Love bite - black chocolate

Love bite - black chocolate

Heheheheee wakija useme nao mwenyewe maana sijawataja kabisaaa, la ujiandae kurudi gerezani na huko ndo utafikisha salamu zangu kwa Silas maana siku zote naona unakaa nazo tuu huzifikishi.😛

Haha hawana noma, bado wanashangaa mjini. Again, simjui any Silas.
 
Pole sana best....ila huyo bae wako atakuwa mjukuu wa vampire huyo. Love bite kimsingi utakachosikia ni raha tuuuu baasi. Anahitaji orientation aisee. Mara nyingi mtu unakuja kushtuliwa na alama aidha wakati unajitazama kwenye kioo au mtu mwingine kukustua.

Huo mchezo hauhitaji hasira na kuanza kuumizana. Ha ha ha

Hahaha hahaha mchezo hauhitaji hasira aiseeeeee hahaha
 
"Kulipokucha bidada akazima simu maana alihisi jamaa angempigia na angerudi kumnyonya damu" HAHAHAHAHAHA
 
Hahahahaha kasinde umenichekesha htr hyo atakuwa dungdunga au vampire hah!!nakumbuka cku moja bae wngu akaniambia natka nikukic shingon mi nikajua just a kiss,akaanza taratibu nikawa nackilizia utamu lol mara kaanza kukaza mdomo mara meno yapo juu ya shingo weee!!!alikula kofi mpka 5 finger zikatokea mana nilihic anataka kunikausha damu!!!!
nimecheka kwa nguvu sana jamani alikuwa kawa vampire ghafla?
 
Habari za jioni,

Mng'ato wa mapenzi - kung'atwa kwa kupenda - mapenzi ya kung'atana - alama ya kuonesha kuwa umetoka kuchubwika n.k. n.k.

Japo ni mambo ya kizungu inatuhusu maana tumeiiga na sidhani kama asili yake ni huku afrika. Nachelea kusema si kila kitu kinafaa kuiga maana yaliyomkuta bidada mmoja wa mjengo flani hamu hana. Huyo dada tunafahamiana ile ya kusalimiana tuu na si zaidi ya hapo. Sasa tulikutana saluni week end hii na akawa anamsimulia huyo mdada mwenye saluni yaliyomsibu kama kawaida masikio hayana kufuli nikiwa nasubiri zamu yangu kunyolewa nikajikuta nasikiliza issue yote.

Bidada akawa anasimulia ijumaa jioni walitoka out na bwana ake hadi usiku mnene jamaa akamrudisha bidada kwake. Kama kawaida ya wapenzi jamaa akaingia kupiga viwili ili nae arudi kwake. Baada ya libeneke kuisha jamaa akamwambia nataka nikuachie love bite bidada akaelewa ni romantic kiss hehehee... weeh anasema nusu azimie. Maana jamaa alikuwa anamnyonya shingoni kwa pembeni kumbuka hapo pamepita mshipa mkubwa unaosambaza damu mwilini hivo bidada alilegea ila jamaa akawa anaongeza nguvu na kung'ata kabisa na meno yeeeeh si ndo bidada akaona mapigo ya moyo yanamtoka na roho inataka muacha huku anajiona.

Jamaa alimnyonya kwa dakika 25 bila kumuachia na hapo aliacha baada ya bidada kuonesha dalili anazimia kama vile kukoroma na kutapatapa.

Jamaa akamwambia kesho nakuja kurudia hadi love bite ionekane. Usiku ule hakumjibu kitu akafunga mlango wake akalala.

Kulipokucha bidada akazima simu maana alihisi jamaa angempigia na angerudi kumnyonya damu, sasa kilichonivunja mbavu kwenye habari hii ni kuwa bidada ni mweusi kama mpoki au lupita nyong'o. Sasa hebu jiulize hizi love bite kwa watu weusi kama Kasie hapa au mpoki si kutafuta kutoana damu kama si kuachiana kidonda maana alama haionekani. Au kidonda ndo love bite yenyewe......? Sasa mbona love yenyewe inasababisha maumivu? Maana kidonda lazima kiume au kung'atwa kunauma au mie sielewi.

Nlichokizoea mie love bite inaonekana kirahisi kwa watu weupe au wazungu wala mtu hutumii nguvu ni vaap love bite hiyoo shingo yote utasema mtu kuvaa cheni ya mbwa heheee

Haya ni mashokolo mageni kwa Kasie sijui ndo uzee.
Hapo hapo huyo mdada wa saluni akaunganisha nyie mapenzi hayana umri, akasema kuna mama mmoja ni mteja wake alienda saluni kwake amfanyie massage yaani huyo mama ni wa miaka 50 hadi 55 yaani alikuwa na love bite shingo yote. Huyo dada wa saluni akabaki anakodoa macho daah hadi bibi kama huyu bado anachubwika ki love bite.

Tukaishia kucheka, nikajikuta nawaza kwa sauti hivi siku Dr. Mengi anatoka kwenye luninga na love bite kibao shingoni si watu watacheka. ... of course atakuwa kaweka na Jackline ila daah mtandio na pull neck vitamhusu looh.

Ushawahi kupata love bite weye? Ulipigwa chata ya wapi? Shingoni? Mguuni? Mkononi? Pajani? .....???

Kasie bin popo.
Usijali sababu mtu hata awe mweusi vipi lakini mapajani na matakono huwa pana unafuu,mimi ndio huwapiga mihuri wanawake sehemu hizo,.
 
You are interested in so many things eeehh.............. I wonder how you manage your interests..............

Anyways, there are things in life are so difficult to explain............ you know why.

Msalimie kabanga maana nae utamsikia ''Aiseeeh.....''

Ha ha ha, kabanga anaweza kusema, "Sawa...!" Kamaliza hapo.
 
Hata mie sijui naona mashokolo mageni tuu ngoja wenye uzoefu nayo watakueleza inawekwaje khaaa ila uw na tahadhari usijepatwa na kesi ya kutaka kuua bila kukusudia hahahahaaa
ahahaha,bite ukitafsiri kiswahili maana yake si kung'ata,bas me nadhani nikimuachia mtu alama za meno ntakuwa nimefanikiwa.kuna jamaa yangu nilikuwa nae somewhere tukakutana na marafiki wa manzi ake wale wadada wakaniambia "sasa na wewe (jina langu) ndo nn kumng'ata mwenzako" me sikujua kinachoendelea ila nikajiongeza nikasema "bwana huyu alinikaba ikabid nimang'ate ili aniachie" wakasema "na nyie mna michezo ya kitoto"tukacheka na kuzuga mada ikaisha,badae jamaa/rafiki yangu akaniambia "daa umecheza kama pele unajua juz kati nilikutana nao wakaniona na love bite shingoni wakaniuliza nimeipataje nikasema wewe(yani mimi) umening'ata" ningekana kama sikumng'ata bas wangejua rafiki yao anasalitiwa kitu ambacho ni kweli.
 
maliza balehe kwanza ndiyo uje hapa!
acha zako wewe,kwani kuweza kuweka hyo love bite ndo kiashirio cha kumaliza balehe? kuna watu kibao hawajui hyo love bite nini na wengine wameoa,btw hzi mambo sisi tunaiga tuu toka kwa tamaduni za magharibi so kama wewe unaona kuweka love bite ndo kupevuka au kukomaa na kukua bas nakuweka kwenye kundi la watumwa wa kifikra.
 
Saluni wanawake wengi wanaenda kujifunza upuuzi!naona kama mtoa mada nae anatamani kung'atwa na hajawahi.

That's what came in your mind.............. there is no way to change it neither to clear the doubt.....

Up to you bro!
 
Haya mambo ya kulambana kama chatu ni hatari sana. Mwenzako kapaka ma-lotion yake na mazagazaga mengine then we unakuja kutia ufundi wako.
Ukipata kansa ya koo unataka uhurumiwe...

wanasemaga ukizama kwenye ulimwengu wa mapenzi, hata mtu aje akupe taarifa kuwa mzazi wako anaumwa kalazwa mahututi hustuki husikii wala huelewi sasa sijui kama akili ikishindwa kung'amua hayo, itaweza kuwaza kuwa mtarajiwa mnyonywa kapaka nini eneo nyonywa.............🙄😕
 
ahahaha,bite ukitafsiri kiswahili maana yake si kung'ata,bas me nadhani nikimuachia mtu alama za meno ntakuwa nimefanikiwa.kuna jamaa yangu nilikuwa nae somewhere tukakutana na marafiki wa manzi ake wale wadada wakaniambia "sasa na wewe (jina langu) ndo nn kumng'ata mwenzako" me sikujua kinachoendelea ila nikajiongeza nikasema "bwana huyu alinikaba ikabid nimang'ate ili aniachie" wakasema "na nyie mna michezo ya kitoto"tukacheka na kuzuga mada ikaisha,badae jamaa/rafiki yangu akaniambia "daa umecheza kama pele unajua juz kati nilikutana nao wakaniona na love bite shingoni wakaniuliza nimeipataje nikasema wewe(yani mimi) umening'ata" ningekana kama sikumng'ata bas wangejua rafiki yao anasalitiwa kitu ambacho ni kweli.

Duuuh kumbe hizi love bite ni hatari kwa mchepuko eeeh, maana ikionekana na watu huku wanajua mwenyemali hajakung'ata basi habari inajulikana kuwa umepita mchepuko heheheee. Ni sheeeedaaaarrr
 
Back
Top Bottom