Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,206
- 1,465
Habari za asubuhi GT's
Leo katika kupitia magazeti asubuhi hii nimekutana na kichwa cha habari kikubwa chenye picha ya Rais wetu JPM na picha yenye ukubwa Kama hiyo ya Lowassa wakiwa wametazamana. Rais wetu JPM akiwa anatabasamu na Lowassa akiwa Kama mtu anayefoka.
Picha hizo na hicho kichwa cha habari zimechukua asilimia 90 ya ukurasa wa kwanza wa gazeti. Gazeti hili ni la Nipashe la Leo Tarehe 9/11/2015 (ISSN 0856.No 0578662).
Baada ya kutoa Utangulizi naomba kutoa hoja:-
1. Gazeti la Nipashe limeshindwa kuweka picha sahihi kwa heshima ya Rais wa awamu ya 5 na hilo ni kutokumtendea haki. Huwezi kuweka picha za ukubwa SAWASAWA na zaidi huyu Lowassa anaonekana Kama anatoa maneno makali kwa Rais wetu Dr. JPM
2. Gazeti la Nipashe linatakiwa kufahamu kipindi cha kampeni kimekwisha na Rais amepata kana. Huwezi kutoa umuhimu sawa kwa vitu visivyolingana.
3. Taarifa hii imepewa uzito mkubwa na ina Lengo fulani nyuma Yake ambayo wenye Hekima wamenielewa.
4. Sasa na kuja kwenye ujumbe wenyewe (contents)
- Naomba Mhe. Lowassa na watu wake wafahamu kuwa Rais wa awamu ya tano Dr. JPM anatimiza ilani ya CCM.
- Ni makosa ya kiufundi na ya kitaalamu kwa wasaidizi wa Lowassa kumshauri aje kwenye vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia Rais wake ambaye mpaka sasa CHADEMA hawajamtambua.
- Namna Yake (Lowassa) ya kutoa elimu bure aendelee kuiweka na siku akiwa Rais aitumie, kwanza ni vizuri CCM hawaku copy maana ingekuwa nongwa.
- Serikali ya CCM imeanza kutekeleza Yale iliyosema kwenye kampeni kupitia ilani ambayo kwa upande wa Chadema hatukuona mgombea hata mmoja wa Chadema akikabidhiwa. Sasa kiherehere cha nini?
- Nashauri WAPAMBE wa Lowassa muachane na kukosoa ilani ya CCM kwani muda wa kampeni UMEISHA na sasa ni muda wa utekelezaji. "#HAPA KAZI TU#
- Nashauri Mhe. Lowassa uwe mvumilivu na uiache awamu ya 5 itekeleze majukumu yake. Mambo ya kutafuta waandishi wa habari ili uwe unafuta nyayo za Rais ni sehemu ya uhaini. Pia unasahau kuwa "Mamlaka na iheshimiwe na watu wote".
- Chochote unachokosoa kuanzia sasa kuhusu serikali ya awamu ya 5 uwe na reference ambayo ni Ilani ya CCM na sio maneno yako wakati upo kwenye majukwaa ya siasa. CCM haitekelezi maneno yako au matakwa yako.
- Kama kweli wewe ni mzalendo na unataka tujenge Tanzania yetu na unaona kuna hoja ya msingi; omba appointment kamuone Mhe. Rais.
- Achana kabisa na mambo ya kutafuta umaarufu kwenye magazeti na vyombo vya habari kujaribu ku water down juhudi za mheshimiwa Rais. Watanzania hatutaki malumbano sasa tunataka kuona kazi. (#Hapa ni Kazi Tu#)
Naomba kuwasilisha.
Queen Esther
============================================
Chanzo: Nipashe

Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.
"Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi," alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
"Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao," alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.
Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
Chanzo: Nipashe