Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli

Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli

Wacha tufeli mitihani kama huu ndio uwezo wetu wa kuchambua mambo
 
Sasa Lowassa anamhoji vipi Rais asiyemtambua, au na yeye anafanya siasa za kilaghai kama Mbowe!?
 
taratibu tu mpaka nae ataomba appoitment ya kwenda kunywa juice ikulu na na rais magufuli.
 
Teh teh kumbe CHADEMA via Lowassa mmeshakubali kuwa JPM ndo rais., safi sana hii
 
He ja yake ya elimu bure mpaka chuo kikuu ilikataliwa na wapiga kura. Kwani bado tu hajarudi Monduli kuchunga ng'ombe!!?
 
Sikiliza wewe dogo mleta uzi, siku zote mwanasiasa umuamini kwa mambo mawili tu;
1> salamu
2 > majina yake
Zaidi ya hapo shika jembe ukalime.
ndugu upo sahihi,mi nangoja mahakama ya mafisadi tu.ili awafunge wezi wa rasilimali zetu.
 
Mbona wewe unaonyesha ni mpumbavu tu hata hujilewi. Umeshasema ni raisi wa ccm. Halafu bado unazidi kuonyesha ujuha wako.

Unakidhalilisha chama chetu kwa kujifanya unahekima kumbe sifuri. Wana Ccm wa kweli tunaamini katika kukosoana bila kukosana, kupingana bila kupigana mwa misingi ya umoja na uhuru. Unataka wapinzani wasitoe mawazo yao, wakasikilizwa, unataka kuniambia hao wapoinzani ni wananchi wa nchi gani? Hivi unajua ccm tumebakia wangapi na kama tukiwabagua hawa wapinzani kwamba hatutaweza kuhimili vishindo vyao?

Hicho kiburi chako na ujuha unaopandikiza hapa, utakuja kuelewa athari zake pale wapiga kura watakapoanza kuwasilisha maumivu yao ya kuharibiwa kwa uchaguzi na kubandikwa raisi asiychaguliwa kwa nguvu ya tume ya lubuva na Makamba January.

Usidhani Ccm tunanguvu ya kuwashinda Watanzania wakiamua hata kama tutandelea kutumia vitisho na mizinga.

Mwenye nchi siyo ccm. Tanzania ni ya Watanzania na kila Mtanzania anayohaki ya kutoa mawazo yake, na kuthaminiwa kwa faida ya wote. Haya wanayoyasema Wapinzani ni kwa faida ya taifa zima. Cheo ni Dhamana, nitatumia elimu yang ukwa faida ya wote.

Hiyo tabia ya ubinafsi na ugandamizaji wa fikra unautoa kwenye ilani gani ya ccm wwe? Kama kuulizwa maswali ni kudharuliwa, ulipaswa kumshauri raisi wetu atangaze kuanzia sasa Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya ki dictator. Ficha upumbavu wako.



KIKATIBA KILA MWANANCHI ANA HAKI YA KUTOA NA KUSHAURI MAWAZO YAKE! LAKINI HANA HAKI WALA SIFA YA KUMUHOJI RAISI.
tofautisha ivo vitu viwili we Nyumbu.
 
Qeen

Wasikusumbue hao n ajenda yao ya siri ndio maana wanazomewa siku hizi wao na bosi kutikana na ufurukutwa wao na kuacha maadili ya uandishi wa habari

Dah!!!! Usiniambie magazeti yenye weledi ni Uhuru,Mzalendo,Daily News na Sunday News......!!!! Tatizo lenu CCM mnataka watanzania wote wawe na mawazo kama ya kwenu!!!! Tushangilie TBC,Star tv, Uhuru na watoto wao....No thank you sie tunasimamia usawa na tunasema Hongera gazeti la Nipashe kwa kutupa habari za upande wa pili.
 
Kwa nini asijihoji ye mwenyewe hadi sasa hayupo ikulu wakat alisema tar 25 asbh atakuwa pale
 
Ametaka kujua kama hata walioko mashule hawatalipa ada au ni wale wanaoanza shule pekeee? Mbona ni swali la msingi sana
 
Serikali ina siku tatu tu.. tumpe muda.. kama angetaka kumhoji angepimana naye kwemye mdahalo...hata hivyo inabidi ashushe gear ya kampeni ya matumaini na sasa ni kipindi cha kuwalettea wananchi maendeleo ya kweli!
 
mtoa post wadhani utapewa ubunge,tuliza mshono fanya yako siasa waache wenyewe
 
Namshkuri Mungu kwa Lowassa kuwa mtulivu,na kukubali JPM ndie Raisi wake.Kwa hili tu la kumuuliza maswali juu ya elimu ya bure inapaswa kuanzia wapi unaona kabisa Mungu ametenda....Lowassa we hatuachi,kukupenda hatuachi,Lowassa we hatuachi..nakumbuka kale kawimbo ka kampeni
 
Nimenukuu heading na content kama ilivyo kwenye gazeti. Kwa hali hiyo huyu mwandishi ndio atakuwa kala hayo maharagwe.

Queen Esther
Title yako inakosa hayo maswali.....au nakuwekea hapa chini ili atakayefungua ayaone

-Elimu ya bure itatolewa kwa kiwango gani?
-Atashughulikia vipi suala la wanafunzi waliokosa mikopo? na
-Kueleza wazi hatma ya wanafunzi walioko mashueni kwa sasa kuhusu kusoma bure.
 
Swali la msingi katika hoja hiyo ni juu ya wanafunzi waliopo shuleni yaani wale wa kidato cha pili na nne kwani Magufuli katika maelekezo yake alisema wale wanafunzi watakao anza January wasome bure hapo ndio kwenye tatizo.
 
- Dr. JPM Kama Rais anaendelea kutengeneza sera za utekelezaji wa ilani Yake SAWASAWA na ahadi alizotoa kwa watanzania wakati wa kampeni.

- Ahadi ya kutoa elimu kwa Dr. JPM haikufanana na ya Lowassa hivyo ni makosa kwa Lowassa kusema mimi nilitaka au niliahidi iwe hivi na vile. Huu sio wakati wa kampeni. Lowassa anajua yeye ni tajiri hivyo hata kupitia miradi aliyonayo anayolipwa yeye na marafiki zake kila mwezi angeweza kutoa hiyo hela bila kuitegemea Serikali.

- Tunashukuru Kama ulivyoandika inaashiria Mhe. Lowassa amemkubali Dr. JPM kuwa Rais. Tu naomba ukiongea nae mwambie asubiri siku 100 ziishe.

- Anakaribishwa Ikulu pia Kama ana mchango wa kusaidia Taifa haili. Kutokana na uungwana wake ambao ninaujua afanye appointment.

Tuweke Tanzania kwanza na sio kuibuka na hoja za kupunguza kasi ya wengine au ku divert attention.

Queen Esther

MAGUFULI NI RAISI WA JMT HIVYO SIO RAISI WA CCM ANA HAKI YA KUKUSANYA ILANI KUTOKA CHAMA CHOCHOTE NA KUANGALIA YALE MAZURI ZAIDI NA KUWATENDEA WATANZANIA. WEWE ULIYEPOST UACHAMA HAPA JITAMBUE NYINYI NDO MNAOPANDIKIZA CHUKI KWA WANANCHI WASIIPENDE SELIKALI NA KULETA MAKUNDI YENYE MSIMAMO TOFAUTI. HIVYO BASI KITENDO CHA MAGUFULI KUPEWA SERA KUTOKA VYAMA VINGINE KUSAIDIA WANANCHI SIO KOSA NA AKIFANYA HIVYO WANANCHI ATAFANIKIWA KUWAUNGANISHA NA KUONA KWAMBA KILE KILICHOKUWA KINATAFUTWA NJE YA SERIKALI KINAWEZA KUPATIKANA NDANI YA SERIKALI MPYA YA CHAMA KILE KILE KUPITIA MAGUFULI. ACHA UJINGA LENGO LA WATANZANIA NI MAENDELEO KWENYE SEKTA ZOTE NA SIO KUIPATA "CHADEM WALA CCM" NDO MAANA WALIKUWA WANAJARIBU KUFUMUA MFUMO WA CCM KWENDA CHADEMA ZOEZI AMBALO LIMETIKISA SERIKALI NA KUJITATHIMINI NA KUONA NI KWELI WANA MAKOSA KIUNDENDAJI NA WAKAOMBA MAGUFULI AOKOE JAHAZI KWA KUWATULIZA KIU YA WATANZANIA YA KUPATA KIONGOZI ANAYEJITUMA KWA NGUVU ZOTE. SIO VIZURI SASA HIVI KUISHI KWA KUZOMEANA TUACHE SIASA TUOMBANE MSAMAHA TUCHAPE KAZI HUKU TUKIWAHIMIZA WABUNGE KUIBANA SERIKALI KUTEKELEZA MEMA KWA WANANCHI. "HAPA KAZI TU" PIA NA WANAFUNZI "HAPA SHULE TU"

  • :lock1:
 
Your Majesty the Queen, Umenena neno ambalo mja tu ataweza kuongezea maana kuna wengine wanadhani wao ni mahodari wa kunena
 
Anachokoza moto wa watanzania au ulioko kifuani pako????
Dr. JPM ni Rais wa awamu ya tano. Acha haya makitu unayoshabikia ndg yangu. Hata Kama humpendi uchaguzi ndio umeshaisha na maisha yanaendelea.
Hapa kazi Tu

Queen Esther

Angeshindwa angerudi tu Monduli. Sasa Lowasa hajashindwa kwenye uchaguzi. Ila tume imeamua kumtangaza wanayemtaka wao bila kujali matakwa ya Watanzania.

Naomba usibishe kishabiki.

Toa maelezo ya msingi kwa nini polisi walivamia na kuharibu mifumo ya kukusanyia matokeo ya UKAWA na kuwaacha Ccmwakiendelea kujumulisha.

Toa sababu za polisi kuvamia kituo cha sheria na haki za binadamu na kuwazuia kujumulisha matokeo yaliyokuwa yameshatangazwa na tume vituoni.

Ccm tutajiokoa na dhambi ya wiizi wa uraisi (siyo wa kura kwa kuwa polisi walilinda vituo vizuri vya kupigia kura vizuri), kama tutatoa majibu y akwanini Lowasa alipopeleka petition kwenye Tume ya Lubuva hakusikilizwa wakti ni suala ambalo liko kwa mujibu wa sheria.

Kinyume cha hapo, acha kabisa kuchokoza moto ulio kwenye mioyo ya Watanzania maana matusi yako na propaganda hazitauzima utakapolipuka.

Ni afadhli kukaa kimya kuliko kutafuta hasira za Watanzania. Jitambue.
 
Back
Top Bottom