Chonde chonde raisi wetu Magufuli asikufundishe yeyote iwe toka kwa viongozi waliokutangulia wala wapambe wao namna ya kuongoza nchi wala chama.Sikatai kupokea ushauri wao na si lazima uutekeleze kwani kwa miaka yao ufisadi na wizi wa rasilimali za watanzania zilitamalaki.Amani wanayoweza kujivunia tunayo tu na watanzania kwa ujumla hawakulelewa na Nyerere katika vurugu.Ukishapokea kofia ya m/kiti chama taifa ni kuwa umekamilika kuongoza nchi na chama na tenda kadri yote kwa manufaa ya wananchi unaowaongoza na ndivyo ulivyokuwa unawaahidi katika mikutano yako ya kampeni na wananchi wakakupa ridhaa kwa imani hiyo.Nakuhakikishia hadi sasa una asili mia 85 ya imani ya watanzania kwa uongozi wako wa miezi sita tu.Wasikudanganye kuwa asilimia hizo ni za wanaccm wenzako tu na wapinzani wapo.Ushari wa kuwa tunakubali utumbuaji majipu anaoufanya raisi ila akisha pewa kofia ya chama taifa apunguze ukali ili wanachama wabaki ndani ya chama hauna manufaa kwako na watanzania huo pengine ni upotoshaji.Mtamshaurije awe mpole wakati hata yeye mwenyewe anajua fika waovu na mafisadi ndiko walikojificha?Hivi hadi leo hamjiulizi sababu za kuepuka sana kujinadi kwa kutumia chama kwenye kampeni zake?Namshauri raisi aanzie huko huko kwenye chama chake mafisadi na wasiotenda kuenenda na taratibu za chama sio tu kuwatimua na kuanza nao kwenye mahakama ya mafisadi mwezi July bali awanyanganye na kadi za chama.Chama kisicho safi kitaongozaje serikali?Pia mapema tu kabla moto haujapoa alirudishe na azimio la Arusha na kuachana na la Zanzibar walikokwenda kuhalalisha ulaji wa wakubwa na viongozi serikalini kumiliki mabiashara makubwa kuanzia maduka,mahoteli,meli kubwa kubwa hadi migodi.Pili atoe agizo bunge la katiba kuheshimu mawazo na matakwa ya wananchi na kuipitisha rasimu ya judge Warioba na kuachana na matakwa ya wabunge wachache wa ccm na wateule wachache kwa manufaa yao na chama chao.Ukishatekeleza hayo ndio mwisho wa wewe na viongozi kuhangaika na utumbuaji maana yatakuwa yamejitumbua yenyewe kwenye azimio na katiba.Nakuhakikishia mwaka 2020 kampeni zako zitakuwa kidogo sana na utaongoza kwa raha.Hayo ndiyo wanayoyataka wananchi na mwenyezi Mungu kwa waja wake.[/QUOTE MAGUFULI:- " Mimi sipendi Mavyama vyama haya"