Lowassa aenda kuhiji, kujitakasa na kujisafisha Israel

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
162
Heshima Mbele,
Habari ambazo zilinifikia jana usiku ni kwamba,aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Lowassa(MB) ameelekea Israel na bethelehem kwenda kuhiji na kujisafisha ili aje aanze upya na mambo yake.Hii ni moja ya Mbinu aliyoibuni ili kuhakikisha anaedelea kuwa juu,wapambe wake wana mipango mingi ya kuhakikisha anabaki juu.

Habari ndio hiyo,Huu utakuwa ushuri wa Askofu Laizer,yule Mpambe na Mshabiki mkuu wa EL
 
Heshima mbele wakubwa!

Hija bila toba inawezekana? Naomba watalaamu wa mambo haya wayaweke wazi.

Kwa maoni yangu alipaswa kwanza kujisafisha kwa watanzania kwa kukiri makosa aliyowafanyia na kuomba asamehewe.

Kama aliiba mali ya umma airudishe pamoja na riba ili kuliinua taifa kiuchumi.

Hatua ya mwisho ndio angeenda huko kwa Wayahudi kuhiji
 
Nani kamwambia kutubu dhambi kuna uhusiano na kwenda Israel?

Sala ya Toba inasemwa popote pale.

Mungu siku zote anaabudiwa katika roho na kweli si kwa kwenda mahali fulani.
 
Isije ikawa ndio amehama TZ,au amekwenda kufichwa huko ili akihitajika na vyombo vya sheria waibue hoja ya kwamba hapatikani.
 
Kabla ya hija ni lazima ujitakase kwanza ambako kunaambatana na toba.
Toba ya huyu mwenzetu ni lazima ihusishwe na urejeshaji wa fedha za umma as manunguniko ya walalahoi wa Tz tayari yako mbele ya Mungu.Kuna zaburi yasema sala ya mwenye dhambi mbele ya mungu ni sawa na kelele.

Toba ya kweli ni pamoja na kurejesha fedha za walala hoi
 
Hivi mpaka Leo bado mnamtuhumu E.L.mwenye ushahidi aende mahakamani.
 
Back
Top Bottom