Lowassa achomoza Kamati Kuu ya CCM Dodoma

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma.

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Sasa Mzee Tupatupa hiyo ya kumjadili Lowassa ilikuwa ajenda yenu pia?Kuna ile kauli ya wale wapendao kuzungumzia watu na si Mambo yenye faida wanaitwaje vile....................Mwambie JK ameshatoka CCM asiendelee kumzungumzia Lowassa...............
 
Kwa hiyo bado wapo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wanaotoa siri za vikao vyao?
 
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Mzee Tupatupa maskini toka Lowasa wako abwagwe akili yako imevurugika huishi kutunga vitu vya kuota.Utakuwa kichaa usipoangalia.Kichaa huanza hivi mfano unaenda Dodoma unamwambia mtu naenda morogoro.Sasa wewe UKo CHADEMA lakini kutwa unajifanya kuongelea ya CCM ukijifanya mwana CCM wakati ni CHADEMA. Una CONFLICT OF PERSONALITY WITHIN YOURSELF!!! hizo ni dalili za kwanza za ugonjwa wa kichaa.

Jamii forums mwenye namba ya hospitali ya mirembe ampe Mzee tupatupa yaweza msaidia kichaa kikipanda awapigie
 
Mzee tupa tupa unaweza kuambulia matusi kwenye huu Uzi....ngoja wale kindakinda waje uwasikie....kuna watu huku JF huwa wanajifanya wanaijua ccm kuliko wenye ccm wanavoijua...ila atakayepingana na kauli ya JK na wajunbe wa KK atakuwa anapingana na ukweli...
 
Sasa Mzee Tupatupa hiyo ya kumjadili Lowassa ilikuwa ajenda yenu pia?Kuna ile kauli ya wale wapendao kuzungumzia watu na si Mambo yenye faida wanaitwaje vile....................Mwambie JK ameshatoka CCM asiendelee kumzungumzia Lowassa...............
Hawawezi kumaliza vikao bila kumtaja lowassa mkuu.nguvu ya lowassa ni kubwa ndani na nje ya chama.
 
Kwani Obama ni mwenyekiti wa Democratic? Sasa kama Magufuli mnataka kumpa uenyekiti chama kitaisimamia vipi serikali? Upuuzi huu upo Tanzania peke yake.

Hivi huyu Uhuru Kenyatta naye ni mwenyekiti kwenye chama kilichompa ugombea urais?
Mkuu,lisilowezekana duniani hapa tanzania linawezekana.yaani ni mambo ya ajabu sana sasa ikitokea rais ndo mwenyekiti wa chama unatarajia nani atampinga hata kama akikosea?
 
Hawawezi kumaliza vikao bila kumtaja lowassa mkuu.nguvu ya lowassa ni kubwa ndani na nje ya chama.

Kwa hiyo lile Zimwi aliloliweka kwenye Chupa linamuwinda mwenyewe???Nafikiria tu kwa sauti................Hakika aliyesema Chuki inakumaliza mwenyewe hajakosea,Mzee naona anajimaliza mwenyewe...............
 
Back
Top Bottom