London Terror Attacks: 6 people killed 20 Injured

London Terror Attacks: 6 people killed 20 Injured

Watabadili vipi mtazamo wakati wanasikia watu wanawaa nchi kwao na majeshi ya magharibi , mfano last week watu 105 innocent wameuwa na majeshi ya US nchini Irak-mosul and 35 watu Syria ?

MSM za nchi za magharibi hilo huwa alisemwi, we chukulia tukio la London CNN imelitangaza kwa zaidi ya masaa sita wana laani magaidi na maneno chungu mzima hakuna anaye sema kwa nini binadamu wenzao wanafikia hatua ya kufanya matukio mabaya kama hayo, wanawachukulia kama ni wendawazimu!! Lakini wazungu kupeleka ndege za kivita mashariki ya kati, Libya na Afghanistani kuuwa raia wasio na hatia including walio mahospitalini, misikitini , kwenye harusi na mashuleni kwao wanalichukulia kama jambo la kawaida kabisa wanasahau kwamba raia waliouwawa wana ndugu zao, wajomba zao nk hivyo ni rahisi sana kwao kulipiza kisasi - na sijui kwa nini wazungu washangae vitu kama hivyo.

Haya chukulia mfano wa last week, ndege za Marekani zili dondosha mabomu na kuuwa raia 140 kwa mpigo, je, CNN au BBC zilitangaza kwa siku nzima jinsi ndege za Merikani zilivyo uuwa innocent people - hakuna!! Leo hii CNN/BBC wanatangazia Dunia kwa takribani masaa sita kuhusu tukio la London la watu sita kupoteza maisha, to them binadamu ni wazungu tu the rest ni expendable!!

Wazungu walivyo wa ajabu hakuna hata mmoja aliwahi kukaa chini na kufanya a simple arithmetic kwamba wanapo tumia ndege zao za vita kuua rais wasio na hatia wanatengeneza maadui wangapi ambao wako tayari kulipiza kisasi siyo kwa kutumia ndege, vifaru au makombora bila kutumia binadamu kujilipua, kukanyaga watu wa magari madogo na malori, kubamiza ndege za abiria na kutumia visu na hiki ndicho kinacho endelea na si rahisi kujikinga dhidi ya terrorist ambaye yuko determined kufanya lolote, aogopi kitu kwa sababu hana cha kupoteza, kama Wazungu wangefanya mahesabu kidogo kutathimi matendo yao yanavyo zalisha maadui lukuki bila ya kutegemea nadhani wanapaswa kujirudi haraka sana - ngoja nitoe mfano kidogo to drive point home:Tuchukulie kwamba kila raia anaye uwawa na ndege za vita za Marekani na Uingereza kuna nyuma yake wafiwa kama ndugu,wajomba, wanaukoo wote hao idadi yao ni zaidi ya ishirini na hiyo ni conservative figure, sasa zidisha 140 mara ishirini unapata watu/raia 2400 ambao wamegusa moja kwa moja na vifo vya ndugu/jamaa zao vilivyo sababishwa na ndege za kivita - Amerika na nchi za magharibi zinajikuta zinazalisha maadui zaidi ya 2400 kwa tukio moja la ndege zao kudondosha mabomu kwa nchi za watu - la kujiuliza hapa, huu ni mwaka wa ngapi tangu Wamerika, Waingereza wajiingize kwenye mambo ya ndani ya Mataifa ya Africa Kasikazini, Mashariki ya kati na Afghanistani na kufanya uharibifu mkubwa kwa binadamu na mali zao, hivi wanategemea watavuna nini as days goesby - ma refugees wanao wapokea kutoka kanda hizo tajwa ndiyo watawapa wakati mgumu na si ma refugees tu hata Ria wengi wa kigeni walio hamia huko kihalali kwa miaka mingi nao wanashiriki kikamilifu katika masuala ya kigaidi kutokana na ndugu na jamaa zao katika country of their origin kuuwawa kikatiri na ndege za vita za nchi za magharibi.

Amerika na marafiki zao wasifikiri wana haki ya kuvuruga amani kwenye Mataifa ya kigeni halafu wao wakaendelea kula kuku kwa mrija - wanapaswa kujiangalia/tathimini upya katika masuala ya Geopolitics wasifikiri wataendelea kunyanyasa watu miaka nenda rudi - Korea Kasikazini imeonyesha mfano na kuna Mataifa mengi yanao wa support kimya kimya.
 
Bado hawajadigest la Manchester,ila nashangaa hawa Waingereza hawajajifunza kwa jirani zao France?Au wao walijua wako safe?
Kwa muda mrefu walifanikiwa kugundua mipango kabla haijatokea kupitia info za MI5, jamaa sasa wanawazidi ujanja.
 
London is burning, see yonder.....mwisho wa dunia! Maumivu huanA polepole
 
Hii idadi inaweza kabisa kuongezeka maana majeruhi ni 30. Thanks God UK bunduki hazipatikani kirahisi kama Marekani ingekuwa hivyo idadi ya wafu ingepanda zaidi.

Kuna watu wako in critical
Majeruhi ni zaidi ya 47
Ila hizi incidence za kugonga watu, kuchoma visu zitazidi sana nchi za ulaya
Mfano hao wauaji walikuwa wamevaa fake explosive vests
 
Nimesema nawaogopa waarabu,matukio yote yaliyopita ya kigaidi hapa ulaya wahusika ni waarabu,mind you that hakuna nilipotaja kuwa wahusika wa leo ni waarabu pia,ila probability ni kubwa mno kuwa na wa leo nao watakuwa waarabu tu.Huhitaji kuwa rocket scientist kutambua hilo
2013 London-Nigerian born walifanya shambulizi Woolwich na kumchinja mwanajeshi
 
Wewe hayajakukuta,binadam wote waoga wakihisi hali ya hatari,Adrenaline inafanya kazi.Ila ukiwa haupo kwenye hiyo hatari waweza cheka wanavyoreak.Kule Belgium ilipotokea mlipuko aiport jamani watu walikimbia balaa.
ni mazoea tu,
niliwahi kushuhudia Gaza,ndege zinashambulia mtaa huo huo watu wanaendelea na shughuli kama kawaida,
kuna maeneo watu walishakua sugu
 
MSM za nchi za magharibi hilo huwa alisemwi, we chukulia tukio la London CNN imelitangaza kwa zaidi ya masaa sita wana laani magaidi na maneno chungu mzima hakuna anaye sema kwa nini binadamu wenzao wanafikia hatua ya kufanya matukio mabaya kama hayo, wanawachukulia kama ni wendawazimu!! Lakini wazungu kupeleka ndege za kivita mashariki ya kati, Libya na Afghanistani kuuwa raia wasio na hatia including walio mahospitalini, misikitini , kwenye harusi na mashuleni kwao wanalichukulia kama jambo la kawaida kabisa wanasahau kwamba raia waliouwawa wana ndugu zao, wajomba zao nk hivyo ni rahisi sana kwao kulipiza kisasi - chukulia mfano wa last week ndege za Marekani zilivo dondosha mabomu na kuuwa raia 140 kwa mpigo - sasa tuchukulie kwamba kila raia aliye uwawa kuna ndugu,wajomba, wana ukoo zaidi ya ishirini nyuma yake, sasa zidisha 140 mara ishirini unapata watu/raia 2400 ambao wamegusa moja kwa moja na vifo vya ndugu/jamaa zao - Amerika na nchi za magharibi zinajikuta zinazalisha maadui zaidi ya 2400 kwa tukio moja la ndege zao kudondosha mabomu kwa nchi za watu - la kujiuliza hapa huu ni mwaka wa ngapi tangu Wamerika, Waingereza wajiingize kwenye mambo ya ndani ya Maifa ya Africa Kasikazini, Mashariki ya kati na Afghanistani na kufanya uharibifu mkubwa kwa binadamu na mali, hivi wanategemea watavuna nini as days goesby - ma refugees wanao wapokea kutoka kanda hizo tajwa ndiyo watawapa wakati mgumu na si ma refugees tu hata Ria wengi wa kigeni walio hamia huko kihalali kwa miaka mingi nao wanashiriki kikamilifu katika masuala ya kigaidi.

Amerika na marafiki zao wasifikiri wana haki ya kuvuruga amani kwenye Mataifa ya kigeni halafu wao wakaendelea kula kuku kwa mrija - wanapaswa kujiangalia/tathimini upya katika masuala ya Geopolitics wasifikiri wataendelea kunyanyasa watu miaka nenda rudi - Korea Kasikazini imeonyesha mfano na kuna Mataifa mengi yanao wa support kimya kimya.
Ni kweli mkuu wao wanafikiri kuna watu wana haki ya kufa na wengine hawana haki hiyo , binafsi uwa najiuliza saana hivi watu wanaona mauaji yanayofanywa na US na washirika wake nchi nyingine ?
 
London is burning, see yonder.....mwisho wa dunia! Maumivu huanA nchi za ulaya zingejifunza kitu zisivamie na kuvuruga nchi za watu,kwani wao ulaya wako karibu na afrika, asia /middle east , wenzao US yuko mbali ,US anachokoza majanga anawaachia wao wanaangaika
 
Ni kweli mkuu wao wanafikiri kuna watu wana haki ya kufa na wengine hawana haki hiyo , binafsi uwa najiuliza saana hivi watu wanaona mauaji yanayofanywa na US na washirika wake nchi nyingine ?

Mkuu kinacho shangaza zaidi ni waswahili wanao support blindly ushezi wa mataifa haya dhalimu, miaka ya nyuma niliwahi kusoma comments za Mpalestina kwenye magazeti ya magharibi alisema hivi: " Wazungu na Vyombo vyao vya habari magharibi ni binadamu wa ajabu, wanaweza kupoteza siku nzima wanazungumzia Paka aliyekwama kwenye mtaro wa maji machafu, lakini linapo kuja suala la ndege zao kuua binadamu huko Mashariki ya kati na Mataifa mengine yanayo endelea habari hizo uwa hazitangazwi kabisa i.e coverage yake ni sawa sawa na hakuna" huu ndiyo unafiki wa watu hawa - na wakiendelea na tabia zao hizi basi WW3 inaweza kufumuka muda wowote within our lifetime.

Watu hawajui tu - Mataifa kama Uchina, Iran, Korea Kasikazini, Urusi possibly na India vita ikitokea wataungana kumpa fundisho Marekani, kitakacho waunganisha ni kutokana na Amerika kutokuwa predictable mfano wakiwapiga vita let say na Uchina Mataifa tajwa hapo juu hayawezi kujua kesho atashambuliwa nani kati yao, hivyo kumaliza donda ndugu hili ni kuhakikiza wanaungana na kuipiga USA back to stone age tena ndani ya Taifa lao ili USA asiendelee kuwa kero Duniani, na wao watapata hasara lakini Amerika ndiyo itadhuliza zaidi, sijui USA kama akili za kulitambua hilo wanalao.

Yaliyo mpata Hitler wakati wa WW2 yanaweza kujirudia kwa taifa la Marekani, USA ana maadui wengi yeye ajui tu, hata Japan na Ujerumani zinaweza kumugehuka USA wakiona mabo ya vita yanamwendea vibaya i.e hakuna dalili ya kushinda - hilo likitokea Japan itaungana na maadui wa Marekani kulipiza kisasi cha Taifa lao kupigwa mabom mawili ya Nuclear na USA na kuua Wajapan wengi, Japan haijasahau mauuaji hayo ingawa inakaa kimya, Ujerumani vile vile itahungana na maadui wa Marekani kulipiza kisasi cha miji yake kupigwa mambom lukuki na ndege za USA na kuua raia wengi sana wa Ujerumani wakati wa WW2 , Wamerika walipiga mabom Ujerumani mwisho mwishoni mwa WW2 bila sababu yoyte ya msingi huku wakijua Wajerumani walikuwa karibu ku surrender na hawakuwa na nguvu za kijeshi kupigana tena, lakini miji yao muhimu ikapigwa mabomu regardless!!
 
Umefufukia huku , ??? Umekuwa kama mwizi umekimbia majukwaa ya dini ukazuka hapa???

Wewe kimbilia kugeuzwa ndafu na sangara

Everybody will be salted in fire Mark 9:49
Naona avatar yako umesha olewa..[emoji4]
 
55be2b31478ad697bb9bb04b1e8e2962.jpg
...dogo nawe umegoma kula mchana au hujauona nyota...[emoji47]
 
Acha wanyooshwe... Wakati Trump anakazana kuweka vizuizi vya wageni wasio na tija na kufukuza wasio na vibali vya kuishi USA, wenyewe wanakazana kumpinga nakusema kuwa ni " It's inhuman"
Hili ni fundisho tosha kwa wanaompinga Trump kwenye hii issue ya timua timua... Hawa jamaa si wakuwaamini hata siku moja.. Ni watu wamatukio tuu.. Kibaya Zaidi wanaua watu wasio husika na issue zao...
 
Back
Top Bottom