Lowassa alifuata nini Iringa?

Lowassa alifuata nini Iringa?

ameonekana kwenye vyombo mbalimbali akiwa miongoni mwa wageni kwenye JUBILEE YA MIAKA 25 YA UASKOFU WA NGALALEKUMTWA , LAKINI IKUMBUKWE KWAMBA CHAMA CHAO CHINI YA KAMATI YA MANGULA KILIWAONYA WALIOITWA WASAKA URAIS kwa NJIA ZA PANYA KUTUMIA SHUGHULI KAMA HIZI ILI KUTAFUTA KUUNGWA MKONO , SASA CHA KUSHANGAZA AMEONEKANA KWENYE SHUGHULI AMBAYO SIDHANI KAMA WABUNGE WA KIGENI WALIALIKWA ! JE ADHABU YAO IMEISHA ?

Muache afanye yake, kwani kisu kikali anacho na vipi asile Nyama.!
Kelele za mpangaji tu..!
Kama ipo ipo tu.!
Kila jambo atalo fanya Edi ni Nongwa sasa.!
 
Kina lowasa hawajazuiliwa kwenda kwenye jublee, walichozuiliwa ni kushiriki harambee. Au umetumwa na jk au membe?
 
ni ujinga kujiapiza kwa kukubali kwa kukutawaliwa na mwizi aliyehiba kodi za mama yako na bibi zako wanaoangaikakila siku kwa kutafuta mkate wa siku
Mtake mstake, Lowasa ni Kiongozi katika hii nchi. Cheo cha Askofu sio cha kijiji. Na kwamsiofahamu Baba Ngalalekumtwa ndiyo mwenyekiti wa baraza la maaskofu. Hivyo basi shughuli ya jubilee yake lazima watu kama Lowasa waalikwe
 
ni ujinga kujiapiza kwa kukubali kwa kukutawaliwa na mwizi aliyehiba kodi za mama yako na bibi zako wanaoangaikakila siku kwa kutafuta mkate wa siku
Tatizo mna chuki binafsi na Lowasa na mnaona Lowasa ndoo mchafu kuliko wote? Hivi kuna kiongozi hata mmoja wa CCM ambaye ni msafi? Nitajie. Kwahiyo ili kuondoa uovu ni lazima mapambano yalenge mfumo na sio watu binafsi. Sema CCM NO. Halafu mtu kama wewe siwezi kuamini kama unaushahidi wa wizi wa Lowasa zaidi ya maneno ya mitaani.
 
Muache ahangaike, uyo kishajiengua 2015. Uraisni utakatifu wala sio kutumia nguvu wala umungu mtu hapa duniani. Rais ajae ni yule asiekua na makundi kwan akiingia ikulu haendi na jamaa zake na kundi lake na uongoz utakua wa kiuadilifu zaid.
Tuwaepuke watu wanaotaka urais kwa nguvu zao zote hata kama wanazuiwa au wanapotoka kimaadili. Tanzania ni ya watanzania
Mtachonga sana lakini hamtafanikiwa. Mhe. hajaenguliwa na wala hatajiengua!! Tunahitaji Rais ajaye awe mtu wa kujitambua na mwenye agenda siyo hao wa kuchongwa na kusindikizwa sindikizwa. Mhe. Lowasa anatosha sana kuingia ofisi ya Magogoni
 
Kina lowasa hawajazuiliwa kwenda kwenye jublee, walichozuiliwa ni kushiriki harambee. Au umetumwa na jk au membe?

sijatumwa mkuu , nilitaka tu kufahamu kama kwa sasa KUJIPITISHA PITISHA ni ruksa .
 
mtaanza kufikiria lowasa Kwa nini kanya saa sita badala ya saa nane!
 
Huwa najiuliza sana, hivi Lowassa anautafuta urais wa nini wakati afya yake imedhoofu kiasi hicho? Na kama urais ndio unatafutwa hivyo, basi tujiandae kwa mateso.

Mateso gani?
 
Mtake mstake, Lowasa ni Kiongozi katika hii nchi. Cheo cha Askofu sio cha kijiji. Na kwamsiofahamu Baba Ngalalekumtwa ndiyo mwenyekiti wa baraza la maaskofu. Hivyo basi shughuli ya jubilee yake lazima watu kama Lowasa waalikwe

Nakuunga mkono,kwa shughuli kama ile huwezi kumuwekea mtu kikwazo cha kutoshiriki kwani ni imani ya mtu binafsi.
 
Aalikwe kama waziri mkuu mstaafu, sorry sio mstaafu, aliyejiuzulu, sorry tena leo nachapia sana sio aliyejiuzulu ila aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa shinikizo la juu kutokana na kashfa nzito ya ufisadi wa RICHMOND.

Siyo lazima aalikwe ktk shughuli ya kiimani mtu yeyote alikuwa na nafasi ya kushiriki bila kujali umbali uliopo.
 
Ccm Maovu y lowassa mnayajua mpaka mkamwajibisha hatutarajii mtampitisha kugombea urais wakati uchafu wake mnaujua

Haki ya kugombea uongozi ni ya kila mwananchi wa taifa letu ili mradi tu atimize mashariti.
 
utanilaumu bure mjomba ! kamati ya mangula ndiyo iliyowakataza KUJIPITISHA PITISHA ,labda kama KISWAHILI KIMEBADILIKA .

Mtaumiza vichwa vyenu bure,ccm mnawajua kuwa ni ukoo wa panya kila mtu ana sharubu.
 
nisingeshangaa kama mbunge wa eneo husika angehudhuria , lakini kutoka MONDULI hadi IRINGA , tena bila MADARAKA YOYOTE YA KITAIFA ! JE HUKO SIYO KUJIPITISHA PITISHA ?

Kaka yule bado ni muumini,hata kama.
 
Mtachonga sana lakini hamtafanikiwa. Mhe. hajaenguliwa na wala hatajiengua!! Tunahitaji Rais ajaye awe mtu wa kujitambua na mwenye agenda siyo hao wa kuchongwa na kusindikizwa sindikizwa. Mhe. Lowasa anatosha sana kuingia ofisi ya Magogoni

Panapo majaliwa ya mwenyezi mungu,kaka husiseme lazima.
 
sawa , lakini ameruhusiwa KUJIPITISHA PITISHA ? HIVI UNAELEWA MAANA YA KUJIPITISHA PITISHA ?

Mkuu,kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa huyu jamaa anakuwa anajijengea jina ktk jamii ili wakati wa kampeni iwe rahisi kwake kujinadi.
 
Mkuu na wewe ume onja kitei na sumu pale Ilboru? maana hiyo terminology ya Ilborians... Bahati mbaya sana kwa sasa Lowassa hazuiliki! presence yake inawaogofya akina Joka la Mdimu na watu wake ....

Mkuu huyo Punguani hawezi kuwa Xilborian hata kwa mwezi mmoja,
Watu waliopitia pale wako huru ki mawazo sio kama huyo ambaye ni fuata upepo.
Unless aligush kuingia pale kwa iliyokuwa himaya ya Kitemango.
 
Back
Top Bottom