Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,293
- 6,895
Ni ujinga kumdhibiti Lowassa namna hiyo, hata akifanya yote hayo hofu ni nini kwa CCM? Ni nani anayeweza kukataa mwaliko wa kiongozi wake wa dini?
Kama umekuwa katika malezi ya imani ya dini, ni vigumu sana kukataa mwito wa kiongozi wako wa dini, na mara nyingi huonekana ni heshima maalum.
Hebu mwacheni Lowassa aishi anavyoweza, kwani mwisho wa siku si chama chenu wenyewe ndicho kitakachoamua nani awe mgombea wenu.
Kiukweli kwa namna mnavyoendesha suala la Lowassa, CCM mnajitia aibu sana. Mnaonesha mnavyoona alivyo juu ya chama chenu, alivyo na nguvu kuliko chama chenu.
Ova