ya hewa kwa miaka hii ilivyobadilika.
Je bila elimu tutaweza kuwa risk taker.

Japo watu wameelimika mpaka leo TZ ss ni WAOGA wa kujaribu mambo.
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,666
2,000
Ili ni fisadi ambalo linaanza kujisafishia njia ya kuelekea uchaguzi wa 2015 - hamna lolote.
 
achibweni

Member
Nov 17, 2010
22
0
hapo pana majibu mengi sana...

'Anyone who is capable of getting themselves made President should on no account be allowed to do the job' Douglas Adams
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,273
2,000
kila penye kutofautiana kuna ukweli ndani yake.
Elimu kwanza ndo mpango,
Kilimo kwanza inabidi mtu uwe risk taker kutokana na hali ya hewa kwa miaka hii ilivyobadilika.
Je bila elimu tutaweza kuwa risk taker.

Japo watu wameelimika mpaka leo TZ ss ni WAOGA wa kujaribu mambo.

Elimu kwanza hiyo si agenda ya CHADEMA?
 
Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,395
1,500
hata kuoza kwa papai kunategemea sana uozaji wake,
kwa eneo hilo lowasa ameonesha kuwa yeye ni papai lililooza upande mmoja tu.
ni mawa yangu tu............teteteteteee!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom