Sehemu ya 8.
Nilivyo fika nikaenda kwa jim nikamuuliza kuhusu ugonjwa ameupataje ? majibu haya kunirizisha mwisho wa siku ikabidi tuende hospital tukapa tiba wote wawili japo sikua na hakika Kama naumwa na kule dom jamaa alikua fresh hakuumwa kwa hiyo jim alijua mwenyewe alipo pata ugonjwa huo.. Kuanzia hapo nikawa nimepata uoga pia kuhusu yeye! Sasa siku moja ni kamuuliza jim ikitokea nimepata mimba itakuaje ?
Akanijibu ntakuacha 😳 Oh! Okay nikaa kimya kidogo
Akasema kwani mm sio mwanaume? Naweza kukupa mimba pia kwa nn sio mm awe mwingine? mm mwenyewe sina mtoto..
Nikawaza nawaza maisha yake,maisha yangu mmh! Kila nikiwaza jibu linakuja no! Hapana na sababu za kupata jibu hilo ni kwamba kijana alikua Hana kazi na sioni Kama mchapa Kazi na sioni Kama ana ndoto yaani kiufupi nikawa sioni Kama alikua ni mwenye muelekeo yaani yuko yuko tu simuelewi nikawa najifikiri tuta mleaje huyo mtoto na mm nilikua na ndoto za maisha ninayo taka kumpa mwanangu basi kila nikifika hapo nachoka kabisa nguvu ya kuzaa inaisha! Lkn tofauti na hayo kijana alikua mstaarabu sana , tabia nzuri na ana mapenzi, ana nisikiliza yaani ana sifa nyingi tu na zaidi alikua ana nipa raha kwenu kufanya mapenzi ( ILOVE SEX ) ... Lkn kitu kilicho kua kin niboa ni kwamba hafanyi kazi Sasa mm siwezi kuwa na mwanaume ambae hafanyi kazi Yaani nilikua naweza kutoka kwake asubuhi nikaenda kwenye mishe mishe town Lkn nikirud i na mkuta kalala labda hajaoga toka nilivyo muacha dah! Yaani Kama kuna kitu kina kera kwenye maisha yangu ni mwanaume mvivu na mchafu nachukia sana ! Nikawa namvumilia coz when it comes to sex 👌👌 ... na all that time jamaa wa Dodoma akawa ana nipigia cm wkt mwingine akija dar naenda kumuona sasa nikiwa na huyu tunaongelea mtoto ! Na sifa ninazo taka kwa mtu ninae taka kuzaa nae anazo! Kwanza ana muelekeo wa maisha,ana malengo, umri wake sahihi,ana Kazi nzuri na nikiongea nae naona vitu anavyo penda kuhusu ukuaji wa mtoto na mm napenda kwa hiyo maongezi yetu mengi ya kawa yana lingana! Lkn sasa hakua na time yaani naweza nikamuona miezi kazaa Mara moja yaani juu kwa juu tu na nikimuona leo labda mpaka miezi ipite
so tukawa hatuko karibu labda akiwa dar mm Niko nje ya nchi tukawa tunapishana.
Itaendelea......