hivi huyu alisoma wapi?
HIYO INAITWA "MANGULO" KWA WALE WATU WA ARUSHA WANAELEWA..NDO SLANG HIYO..KWA LUGHA NYINGINE.."USANII"
Alikuwa waziri wa ardhi..hivo alishiriki kikamilifu kuiuza nchi yetu!Hivi mnaielewa hii CV ya mheshimiwa Lowassa hapa chini? Jamaa hayuko makini kabisa, yaani ofisi nzima ya Waziri Mkuu wanashindwa kuona kwamba hapa kuna mambo sio sahihi?
Tanzania Government Prime Minister 2006
Ministry of Water and Livestock Development Minister 2000 2005
Ministry of Lands, Human Settlement Development Minister 1993 1995
State, Prime Minister's Office and First Vice President Minister (Judiciary &Parliamentary Affairs) 1990 1993
Arusha International Conference Centre Managing Director 1989 1990
State, Vice President's Office Minister for Environment & Poverty 1988 2000
apparently alisoma Mlimani na Bath Univ.
Unfortunately inelekea kuwa Mlimani hutoa mchanganyiko maalum: Pumba na mchele vyote vinapita tu.
Hebu angalia Alumni ya Mlimani: Mhe. Kivuitu, Rais Mseveni, Mhe. Lowasa, Prof Issa Shivji, Kichuguu (mimi), Mhe. Joseph Warioba, Mhe. Kikwete, Prof Lipumba, Maalim Seif Sharif Hamad.
Yaani Kichuguu naona aibu kuwa nimechanganyika na pumba akina Kivuitu na Lowasa, ingawa vile vile naona ufahari kuchanganyikana na akina Prof Shivji.
Kichuguu,
Huenda na wewe ungelikuwa kwenye siasa Afrika, ungeishiwa kuwa kama hao waheshimiwa (Kwi kwi kwi!!!!).
Yaani ni balaa tupu, tatizo sio Mlimani, tatizo ni culture ya Waafrika kwa ujumla.
Watu wengi wanashindwa kuielewa JF kwa sababu we dare to speak openly wakati culture zetu nyingi ni uoga uoga na uongo. Mkubwa anajamba anasingiziwa mtoto. Labda sisi tuna nafasi kubwa ya kuleta change Tanzania. Hiki chombo inatakiwa hata kipate misaada ya wale jamaa wa civil society maana elimu ya JF ni kubwa kuliko NGO kibao TZ.
Yale aliyoambiwa Lowassa na tume ya Mwakyembe, kikawaida hayatakiwa kuongelewa kwa Afrika.
Kinachosikitisha tu ni pale sisi wenyewe tunavyitoka hapa na kwenda kuwa mafisadi huko ardhi, UDSM, hospitali na kwingineko. Hii vita inatgakiwa isiishie kwa wanasiasa na badala yake iwe mpaka walio chini ambao wananyanyasa wananchi wetu.