Lowassa aisambaratisha Kamati kuu ya CCM, Nape hoi, Mswekwa atokea mlango wa uwani, Chiligati kwisha

Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!

umeshajua sasa umeingiaje hapo?
 
Nape,
Hebu tufafanulie yafuatayo:
-Kigezo mlichotumia kuamua kura za maoni kurudiwa kinatumika wakati wote au katika mazingira flani tu?
-Kigezo kile kiliondolewa kwa nini kwenye KATIBA ya JMT kwenye kura za URAIS?
-Siri zenu hata za ndani ya Secretariet ya watu wachache kabisa zinavujaje kirahisi hivo?
-Nguvu walizonazo baadhi ya wanachama wenu kuliko hata chama na vikao vyake mnazikabili vipi?
Pole sana Nape. Umeamua kupambana ukiwa ndani ya CCM ya aina hii ni kazi kweli. Mtangulize Mungu tu na isimamie kwa dhati dhamira yako hii njema.
 
Hoja ya kutoa matokeo ya kura za maoni Facebook nayo ni mufilisi, lini nimewahi kutoa matokeo hayo kwa chaguzi zote za kura za maoni ndani ya Chama changu? Hakika nawasumbua vichwa vyenu mafisadi na hii ni faraja kubwa kwangu!!!
...husilidhike na kufarijika na kuwasumbua vichwa mafisadi Nape,watanzania tunataka kuona mafisadi wakijivua gamba sio kuumizwa vichwa kwani baada ya kuwaumiza vichwa watameza pandol watapona alfu wataendelea kutufanyia ufisadi...
 
Mkuu Wildcard...
Umejenga hoja nzuri... Wacha tumsubiri Nape,atuweke sawa kwa hayo...
 
huyo lowassa wenu hana lolote tulimpa kazi ya kuhakikisha jimbo la arusha mjini linabaki ccm alishindwa kuonyesha hizo nguvu zake jimbo likapotea,leo nguvu za kaskazini anazitoa wapi?ana nguvu monduli huko labda

Lowassa ni mtu mdogo sana kwa Nape,nape anaingia kwenye kamati kuu lowassa anaishia kwenye viwanja vya bunge..nec yenyewe tunamng'oa atake asitake hatutajali kiharusi chake wala kutetereka kwa afya yake.
KK,
Pambaneni na mfumo. Msipambane na mtu. Kwa NCHI ilivyooza sasa, LOwasa ni masiha wao. Hayuko peke yake. Irudishieni taasisi ya CCM na vikao vyake nguvu ilizokuwa nazo enzi za Mwalimu. Nguvu hizi zilihamishwa kinyemela kwenda kwa watu na makundi yao katili pale mlipoanza kuwakumbatia WAFANYABIASHARA.
 
Hakuna namna ambayo Nape anaweza ukwepeka ktka hili.Yeye ndiye Katibu Mwenezi.Embu nipe kazi moja tu ya mtu anayeitwa Mwenezi.Acha fikra mgando mkuu.Embu niambie kwenye hiyo Blue Nape mpaka sasa anaimpact gani kwa Mafisadi zaidi ya jitihada za kweli toka CHADEMA. yOU NEED TO LEARN TO UNDERSTAND AND NOT CREAMING THE ACTIVITIES.
Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!
 
If you know your enemy and yourself you will not fear the result of a hundred battles to come but if you don't know neither yourself nor your enemy for every one win you will suffer a defeat

Mzazi Mnauye una bahati sana ya kupewa madaraka ukiwa mdogo lakini pengine bahati inaweza kuwa balaa kama isipoambatana na busara esp God's guidance , mkuu, kosa mlilo fanya ni kumwekea fitna Sioi wameru si watu wa majungu ndio maana wamepiga kura kwa hasira na unapomwita mtu wanae mweshimu wao fisadi usitarajie watakusikiliza hata kama kweli ni fisadi...............jimbo Arumeru amtachukua kama tu mta waachia wanasiasa wa hapo Arumeru hiyo kazi .....they know the terrain better ......CHADEMA wamekosea step kidogo kwa kumuweka John Mrema or Lema kuwa Kampeni Kamanda they will definite be beaten, nature ya wameru hawataki kabisa kuletewa mtu wakuja kuwaambia ambia mambo mambo ya kufanya bila wao kuwa wameomba msaada au ushauri CHADEMA tatizo lao kama kule Igunga ni utoto na mambo ya kihuni kama kupiga viongozi wa serikali hadharani .........this make them loose trust from prudent persons
 
Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!

VIjana wa magwanda wana wivu na unavyovimba kwenye V8

 
huyo lowassa wenu hana lolote tulimpa kazi ya kuhakikisha jimbo la arusha mjini linabaki ccm alishindwa kuonyesha hizo nguvu zake jimbo likapotea,leo nguvu za kaskazini anazitoa wapi?ana nguvu monduli huko labda

Lowassa ni mtu mdogo sana kwa Nape,nape anaingia kwenye kamati kuu lowassa anaishia kwenye viwanja vya bunge..nec yenyewe tunamng'oa atake asitake hatutajali kiharusi chake wala kutetereka kwa afya yake.

KIM kwani wewe ni nani?
Sasa kama EL ana kiarusi, ina maana CCM inataka kupitisha rais mgonjwa?
Hakuna wazima kwenye CCM?
 
Ni kweli uongozi wa Tanzania ni wa kuangalia nani ni nani na wala sio kafanya nini na anatarajia kufanya nini baada ya kuwa kiongozi. Jamii haimpimi mtu kwa kwa hoja zake na IQ yake bali ni mtoto wa nani, anatoka wapi wakati mwingine hata jinsia pekee inatosha kumpa mtu cheo cha uspika.

Kwa ujumla wa Tanzania tunarudi nyuma kuliko hata enzi za Ufalme, usultani na uchief. Hata Nape kaingia sababu ni Mtoto wa Moses, lakini je: ana Umoses ndani yake? Ukimpima kulinganisha na vijana wengine ndani ya CCM mizania ikoje? Siyoi na Sarakikya ni kadhalika.

Mwalimu alitukataza kuchagua viongozi kiimla kana kwamba wale waliozaliwa nje ya ufalme hawawezi kuwa na akili ya kuongoza. Hivyo sio kweli kuwa watu wasiokuwa unasaba na waliopata kuwa viongozi hawawezi kuongoza, tuwapime watu kwa hoja zao
 
Its a shame to see a Chama tawala hakitawaliki. SHAME ON YOU! Katibu wa uenezi anajibu hoja ya kushinda kwa mgombea kwa kusema mafisadi wanaumia kichwa!! what a shame! shalll I take this as a confession that there is what is called makundi in the main party? Kama ndivyo, kundi moja linaitwa mafisadi na kundi la pili linaitwa Nape or unt-fisadi? It's a shame bse to my understand at the level of Katibu mwenezi he has to neutralize (by words and action) mashabiki wa wagombea na kuinsist wawe pamoja na kufocus kwenye uchaguzi wa ubunge. Maneno kama katika ushindani lazima mmoja ashinde n.k ndio niliyoyategemea na sio kuonyesha wazi mpasuko uliopo!!! Kama chama kinachoendesha nchi hakijatulia kiuongozi tutaendelea kuwa omba omba na kutibu majeraha bila kuwa na mbinuu ya kuzuia au kujenga nchi. Siku zote walio vitani wanafikiria uhai wao zaidi ya maendeleo.
 
Mimi mwenyewe nashindwa kuwaelewa hawa jamaa wa TLP,CDM na wapinzani wengine wanajua kupambana na CCM ni shughuli nzito wanachosubiri wao na kufurahia ni pale ambapo CCM watagombana kama ilivyokuwa majimbo ya Iringa,Ubungo,Kawe,Mbeya,ilemela na kwingineko ili wao wapate jimbo kiurahisi na ndiyo maana wanashabikia kweli wakiona kuna kukosana kwenye jimbo baina ya wana CCM wenyewe nawaambieni wapinzani msahau haitatokea tena kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu 2010 sasaivi wana CCM wote wanajua hilo baada ya uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama tofauti zinaishia pale wanakwenda kwenye uchaguzi mkuu wa jimbo wakiwa kitu kimoja na kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM mpaka ushindi,hongera sana Sioi Sumari kwa ushindi mzuri sasa tunasubiri jimbo nakufahamu vizuri ni kijana mpole na mwenye msaamuzi ya busara hii ni zawadi kubwa kwa Wana Arumeru na kwa kuwa wanakufahamu vizuri watakuchagua kwa kura nyingi na kuwabwaga wapinzani!
 
Toa maoni yako kuhusu ushindi Wa Sioi huku akisaidawa na Fisadi mnayetaka ajivue gamba

Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!
 
Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!


Kaka Nape sikutarajia wewe kutanguliza maneno kama haya hapa janvini hasa hilo la wewe kuingiaje hapa? Tambua wewe ni Kiongozi katika chama tena Mwenezi. Haukupaswa kupambana na members hapa isipokuwa kutoa majibu yanayostahili kisiasa. Tunatambua mchango wako lakini pia nachukizwa na jinsi unavyowasilisha agenda hapa ukiwa kama kiongozi mkubwa wa chama. Hupaswi kuhamaki zaidi ya kuelimisha wale wenye duku duku kulingana na yanayozagaa katika vyombo vya habari. Maadam umeingia humu, nadhani ulikuwa na jukumu la ku-clear doubts kama mwenezi kwani tambua mabaya huvuma zaidi kuliko mazuri.

Jibu lilikuwa ni rahisi tu kuwa katiba imezingatiwa no matter how the process went, vile vile WanaCCM wa Arumeru wamepata fursa ya kumchagua yule wanaedhani kuwa atawawakilisha vyema. Kamati Kuu itafanya kazi yake kulingana na Mamlaka ya kikatiba iliyopewa na kisha kumtangaza rasmi mgombea atakaye peperusha bendera ya chama katika uchaguzi huo. Pia itambulike kuwa baada ya kutangazwa rasmi, huyu atakuwa mgombea wa chama na atasimamiwa na chama katika kumnadi na kupata ushindi.

Vile vile ulipaswa kujibu tetesi za mgawanyiko kama upo ama haupo full stop.
 
tatizo yetu yamefupishwa vizuri na Kipanya kwenye katuni hii.............

kipanya_6-1-2012_20120106_1167831708.jpg
 
Really? Ni makundi tu, yani mapenzi tu ya watu kwa mtu bila sababu ingine yeyote?

Hakuna tofauti ya itikadi labda kati ya Siyoi na Sarakikya au profile zao, wanavutia watu kwa sababu ya background gani, Sarakikya ni nani na Siyoi ni nani politically, professionally, experientially, hakuna? Kila mmoja ana represent ideals gani? Wanaowasapoti wana wanavutwa na nini, yani wanapenda sura ya mtu na sauti yake tu? Haiwezekani man, makundi tu? Really?

Basi siasa zetu zina vina na upeo mfupi kupita maelezo. Au labda ni waandishi wa habari ndio hawatafiti hivi vitu, manake nikisoma hizi taarifa za chambuzi za kisiasa natoka mtupu, natoka kama nilivyokuja, zaidi ya kujua Sumari ni mtoto wa marehemu Mbunge, Sarakikya ni mtoto wa Mkuu wa majeshi mstaafu, basi. Kwa kweli inapokuja kwenye uchambuzi wa sifa za nani tunataka atuongoze Watanzania vichwa vyetu ndani vimejaa chawa.

Kwani Nassari aliyemaliza kadigrii kamoja juzi, ndio kabisaaaa politically, professionally, experientially ZERO. Lakini kila jambo lina mwanzo, acha vijana nao waingie awe Siyoi au Nassari sawa tu maadam jumuia ya wameru inawapa ridhaa.
 
The reverse could be true. Sioi alipata kura chache katika uchaguzi wa awali kwa kuwa alipigiwa negative campaign na vigogo wa chama. Ndo maana hata katika awamu ya pili walijaribu kupiga negative kampeni hadharani kitu kilichowaudhi wajumbe hata kuamua kumpigia kura nyingi zaidi. BTW, kuna tetesi kuwa hata baadhi ya wagombea walishawishiwa kuingia katika kinyanganyiro ili kupunguza nafasi yake ya kupata kura nyingi. Hakika nguvu ya Lowasa inatisha.
Matola......Lowassa angekuwa Heavyweight Sioi asingepata kura 300 kati ya 1,000 kwenye uchaguzi wa kwanza kabla ya ule wa marudio......

Kuna tatizo kubwa sana ndani ya CCM Arusha na Arumeru.....Tatizo ambalo linaweza kupelekea CCM kushindwa uchaguzi wa Arumeru....Sidhani kama kutumia mapesa mengi kuwahonga watu wakuchague ni kigezo cha kuwa Heaveweight....

Heavyweight ni kama Nasari ambaye ameshinda kwa kishindo uteuzi ndani ya CHADEMA kwa kupata kura 808 ya kura kati ya kura 888 zilizopigwa.....Huyu ndiyo Heavyweight maana ameonekana ana nguvu sana kwa kukubalika kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura zilizopigwa na kapata kihalali bila hata kutoa Rushwa.....

Sidhani kama mwandishi makini wa Habari angeweza kuandika Habari kama hiyo eti 'lowassa aisambaratisha CC ya CCM'......Kiukweli CCM wana hali mbaya sana Arumeru.....Mgawanyiko wa CCM Mkoa wa Arusha ni hatari sana kwa hatma ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki...

NB..
Kumbuka kwamba mgombea wa CCM atatangazwa na CC tarehe 3,March......Lolote laweza kutokea....Vipi CC ikiamua kumpiga chini SIOI kwa tuhuma za rushwa ambapo watu wake wa karibu(katika kambi yake) wamekamatwa na TAKUKURU wakigawawa fedha kwa wajumbe......Ni mapema sana kusema Lowassa ameisambaratisha CC ya CCM.......Lolte laweza kutokea...
 
Back
Top Bottom