Lowassa aisambaratisha Kamati kuu ya CCM, Nape hoi, Mswekwa atokea mlango wa uwani, Chiligati kwisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa aisambaratisha Kamati kuu ya CCM, Nape hoi, Mswekwa atokea mlango wa uwani, Chiligati kwisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Mar 2, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa

  SIYOI AMBWAGA TENA SARAKIKYA

  Waandishi Wetu, Arusha

  KWA mara ya pili, wana CCM Jimbo la Arumeru Mashariki wamedhihirisha kuwa chaguo lao ni Siyoi Sumari baada ya kumchagua kwa kura 761 na kumtupa mbali mpinzani wake, William Sarakikya aliyepata kura 361 katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.Matokeo hayo ni kama ushindi kwa mojawapo ya kambi ndani ya CCM inayohusishwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa dhidi ya wanachama waliopo katika makundi mengine, ambayo yalikuwa yakipinga kwa nguvu zote kupitishwa kwa jina la Siyoi.

  Vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki nzima sasa, vimekuwa vikiripoti kuhusu mgawanyiko ndani ya chama hicho tawala kutokana kuwa na misimamo inayokinza kuhusu nani atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mdogo.

  Siyoi alianza kuzua mtafaruku ndani ya CCM pale suala la uraia wake lilipozua utata ndani ya kikao cha Sekretarieti ya chama hicho, hivyo kusababisha kutolewa kwa mapendekezo kwamba aenguliwe katika kinyang'anyiro hicho.

  Kundi linalomtetea limekuwa likilalamikia kile linachodai kwamba ni kuwapo kwa njama za kumtosa mshindi huyo kwa sababu kadhaa za kimakundi.

  Hata hivyo, Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokutana chini ya Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete kiliamuru kurudiwa kwa uchaguzi baina ya Siyoi na Sarakikya, kwa maelezo kwamba katika wagombea wote sita hakuna aliyekuwa amepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.

  Habari zaidi zilidai kuwa, hata baada ya kutolewa kwa uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi huo, mmoja wa vigogo wa CCM alituma mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu kwenda kumshawishi Siyoi ajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho, jitihada ambazo hazikufanikiwa kwani alikataa.

  Matokeo ya kura
  Matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa Saa 11:30 jioni na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, Sumari aliibuka na ushindi huo wa silimia 67.8 kati ya kura halali 1,122 zilizopigwa, dhidi ya asilimia 32.2 za mpinzani wake anayedaiwa kupigiwa chapuo na viongozi wa chama na Serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi taifa.

  Jumla ya kura 1,124 zilipigwa ambapo mbili ziliharibika na kura halali kubakia 1,122.

  Akitangaza matokeo hayo, Msekwa alilazimika kuanza kwa kumtangaza mshindi hali iliyofanya ukumbi kukosa usikivu kwa wapenzi, mashabiki na wafuasi wa Siyoi kuanza kushangilia.

  Msekwa alisema ameridhishwa na upigaji kura na matokeo hayo yameonyesha imani kubwa waliyonayo wana Arumeru kwa mgombea huyo.

  Baadhi ya wana CCM walidai kuwa kauli tata za Msekwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati katika ufunguzi wa mkutano mkuu maalum wa Wilaya ya Arumeru jana zilimponza, Sarakikya baada ya wajumbe kuamua kupiga kura za hasira wakipinga kile walichodai kushinikizwa kumchagua mtu aliyeelezwa anatakiwa na mfumo (system), wa Serikali na uongozi wa chama.

  Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliohudhuriwa na idadi kubwa ya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), maofisa usalama wa taifa na askari kanzu kutoka Jeshi la Polisi, Msekwa na Chiligati waliwataka wajumbe kutumia vyema kura yao kumchagua mtu atakayemudu na kuhimili vishindo vya upinzani kutoka vyama vingine vitakavyosimamisha wagombea.

  "Ndugu wajumbe napenda kuwakumbusha jambo moja muhimu kabla ya kupiga kura, leo hatuchagui mbunge, mnachofanya ni kupiga kura za maoni. Mgombea atateuliwa na kikao cha Kamati Kuu Machi 3, mwaka huu," alisema Chiligati.

  Wakati Chiligati akisititiza hoja hiyo, Msekwa alikuwa akitikisa kichwa kuonyesha kukubaliana na maneno aliyokuwa akiyasema Naibu Katibu Mkuu huyo huku baadhi ya wajumbe wakiguna.

  Msekwa aliyetumia muda mwingi kuzungumzia historia yake ya uongozi ndani ya chama kuanzia TANU hadi CCM aliwataka wajumbe kutoangalia uswahiba wala ushawishi wa aina yoyote katika maamuzi yao bali wahakikishe wanayemchagua anastahili kupeperusha bendera ya chama hicho tawala na kukiletea ushindi.

  [​IMG]
  Siyoi Sumari akiwa amebebwa na wafuasi wa CCM baada ya kuibuka mshindi wa kura za maoni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama hicho, jana. Picha na Filbert Rweyemamu

  Katika uchaguzi wa awali wa kura za maoni uliofanyika Februari 20, mwaka huu, Siyoi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jeremia Sumari aliyefariki hivi karibuni aliongoza kwa kupata kura 361 akifuatiwa na Sarakikya alijinyakulia kura 259.

  Wagombea wengine na kura walizopata katika uchaguzi wa awali kwenye mabano ni pamoja na Elirehema Kaaya (205), Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (176), Antony Msami (22) na Elishiankira Urio aliyeambulia kura 11.

  Msami tayari amehamia Chadema alikochukua fomu kuomba uteuzi wa kupeperusha bendera ya chama hicho na kuambulia kura 8 katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama hicho zilizopigwa juzi eneo la Maji ya Chai wilayani Arumeru.

  Kamatakamata ya Takukuru

  Katika hatua nyingine, kitendo cha kuwakamata baadhi ya viongozi na makada wa chama hicho juzi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa lengo la kumsaidia mmoja wa wagombea jana kilibadilisha upepo miongoni mwa wapiga kura ambao wengi walidai kitendo hicho kililenga kumnufaisha mmoja wa wagombea na hivyo kuazimia kuonyesha hasira yao kwenye sanduku la kura.

  Miongoni mwa viongozi na makada wa CCM aliyekamatwa kwa kudaiwa kujihusisha isivyo halali katika kampeni za Siyoi ni pamoja na Diwani wa Kata ya Mbuguni, Thomas Mollel maarufu kwa jina la ‘Askofu' aliyesema baada ya kutiwa mbaroni kwa maagizo ya watu aliowaita wakubwa, alihojiwa kwanini anamfanyia kampeni mgombea huyo na aliyemtuma kufanya hivyo.

  Ingawa kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Mbengwa Kasomambuto alikataa kuwataja viongozi wengine walioshikiliwa juzi kwa mahojiano, waandishi wetu waliofika ofisi za taasisi hiyo walimshuhudia mmoja wa waliogombea katika awamu ya kwanza ya kura za maoni pamoja katibu wa UVCCM katika moja za Wilaya za Mkoa wa Arusha wakihojiwa na maafisa wa idara hiyo ya dola.

  Katika orodha hiyo pia walikuwapo madiwani wawili wa Kata za Arumeru na jana eneo lote la mkutano ulijaa maafisa wa Takukuru, na askari kanzu waliokuwa wakiranda kila kona na kujisogeza kwenye kila kundi la watu zaidi ya wawili walioonekana kuzungumza kwa lengo la kunasa mazungumzo yao.

  Maofisa wa Takukuru jana waliendela na kamatakamata hadi muda mfupi kabla ya matokeo ambapo mmoja wa kada maarufu wa vijana wa CCM wilayani Arumeru, Ally Majeshi alitiwa mbaroni kwa mahojiano baada ya kudaiwa kutajwa na baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa juzi.

  Shamrashamra
  Baada ya matokeo, Siyoi alitoka ukumbini akiwa amebebwa juu juu na wafuasi wake kwa umbali wa zaidi ya kilomita mbili huku watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Sarakikya wakiwa wamebaki eneo la ukumbi wa mkutano katika makundi wakijadiliana.

  Akizungumzia matokeo hayo, Sarakikya alikubali kushindwa na kumpongeza mgombea mwenzake akimtakia kila la kheri katika uchaguzi ujao wakati mshindi akiwashukuru wajumbe kwa imani waliyoonyesha kwake akiwataka kuanza kampeni za kutafuta ushindi wa CCM.


  CHANZO: Gazeti la Mwananchi
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeisoma hii thread yako, nilikuwa natafuta "your take" lol.........
  Naamini umeiweka huku tabasamu limekujaa sana mtu mzima....
  Say something Mzazi!
   
 3. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Panzi wanaandaa ugomvi, kunguru kaa sawa.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  My take: Mwisho wa ubaya ni aibu, na hawa mavuvuzela akina Nape sasa ni lazima wakubali kwamba Lowasa ni heavy weight kwao.
  Nape anayejifanyaga yuko up to date facebook mpaka dakika hii ameisusa facebook account yake na ameshindwa kuwapa matokeo haya mafans wake wa facebook.
   
 5. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ccm ina safari ndefu kuelekea demokrasia ya kweli
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Matola......Lowassa angekuwa Heavyweight Sioi asingepata kura 300 kati ya 1,000 kwenye uchaguzi wa kwanza kabla ya ule wa marudio......

  Kuna tatizo kubwa sana ndani ya CCM Arusha na Arumeru.....Tatizo ambalo linaweza kupelekea CCM kushindwa uchaguzi wa Arumeru....Sidhani kama kutumia mapesa mengi kuwahonga watu wakuchague ni kigezo cha kuwa Heaveweight....

  Heavyweight ni kama Nasari ambaye ameshinda kwa kishindo uteuzi ndani ya CHADEMA kwa kupata kura 808 ya kura kati ya kura 888 zilizopigwa.....Huyu ndiyo Heavyweight maana ameonekana ana nguvu sana kwa kukubalika kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura zilizopigwa na kapata kihalali bila hata kutoa Rushwa.....

  Sidhani kama mwandishi makini wa Habari angeweza kuandika Habari kama hiyo eti 'lowassa aisambaratisha CC ya CCM'......Kiukweli CCM wana hali mbaya sana Arumeru.....Mgawanyiko wa CCM Mkoa wa Arusha ni hatari sana kwa hatma ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki...

  NB..
  Kumbuka kwamba mgombea wa CCM atatangazwa na CC tarehe 3,March......Lolote laweza kutokea....Vipi CC ikiamua kumpiga chini SIOI kwa tuhuma za rushwa ambapo watu wake wa karibu(katika kambi yake) wamekamatwa na TAKUKURU wakigawawa fedha kwa wajumbe......Ni mapema sana kusema Lowassa ameisambaratisha CC ya CCM.......Lolte laweza kutokea...
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Come what may Mr Bala, kwanza kabisa mimi ningependa kuweka wazi naissuport CHADEMA ibebe lile jimbo, lakini kiini cha furaha yangu ni huu unafki wa CCM, wa kutumia muda mwingi kushindana na Lowasa halafu majaribio yao yote wanaangukia puwa.

  Kama swala hawakutaka pandikizi la Lowasa walikuwa na option ya kukata jina la huyu kijana katika hatuwa za awali kabisa, lakini kwa sasa hakuna lingine linaloweza kutokea zaidi ya Sioyi Sumari ndio mgombea Wa CCM Arumeru. otherwise labda tuambiwe CCM imejitoa kwenye uchaguzi.

  Jaribio lolote litaloletwa na kamati kuu kumuenguwa huyu Sumari kwenye Kinyanganyiro ni kusubili kura za chuki kutoka kwa wana Arumeru, CCM haitoamini kitakachotokea mark word. inshort CCM imekaliwa kooni kwa kila hali yaani ipo kwenye situation ya kucheka na kulia zote kelele.
   
 8. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JF nakupenda kwa moyo wote.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  watu wa Arumeru tupeni sasa mtazamo wenu baada ya matokeo haya mnadhani sasa njia nyeupe kwa CDM au hali itakuwa ngumu kushinda
   
 10. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Alafu tetesi zinasema lowassa mwenyewe yko nje ya nchii anaangaliakwa kutumia darubini na satelite.ametumaa vifaa vifanye kazi.ni kiboko duh
   
 11. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kampigia debe mkwewe....
   
 12. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamaa anashangilia kama vile hajatoka kufiwa juzi, siasa hizi!
   
 13. T

  Taso JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Really? Ni makundi tu, yani mapenzi tu ya watu kwa mtu bila sababu ingine yeyote?

  Hakuna tofauti ya itikadi labda kati ya Siyoi na Sarakikya au profile zao, wanavutia watu kwa sababu ya background gani, Sarakikya ni nani na Siyoi ni nani politically, professionally, experientially, hakuna? Kila mmoja ana represent ideals gani? Wanaowasapoti wana wanavutwa na nini, yani wanapenda sura ya mtu na sauti yake tu? Haiwezekani man, makundi tu? Really?

  Basi siasa zetu zina vina na upeo mfupi kupita maelezo. Au labda ni waandishi wa habari ndio hawatafiti hivi vitu, manake nikisoma hizi taarifa za chambuzi za kisiasa natoka mtupu, natoka kama nilivyokuja, zaidi ya kujua Sumari ni mtoto wa marehemu Mbunge, Sarakikya ni mtoto wa Mkuu wa majeshi mstaafu, basi. Kwa kweli inapokuja kwenye uchambuzi wa sifa za nani tunataka atuongoze Watanzania vichwa vyetu ndani vimejaa chawa.
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 652
  Trophy Points: 280
  Umejuaje? hapo kwenye nyekundu.
   
 15. T

  Taso JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Nimejuaje? Soma hapa.

  Watoto wa vigogo wajitosa uchaguzi Arumeru

  MWANANCHI
  Tuesday, 14 February 2012 10:45

  Waandishi Wetu

  MTOTO wa Mkuu wa Majeshi mstaafu, William Sarakikya na mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  chiligati should go?
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Heavy weight huko huko Arusha vitongojini kwake,arusha mjini penyewe maji mazito kwake,hiyo ndiyo faraja pekee aliyonayo huyo mwanaume wenu wa shoka......na bado mpaka tumfanyie kile anc walichomfanyia malema..
   
 18. H

  Honey K JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi Nape anaingiaje hapa? Nimesoma stori yote uloweka hapo hakuna mahali kuhusika kwa Nape kwenye uchaguzi wa Arumeru lakini kichwani mwako kwakuwa Nape ni mwiba kwa ufisadi basi usipomtaja hupumui!
  Nafurahia jinsi mafisadi mnavyoteswa na jina Nape!thank you God kwa kuniwezesha kufanya yote niliyofanya kuwatetea Wanzania!
   
 19. H

  Honey K JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hoja ya kutoa matokeo ya kura za maoni Facebook nayo ni mufilisi, lini nimewahi kutoa matokeo hayo kwa chaguzi zote za kura za maoni ndani ya Chama changu? Hakika nawasumbua vichwa vyenu mafisadi na hii ni faraja kubwa kwangu!!!
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na jaribio la kumng'oa kamati kuu nalo lilishindwa?acha kuleta ukinega wako ndani ya chama chetu wewe,kumbe mtu mwenyewe ni mwanachama wa vinega unasumbua akili zetu bure tu hapa,wewe ongelea mambo ya slaa na mbowe na mgombea wa chama chenu hicho cha vinega,mgombea wa ccm kwanza anakuhusu nini wakati wewe ni kinega
   
Loading...