Liyumba Kuachiwa Huru Leo?

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Je hukumu dhidi ya Liyumba leo inaweza kuwa ya pili baada ya kusota gerezani kwa muda mrefu tu kutokana na kunyimwa dhamana?Je kesi hii ina 'mengine binafsi' zaidi ya ubadhirifu wa fedha za umma?Je waendesha mashtaka wa serikali wataweza kuondoa hisia za baadhi ya wanajamii kuwa 'uchovu wao kitaaluma' umekuwa kikwazo kwa jamuhuri kushinda kesi nyingi za 'high profile'?Yote haya yanajadiliwa kwa mapana na marefu hapa Liyumba Kuachiwa Huru Leo? | KULIKONI UGHAIBUNI
 
possible, kuna kitu wanaita 'justice' sijui neno sahihi la kiswahili ni lipi.
 
Leo huyo fisadi huenda akaachiwa pia kama ilvokuwa kwa akina mramba na wenzake, hiyo ndo CCM bwana.
 
............Bora t u naye wamwachie mbona walimuachia Mramba, Yona, na Chenge wala hawajamgusa kabisa, kwanza hizo pesa hakula peke yake.
 
Maneno ya wale wafadhili wa bajeti yetu yatatimia leo, Liyumba hana kesi ila kabambikiwa au katolewa kafara tu.Kwani ni mafisadi wangapi wako nje hawajashtakiwa? Hii ndio bongo bwana inayojengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo.
 
Haya maigizo yana tija yeyote kwa taifa? Seems watu wako inclined na kuona mtu yupo behind bars badala ya ku-recover kilicho chetu.
 
i wont raise my hopes up ati kwamba kuna "justice" yoyote itakayotendeka.......HAKUNA. Huyo ni mwenzao na leo nadhani kuna part imeandaliwa somewhere ya kumkaribisha nyumbani (jinsi gani natamani isiwe hivyo):angry:
 
Hana kesi ya kujibu ule ni usanii wa serikali ,kwanza atadai fidia tutamlipa mpaka tuchakae.tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
Hakuna kesi dhaifu kama hii ya Liyumba; hata wakiweza kumkuta na hatia (which I doubt) kesiyake haiwezi kusimama kwenye rufaa. So.. natabiri mahakama itamkuta hana hatia kwani mzigo wa ushahidi ulikuwa uko kwa serikali. Mtu aliyetakiwa kufikishwa mahakamani alikuwa ni Ballali. So.. kama kesi ya Zombe.. mshtakiwa mwenyewe hayupo! Tatizo serikali itasema inataka kukata rufaa "haijaridhika".. hii ni preview tu ya kesi za Yona, Mgonja na Mramba.
 
Miafrika jinsi tulivyo tutanyweshwa hii kesi na kutakuwa hakuna lolote la kufanya! Hakuna wa EPA atakayefungwa, hasa mwaka huu wa uchaguzi, kwani kufanya hivyo ina maana CCM ilifaidi na mahela yaliyoibiwa. Majaji wameagizwa kuhakikisha hakuna atakayeenda Lupango.
 
Hakuna kesi dhaifu kama hii ya Liyumba; hata wakiweza kumkuta na hatia (which I doubt) kesiyake haiwezi kusimama kwenye rufaa. So.. natabiri mahakama itamkuta hana hatia kwani mzigo wa ushahidi ulikuwa uko kwa serikali. Mtu aliyetakiwa kufikishwa mahakamani alikuwa ni Ballali. So.. kama kesi ya Zombe.. mshtakiwa mwenyewe hayupo! Tatizo serikali itasema inataka kukata rufaa "haijaridhika".. hii ni preview tu ya kesi za Yona, Mgonja na Mramba.

Ni kweli kabisa! Na wao wakaifanya eti kesi ni ni serious na wakamnyima dhamana! Inasikitisha kuona usanii wa aina hii unaishirikisha Judiciary yetu pia! Watanzania tumemalizwa kabisa!
 
Je waendesha mashtaka wa serikali wataweza kuondoa hisia za baadhi ya wanajamii kuwa 'uchovu wao kitaaluma' umekuwa kikwazo kwa jamuhuri kushinda kesi nyingi za 'high profile'?Liyumba Kuachiwa Huru Leo? | KULIKONI UGHAIBUNI

Na wasiwasi sana na kama unaushahidi wa kuonyesha waendesha mashtaka wa serikali "ni wachovu kitaaluma". Kushinda au kushindwa kesi inategemea mambo mengi. lakini kwenye high profile kesi unazo sema tatizo ni system mbovu. Bila kujenga system through strong institutions sahau. Kubwa kabla ya kuhukumu taaluma, tuangalie kwanza mfumo mzima wa mashitaka ulivyokaa hapa kwetu
 
Hakuna kesi dhaifu kama hii ya Liyumba; hata wakiweza kumkuta na hatia (which I doubt) kesiyake haiwezi kusimama kwenye rufaa. So.. natabiri mahakama itamkuta hana hatia kwani mzigo wa ushahidi ulikuwa uko kwa serikali. Mtu aliyetakiwa kufikishwa mahakamani alikuwa ni Ballali. So.. kama kesi ya Zombe.. mshtakiwa mwenyewe hayupo! Tatizo serikali itasema inataka kukata rufaa "haijaridhika".. hii ni preview tu ya kesi za Yona, Mgonja na Mramba.
.
Mzee Mwanakijiji, hili nilishalisemea kule nyuma kuwa Liyumba, anaonewa bure!. Haikuhitaji mtu kujua sheria, kuona makosa ya wazi kwenye kesi ya msingi ambayo the charge was defective ab inition (toka mwanzo). Huwezi kumshtaki mtu for the full value ya Twin Tower wakati majengo yapo yale yamesimama na tunayaona kwa macho.

The right forum ilikuwa ni kufanyika kwa thathmini ya thamani halisi ya majengo hayo, halafu unaangalia kiasi kilicholipwa, ndipo Liyumba angeshitakiwa kwa diference btn thamani halisi na cha juu walichoongezea kugawana.

Japo sitetei ufisadi wa aina yoyote, lakini kwa wapenda haki, wangependa kuona Liyumba anatendewa haki, baada ya kukaa jela miaka miwili leo ataachiwa na mawakili wake wataishitaki serikali na atalipwa mamilioni ya fidia.

Kesi ya Kina Mramba, Yona na Mgonja ni hivyo hivyo. Serikali yetu imejaa wanasheria duni, matokeo yake ni kuharakisha defective charges mahakamani at the end of the day, serikali inashindwa.

Niliposema enzi zile kuwa kesi zote hizi pamoja na za EPA, hakuna kitu humo, nilionekana ni mtu wa ajabu, lakini angalau sasa ukweli ndio huu unakuja kudhihirika.
 
Natabiri attachiwa huru. Hii ndio bongo bwana mtu anadanga umri anajiuzulu na mwingine anatudanganya elimu anaendelea kula bata
 
Kama Mahakama ilishamwona Liyumba hana hatia (hana kesi ya kujibu) katika kuisababishia hasara Serikali, sioni itamkutaje na kosa la kutumia vibaya madaraka! All in all, nionavyo kwenye kesi hii Liyumba atalala leo nyumbani kwake na my wife wake (kama yupo), pamoja na kufanya tafrija ya kushinda kesi na familia yake!
 
Hakuna kesi dhaifu kama hii ya Liyumba; hata wakiweza kumkuta na hatia (which I doubt) kesiyake haiwezi kusimama kwenye rufaa. So.. natabiri mahakama itamkuta hana hatia kwani mzigo wa ushahidi ulikuwa uko kwa serikali. Mtu aliyetakiwa kufikishwa mahakamani alikuwa ni Ballali. So.. kama kesi ya Zombe.. mshtakiwa mwenyewe hayupo! Tatizo serikali itasema inataka kukata rufaa "haijaridhika".. hii ni preview tu ya kesi za Yona, Mgonja na Mramba.

Well presented!! Welcome home Bro Liyumba!! Haya ndiyo matamanio yangu kwa kuwa serikali imebagua!! Kama ilikuwa inataka kutenda haki ingewafikisha mbele ya sheri wale wote waliohusika na tuhuma za kuisababishia serikali hasara akiwemo kiongozi wao RA. Kwa nini Liyumba ateseke peke yake wakati wamekula wengi? Kwa nini EPA iliyopelekwa mahakamani iwe ya utatuta, tena ile figure halisi ya EPA bil 600 imefanyiwa upambe hadi kufikia bil 133? Yapo mengi ya uozo, nasikia kichefuchefu.

Majaji wameagizwa kuhakikisha hakuna atakayeenda Lupango.
Mimi sidhani kama majaji wameagizwa hivyo. Kama ulifuatilia kesi nzima ni wazi Liyumba ataachiwa tu, hata ungekuwa wewe ndiye jaji. Kwanza kuna shahidi upande wa mashtaka alisema ukaguzi wa majengo haujafanyika hivyo hatuwezi kujua kama serikali imepata hasara yoyote,Hapa ina maana hakuna mtaalamu aliyethibitisha hasara. Pili kumbuka alipoitwa Juma ambaye nadhani ni gavana masaidizi - yeye alisema wazi kuwa hajui kama serikali imepata hasara yoyote; kumbuka pia huyu ni shahidi upande wa mashtaka.
Kumbuka pia kuwa ilielezwa utaratibu kuwa mabadiliko yoyote yaliidhinishwa ma bodi, sasa kama bodi yenyewe ilikuwa ya vihiyo ikaidhinisha mabadiliko, unamfungaje Liyumba?
Generally framing yenyewe ya case na ushahidi ulioletwa kimaksudi umekuwa ni dhaifu sana.
Mimi nadhani waliopewa maelekezo kuwa watu wasifungwe ni waendesha mashtaka, kwani wanahakikisha wanapeleka ushahidi dhaifu.
Anyway dawa yao iko jikoni - nikuiondoa CCM madarakani halafu kesi hizi zinafunguliwa upya kwani utakuwa umepatikana ushahidi mpya
 
Back
Top Bottom