Love is a drug abuse

Love is a drug abuse

Nikiona mtu ameanzisha uzi wa simulizi/riwaya naangalia kwanza kama huwa ana historia ya kumalizia story

Huyu kwa historia yake nam rate 0.5/10
Yaani hamnamo mtu

Ni takataka

Ni mtoto

Haeleweki

Anajifurahisha

Sio msimuliaji

Amevamia fani

Hajui

Anakurupuka

Hajifunzi kwa wengine

Anatafuta fame

Anatupotezea muda

Hajui anachofanya
 
Nikiona mtu ameanzisha uzi wa simulizi/riwaya naangalia kwanza kama huwa ana historia ya kumalizia story

Huyu kwa historia yake nam rate 0.5/10
Yaani hamnamo mtu

Ni takataka

Ni mtoto

Haeleweki

Anajifurahisha

Sio msimuliaji

Amevamia fani

Hajui

Anakurupuka

Hajifunzi kwa wengine

Anatafuta fame

Anatupotezea muda

Hajui anachofanya
Powa bhna asnte
 
SEHEMU YA NANE (8).


" Vai jikaze tutoke eneo hili hapa siyo salama". Nikazungumza na kujitahidi kumbeba vizuri huku kichwani mwangu nikiwa nishapata majibu kuwa wale siyo boko haramu wafate nini,kwetu nikambeba na kufungua mlango huku nikiona taa zikizima na kuwaka maana ule mripuko ulipelekea mpaka shoti chuo kizima,nikaanza kutoka naye huku nikiwa makini, nikasika mtu akija au watu wakija kwa mbele baada ya kuona miale ya taa zao zikimurika murika,nikatizama chumba cha dokta na kwa haraka nikafunguna na tukaingia huko ndani, kisha nikampeleka Vai na kumketisha kwenye kiti na nikamwambie hatulie kisha nikawahi pale mlangoni na kujibanza ili atakayefungua awe halali yangu kivyovyote,.
" Najua kuna watu tokeni nje watu wote popote mlipo kabla hatujapiga risasi ovyo". Sauti ikasikika kwa nguvu na kufanya nimuone Vai akitetemeka lipsi za mdomo wake, nikameza fundo la mate na kumtizama kisha taratibu nikafata meza na kuikalisha pale mlangoni,nikaenda dirishani na kufungua kidogo nikakutana na nondo pamoja na kioo kwahiyo hakuna njia ya kupita ni lazima tungekamatika humo, mlango ukasukumwa mara ya kwanza bila kufunguka nikazidi kuchanganyikiwa baada ya kusukumwa mara ya pili na ukafunguka, miale ya taa ikatupiga machoni na kufanya sote tukinge macho yetu kwa viganja vya mikono, kwani zilikuwa tochi kali mno,..
"Hahaha Upo na mpenzi wako kijana ina maana nyie viziwi". Sauti ikasikika na huyo mtu akaanza kusogea taratibu kutufata,nikawa makini kumtizama kama ana silaha na niliona akiwa na bunduki ya kivita mkononi mwake, mkono wake wa kulia ulishika tochi kubwa, huku akiwa na koti kubwa jeusi, muonekano wake ni kama majambazi wa zamani wa filamu za kibongo za seba na J_plus.
" Vai ?". Nikamsikia huyo jamaa akiita jina la vai na kufanya nishtuke nikamtizama vai na kumuona naye akimtizama mtu huyo kwa umakini.
" Kaka". Vai akaita na huyo jamaa kwa haraka akazima taa baada ya kusika sauti za watu wakija kule tulipo.
" W12 UKO WAPI?". sauti ikaita nje ya chumba tulichomo.
" Nakuja boss". Mtu ambaye inaonekana ni kaka vai akazungumza.
" fanya haraka tunahitaji watu wote wakiwa hai na idadi yao iwe sawa".
" Sawa mkuu". Kaka vai ambaye ni W12 akazungumza na taa ya mule ndani ikazima kabisa kukawa giza tena totoro.
" Kaka imekuwaje nini kinaendelea?". Nikawa nasikia sauti zao na jamaa akawasha taa na kuifunika kidogo ikawa inatoa mwanga mdogo kama wa simu ya nokia.
" Story ndefu sana, imekuwaje hupo chuo nilikuacha nyumbani na hakuna kila kitu".
" Tulipata mdhamini ila sikuelewi mpaka sasa ina maana umekuwa mtekaji". Vai akazungumza
" Ina maana ulimuua kweli Fredy". Vai akazungumza na kufanya nishangae na kutaka kujua nini kinaendelea.
" hayo siyo mambo ya kuzungumza hapa, huyu nani yako". Akazungumza na kunimulika na tochi.
" aah hahah mtoto wa raisi". Jamaa akazungumza na kujijibu mwenyewe baada ya kunifahamu,akatingisha kichwa kisha kumtizama dada yake maana yeye alionekana mkubwa kwa vai.
" Nitakufungia humu ila huyu naondoka naye". Akazungumza na kumtizama dada yake ambaye vai anaonekana hakupenda kauli hiyo toka kwa kaka ake.
" Rich haiwezekeni muache kijana wa watu kama kweli me na undugu na wewe". VAI akazungumza kwa msisitizo ila jamaa hakutaka kumsikiliza akaninyooshea bunduki na nikaweka mikono juu kisha akanambia nilale chini na nikatii huku nikimtizama vai ambaye anajitahidi kunyanyuka ila akashindwa, ila taa ya chumba ikawaka na kufanya chumba kiwe na mwanga mkali, nikataka kuinuka kwa haraka ila jamaa alikuwa na kasi ambayo sikutegemea akanipiga teke la mgongo na kufanya nirudi chini kama mzigo.
" Staki nikudhulu". Akazungumza, kisha akachukua gundi kubwa mfukoni mwake na kunifunga nayo kwenye mikono yangu na akanisimamisha,baada ya hapo jamaa nikamuona akipanda juu ya meza na kutoa ile taa, kisha akamfata dada yake ambaye muda wote huo alikuwa akigomba kwa sauti ya chini sana huku akinitetea, na muda huo chumba kilibaki na mwanga wa tochi yake tu, akafungua ile gundi na bila huruma akamfunga dada yake gundi ya mdomoni.
" Samahani dada baki humu kwanza". Akazungumza na bila huruma akashushua kitako cha bunduki kichwani mwa dada yake na akazimia kisha akambeba vizuri na kumalaza chini, na akachukua funguo ya chumba icho ilikuwa mezani na tukatoka naye na akafunga kile chumba kwa nje huku akimuacha dada yake mule ndani..

" Kwanini hauna huruma". Nikazungumza na jamaa akanitizama na kunimulika machoni nikamkazia macho bila uwoga, akaacha kunimulika na kunishika mkono kisha kunitoa nje ya icho chumba na nje ya hospitali..
" Mkuu nimempata". Akazungumza kupitia mic yake ya masikio baada ya kuiwasha maana aliizima alivyoingia mule ndani ya kile chumba tulichokuwemo
"Sawa mkuu". Akajibu na akaacha kuzungumza akawa ana nikokota kutoka humo ndani.
" Vipi kama nikisema umemuacha mtu humu ndani". Nikazungumza na akasita kisha ndiyo kwanza akanitia gundi mdomoni.
" Nitasema ni dada yangu". Akazungumza kwa kujihamini na nikagundua huyu jamaa ni katiri na hateteleki hata kwa maneno.
" Kwanini umuue fredy". Nikaendelea kumtingisha kwa maswali ili kumpima akili yake kama naweza mtongoza kwa maneno maana ndiyo silaha yangu ya kwanza.
" Unajua nini kuhusu Fredy" . Akafoka kwa ukali na kunibana ukutani kwa nguvu.
" nini kinaendelea". Sauti ikasikika na akaniachia.
" Nisamehe mkuu". Akazungumza na kuniachia kisha akampa heshima mtu aliyevaaa mask usoni mwake.

Mtu yule akanitizama na kunirekebisha vizuri shati langu.
" Kupona kwako na hawa watu ni baba yako tu kutoa kiasi cha pesa tunachotaka, hatuhiatji kwenda bank kuiteka maana hatukutaka usumbufu wowote,". Akazungumza na kuniachia.
" Najua hamjafata pesa tu". Nikazungumza na nikaona akisimama maana alikwisha anza kutembea.
" SIASA". nikazungumza na akageuka na tukatizamana.

ITAENDELEAA
( SIJALAZIMISHA MTU KUSOMA MAANA KUNA WATU HUMU WANANITUKANA, WANASEMA SIJUHI KUANDIKA YOYE NI SAWA ILA ME TAENDELEA KUPOST HATA WAKIBAKI WAWILI ndo kwanza bado mchanga kwenye hili group ni vyema mkimpa mtu muda kabla ya kuanza lawama mbona nilikuwaga napost kila sku huwezi elewa mtu anapitia changamoto gani ni vyem zaid kuwa nasubila ili changamot zikiisha mtu hapost kila sku kama kawaida mbona filamu kuna filamu watu wanasubiri mpaka miaka 10, KIUFUPI NITAPOST KAMA KAWA matatizo yangu yakiisha taendelea kama zamani mzigo kila sku kama zamani ni vyema mumpe mtu muda shida yake ikiisha, aendleee kupost kama zamani, nahitaji kuandika kitu kilichobora zaidi mimi ni bainadamu nina shida zangu, hata ungekuwa ni wewe ila zitaishia hivi karibuni na zitafata kwa fujo zaidi....
 
Mkuu humu ndani wajuaji ni wengi mno usiwajali kwasababu humu ndani wote ni wasomi sana,humu ndani watu wote wana magari ya bei mbaya sana na pia humu ndani wote ni wajanja tupu kwahiyo wewe usiwajali
 
SEHEMU YA TISA


Yule mtu mwenye kinyago aliponitizama akampa ishara ndugu yake na vai kuwa anichukue na akafanya ivyo na nikatoka mpaka nje na kukuta kundi la watu la wale manesi na yule daktari aliyenidhulu ubavuni mwangu,tukapelekwa mpaka sehemu waliopo watu wengine ambao wapo chini ya ulinzi nikajaribu kuangaza huku na kule sikufanikiwa kumuona rafiki yangu pamoja na yule binti mgeni nikajua uwenda bado hawajashikwa hata madam aliyekuwa anafanya mapenzi na rafiki yangu naye sikuwaona eneo hilo.
" Mleteni huku". Sauti ikasikika na wakanitengenisha na wale watu wote kisha wakanifungua mikono na kunikabidhi simu mkononi,
"Zungumza na baba yako". Jamaa hao wakazungumza na nikatizama ile simu na kuiweka sikioni.
" Dominck upo salama". Sauti ya baba ikasikika,
" Sipo salama". Nikamjibu na nikamsikia akishusha pumzi ya kuwa na hofu na mimi.
Jamaa alonipa simu akaichukua na kuiweka sikioni mwake.
" Umemsikia fanya tulichokwambia ruhusu mzigo uingie ndani,na pia kiasi cha pesa tunahitaji tulichikubaliana". Jamaa akazungumza kwa msisitizo
" nitawapa hizo pesa lakini huo mzigo wenu siwezi kukubali uingie ndani".
" Una muhitaji mtoto wako na watu wengine wawe hai fanya hivyo mheshimiwa RASI". Akazungumza na sikusikia sauti ya baba kisha jamaa akaendelea
" Hatuna muda wa kupoteza tunaondoka hapa muda so mrefu fanya ivyo sasa hivi".
" Okay". Baba akamjibu
" Iwapo ukileta askari wako au watu wowote kufanya chochote basi kijana wako tutampoteza". Akazungumza kwa msisitizo na kunikazia macho
" Na hayupo peke yake yupo na wanafunzi kibao". Akazungumza
" kwahiyo pesa nawapea wapi?".
" Tulivyokubaliana kumbuka haya yote umeyataka wewe, na sisi ndiyo kila kitu kwako".
" Ayo mambo usizungumzie hapo kwa mwanangu stanley". Baba akasikika.
" hahaha unaogopa asijue siri zako okay tunakuoa dakika 30 tu". Jamaa akazungumza na kukata simu
Kisha akanitizama na kunishika bega
" inaonekana we jasiri sana". Akabinya bega langu na akaondoka na kuniacha na walinzi wake baadhi, akapanda kwenye gari na wakaondoka, wakabaki kama askari wao kumi na nne wakiwa na silaha za moto, na wanafunzi wote tulikuwa katikati kasoro mimi ambaye nilikuwa nao pembeni, ndani ya dakika 30 jamaa wakaanza kuondoka kwa vikundi na mwisho wakatokomea wote na kutuacha sisi pale pale huku wengine wakiwa wanatetemeka, gari za polisi zikaja kwa wingi pamoja na zima moto na kuanza kufanya utaratibu wa kuzima ule moto unaowaka ndani ya lile jengo..
" Kuna mtu kafungiwa ndani ya hospitali". Nikazungumza na muokoaji mmoja huku nikimwambia akamtoe vai na akanitii na akaelekea ndani ya jengo la hospitali na timu yake, wakatuambia tuingie ukumbi wa chuo ili kupata idadi yetu kamili na kuangalia kama kuna mtu aliyeumia aweze kupewa huduma, mpaka sasa sikufanikiwa kumuona rafiki yangu pamoja na yule msichana mgeni, nikaanza kupata wasiwasi na nikakata shauri na kutoroka ukumbini kuelekea kule nyuma ya jengo la hospitali maana nilijua wale ni waoga uwenda wanaogopa kutoka kule nyuma. SIKUONA mtu yeyote zaidi ya mwanga tu wa balbu ukiwaka kwa kufifia, zikikuwa ni taa za dharula kama umeme ukikatika basi zenyewe ndiyo zingewaka, nikajikuta moyo wangu ukinisukuma kumtafuta yule msichana mgeni, sikujua kwanini hali yangu imekuwa hivyo yani hamu ya kutaka kumuona ikaongezeka maradufu huku moyo wangu ukiwa na wasiwasi wa kupindukia, nikasikia kwenye dustbin kukiwa na mchakachomchakacho
Nikanyata taratibu na kulisogelea diaba hilo kubwa lilikuwa limefungwa na mfuniko wake nikafungua na ngumi laini ikatua shavuni mwangu, nikamuona yule binti mgeni akipiga kelele za uwaoga baada ya kunipiga.
" Ni mimi". Nikazungumza na kwa haraka akaniwahi na kunikumbatia kwa nguvu huku akiwa amechafuka sare zake zote, sikuwahi fanyiwa hivyo wala kukumbatiwa na mwanamke mwengine zaidi ya mama yangu, nikahisi mapigo yangu ya moyo yanaenda kasi na kukosa mwingiliano sawa, ghafla rafiki yangu naye akaibuka huku akihema juu juu na nilipomtizma suruali yake ilikuwa imelowa mikojo bila shaka, na alikuwa muoga kupindukia, nikajikuta nikicheka kwa sauti kubwa na kumfanya na yeye aanze kucheka na kujitizama, akatoka mule ndani na kisha kuanza kunikagua.
" Kama unacheka hivyo una maanisha kuko salama". Akazungumza na nikaitikia kwa kichwa akamtizama yule binti machoni mwake na akatabasamu na wakaanza kuchekana wao kwa wao.
" Ni salama sasa". Nikazungumza huku nikijikaza lile jeraha langu la ubavuni nisionyeshe mbele yao..

( VITA YA MAPENZI SASA INAENDA KUANZA )
ITAENDLEAA......................KWA MARAFIKI HAO......
 
Mnisamehe trhe 28 nachukua likizo ya mwezi mmoja ndo zamu yangu imeanz nimepta likizo ndo tamalizia kazi maan kipnd napost vile nilivyoanza kwa moto nililuwa likiz ko hii likiz tunazimaliza hii likiz nisipomaliz basi mnitukane mtakavyo ndugu zangu
 
Nimefanikiwa kupata likizo mwezi mzima kwahiyo kwanzia leo saa 4 usku mzigo unaanza kushuka kila siku vipande vitatu virefuuuuuuuuuu
 
Bado nazimalizia wazee so msione nipo kimya bado nazimalizia zote mbili ili niziachie kwa pamoja
 
Oi ndo nazimalizia zitakuwa hewani zote kwa pamoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom