London Terror Attacks: 6 people killed 20 Injured

London Terror Attacks: 6 people killed 20 Injured

Sio wote ila kusema ukweli hawa jamaa wana tabia za ajabu ajabu sana.
Nchi za kiarab zikemee nini wakati hawa watu ni raia wa UK ni jukumu lao waingereza kupambana wenyewe siwanadai wao wanawapelelezi wakubwa vifaa vya kujilinda na wanaweza kupigana na taifa lolote na kuondoa viongozi wa nchi huru madarakani mf.Saddam husein na Gaddafi na sasa wanapigana syria kumuondoa Bashar al Asad wajilinde na nyumbani sasa yasitokee
 
Washambuliaji watatu, ambao walikuwa wamevalia mikanda ya bandia ya miripuko , pia walipigwa risasi na polisi na wamefariki, polisi ya mjini London imesema.

39110450_404.jpg

M;ajeruhi wakipelekwa hospitali baada ya tukio la kigaidi mjini London

"Katika wakati huu, tunaamini kwamba watu sita wameuwawa pamoja na washambuliaji watatu waliopigwa risasi na polisi," amesema kamishna msaidizi Mark Rowley , ambae pia ni mkuu wa kitengo cha kupambana na ugaidi.

Washukiwa waliwagonga wapita njia katika daraja la London kabla ya kuwashambulia watu katika baa za karibu na migahawa, Rowley alisema. Polisi wenye silaha waliwapiga risasi washambuliaji watatu katika muda wa dakika nane baada ya polisi kupokea siku ya kwanza ya kuhusiana na mashambulio hayo ya kigaidi katikati ya London usiku wa Jumamosi, amesema.

Simu ya kwanza ilipokelewa baada ya washambuliaji kuendesha gari yao na kuwagonga wapita njia katika daraja la London kabla ya kuwachoma visu watu katika soko la karibu la Borough, Rowley amesema.

39110508_404.jpg

Polisi wakilinda usalama katika eneo la tukio la kigaidi mjini London

Watu walioshuhudia waliliambia gazeti la Guardian waliwaona watu wawili wakiwachoma visu watu nje ya mgahawa maarufu wa Roast katika soko la Borough. "Niliwaona watu wawili wakiwa na visu vikubwa nje ya mgahawa huo wa Roast," mpishi kutoka katika mgahawa wa karibu aliliambia gazeti hilo.

Polisi wachukua hatua ya haraka

Walikuwa wakiwachoma visu watu , tulikuwa tunapiga kelele "acha, acha" na watu walikuwa wakiwatupia viti," mpishi huyo alisema. "polisi walikuja na kuwapiga risasi watu hao moja kwa moja."

39110373_404.jpg

Watu ambao walipata mshituko baada ya tukio la kigaidi mjini London

Waziri mkuu Theresa May aliliita shambulio hilo kuwa "tukio la kigaidi" na alieleza "shukrani zake nyingi" kwa polisi na huduma za dharura. Meya wa London Sadiq Khan amesema anapanga kuhudhuria mkutano mapema leo Jumapili (04.06.2017) wa kamati ya dharura ya serikali inayojulikana kama cobra, ambayo inatarajiwa kuongozwa na waziri mkuu May.

"Mpaka sasa hatufahamu maelezo zaidi, lakini hili lilikuwa shambulio la makusudi na la waoga dhidi ya wakaazi wa London ambao hawana hatia na watu wanaotembelea mji wetu wakifurahia usiku wao wa Jumamosi," Khan alisema.

Trump azungumza na May

Rais donald Trump amempigia simu waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na kumpa rambi brambi zake kufuatia tukio la kigaidi mjini London.

39110274_404.jpg

Watu wakikimbia kutoka eneo la tukio mjini London

Rais Trump alizungumza na waziri mkuu May leo na alitoa rambi rambi zake kwa shambulio hilo la kinyama la kigaidi katikati ya London.Trump aliahidi msaada kwa Uingereza kutokana na mashambulio hayo mawili ya kigaidi ambapo watu sita waliuwawa , baada ya gari kuwagonga wapita njia na washambuliaji hao kuwachoma visu watu kadha.

Katika mazungumzo yao ya simu Trump aliahidi kwamba Marekani itatoa ushirikiano kamili kwa Uingereza katika uchunguzi wa tukio hilo na kuwafikisha watu wanaohusika na tukio hilo la kiuwoga mbele ya sheria.

39110597_404.jpg

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema kwamba wacanada , "wanasimama pamoja na Waingereza" baada ya washambuliaji kuwachoma visu holela watu na kuwagonga wapita njia kwa gari na kuuwa watu sita.
 
Duh

Risasi nazo, tusubirie kujua zaidi

Maeneo hayo kwa matanuzi pia lazima watu wanasepa, walio njiani wanageuza kurudi makwao.
Hiyo picha kwenye avatar ni yako my?samahani kama ni Me.
 
Kumbe nchi za magharibi ndiko kuna watu wenye kustahili kuishi pekee, mashariki ya kati wao hawastahili kuishi
 
Haya mambo ya haki za binadamu, kuna wakati yanasababisha kupotea kwa haki ya kuishi kwa binadamu wengine.

Trump alikuwa sahihi. Ni lazima kuwe na udhibiti mkubwa wa wageni toka kwa mataifa ya kiarabu kwenda mataifa ya Ulaya na Amerika. Ni ngumu sana kutenganisha kati ya Waarabu wema na waarabu magaidi japo ni wachache sana ukilinganisha na wale walio wema.

Kuna wakati Israel inalaumiwa sana kwa kutowatendea haki Wapalestina. Lakini kwa kiasi kikubwa Israel inawahakikishia usalama wananchi wake kuliko nchi za Ulaya, licha ya kuzungukwa na mataifa adui. Magaidi wanajua kabisa kuwa shambulio moja dhidi ya Israel itasababisha mashambulio zaidi ya 10 dhidi yao, familia zao na hata dhidi ya watu wasio na hatia wa jamii yao. Inaweza isiwe njia sahihi, lakini wafanye nini?

Nchi za Ulaya zisipochukua hatua madhubuti, nchi zao zitageuka kuwa mahali hatari kwa usalama wa wananchi wao.
 
Waislam wenye misimamo mikali ni tatizo.
Well said, inasikitisha sana sana! Utukufu wa Mwenye Enzi Mungu ni binadamu kuwa hai! Sijui faith ya namna gani inayo mfanya mtu kujitoa mhanga!
 
Haiwezi kuwa ajabu iwapo hili tukio ni mtu alipanga na kuhusisha waislamu ili aungwe mkono kwenye kupitisha travel ban.
 
Back
Top Bottom