Hivi watanzania sisi mazuzu nini? Hivi akili zetu ziko sawa kweli? Napata wasiwasi, acha niseme, mwenye kupinga alete hoja sio kubwabwaja tu.
Kwa akili ya kawaida tu tena isiyohitaji darasa, kiongozi anayetumia pesa au utajiri wake kupata uongozi anafaa kwa nchi kama hii? Kutumia pesa huenda isiwe tatizo, swali ni je, kama kiongozi, pesa yote hiyo anayotapanya kaipata wapi?? Hivi hatuwezi hata kufikiri kuwa ni kodi zetu hizi hizi zinazokatwa kwenye mishahara yetu au katika bidhaa tunazouza na kununua?? Unashabikia nini kama sio ujinga uliokithiri? Na kwa akili ndogo tu unadhani mtu huyu ana upendo saaana na watu hata atapanye pesa bila hesabu? Ujue kila shilingi anayotoa akipata nafasi anayotafuta atairejesha mahali pake na riba juu! Cha ajabu mtu anashabikia ujinga hapa bila kujua gharama za maisha source ni nini kwa huduma za msingi kama umeme kuwa ghali sana, mnadhani yeye anakisima cha pesa, ni hizo hizo kodi za masikini maana matajiri kodi hawalipi, wanalipa rushwa yenye discount. Nani aijenge nchi kama mawazo yetu ni mgando kiasi hiki pamoja na kwenda shule?
Hivi kwa akili ya kawaida tu, mwalimu JK aliposema umasikini wa mawazo ndo mbaya kuliko wote alimaanisha nini? Simple, alimaanisha katika hiki ambacho huyu mtu mnayemshabikia anacapitalise on, yaani fikra mgando.
Oh ni jasiri na anauthubutu, thibitisha. Acha kushabikia bila kutafakari, nchi hii ni tajiri lakini watu wake walio wengi ni masikini, hivyo usitegemee bepari akamkumbuka masikini.
Mwalim aliuliza Ikulu kuna biashara gani? Sasa ole wa TZ huyu mtu akipata nafasi hiyo, nawahakikishieni pesa zooote alizomwaga kwa viongozi uchwara wa dini wasiomjua Mungu na kwa watu au makundi ya watu tutazilipa mara 100 zaidi, hakuna tajiri anayetupa pesa, hayupo.
Kwa ujumla nchi hii bado haijapata mzalendo wa aina ya kizazi cha akina nyerere, sokoine, kawawa, n.k. ila tusubiri wakati utaamua, ila ushabiki wa kijinga kumsufia mtu anayejulikana public kuwa hafai, ambaye hata boss wake alimkataa waziwazi (mwalim JK), ni mawazo mgando yasiyo na tija kwa taifa letu.