Liwe ni fundisho kwa yaliyowapata Ben Saanane na Mpoki Mwambulukutu(Mchambuzi)

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Kwanza nianze kwa kuwapongeza hawa wanachama wenzetu wa Jamiiforums kwa kuthubutu, kutenda na hatimaye kuangukia pua katika kinyang'anyilo cha kuteuliwa kuwa mgombea ubunge kwa kupitia tiketi ya CHADEMA.

Pili, ninaomba liwe ni fundisho kwa siku zijazo kwetu wanaJF kama tutaamua kutaka kugombea katika uongozi kwa njia ya kupigiwa kura.

Tunatakiwa tujifunze kuwa, kufahamika sana au kuwa maarufu katika Jamiiforums siyo kigezo timilifu cha kukufanya ueleweke na kukubalika katika jamii kiasi cha kukuwezesha kupewa uongozi kwa njia ya kura.

Lazima tuelewe kuwa, Jamiiforums can be applied as a launching pad for political aspiration and not landing pad for Trumping Political Success.

Jamiiforums is too global to triumph locally!

Tatizo la Jamiiforums unaweza ukawa unapata LIKE nyingi za watu kama mimi ambao tuko Bariadi Kijijini wakati wewe unaenda kugombea jimbo la Nkasi Kusini, Mkoani Rukwa, kwa lugha nyingine, kufahamika sana Jamiiforums kwa michango yako mizuri siyo ishara kama unafahamika sana na kwa mazuri nje ya Jamiiforums.

Hawa wanachama wenzetu waliamua kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kuwa wagombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kupata LIKE nyingi sana hapa Jamiiforums katika michango mbali mbali lakini kwa vile wanachama wengi wa CHADEMA kule ‘site' hawafahamu hata uwepo wa Jamiiforums achilia mbali maana ya LIKE , wamewanyima kura za kutosha kuweza kuteuliwa kuwa wagombea Ubunge.

Ben Saanane ameambulia kura 26 kati ya kura 397 zilizopigwa katika Jimbo la Rombo, Mkoani Kilimanjaro.

Mpoki Mwambulukutu anayejulikana hapa JF kama Mchambuzi alichukua fomu katika Jimbo la Kinondoni lakini hakuirudisha! Kwa sasa nimeambiwa anadai hakufahamu vizuri siku ya kurudisha fomu na pia siku ya kupiga kura za maoni wakati CHADEMA walitangaza ratiba zake mpaka kwenye vyombo vya habari!

Haiingii akilini kama una akili timamu uchukue fomu halafu usifahamu siku ya kurudisha na kupiga kura. Kwa nini wengine walirudisha fomu na kupigiwa kura?

Matokeo katika Jimbo la Kinondoni kwa wale waliorudisha fomu yalikuwa, Mustafa Muro aliyepata kura (47), Susan Lyimo (32), Rose Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na Francis Nyerere (0).

Hizi ni lugha za kisiasa! Nadhani baada ya kunusa hali halisi ya mpambano aliamua ‘kulala mbele'.

Vijana kama kina Mnyika, Mdee na Zitto harakati zao kuingia bungeni zilianzia ''site'' kwenye ground zero, Jamiiforums ilikuwa ni political launching pad katika kuyafikia malengo yao.

Kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!

Safari ya kisiasa kufika kileleni ni safari ndefu sana!
 
Smart thread! Inabidi kama una plan ya kugombea jimbo uliloko mbali nale basi Nenda mapema wanamji wakujue vena. Inawezeka toka umalize Primary hujawahi kurudi kwenu na wapiga kura wako hata jina hawajawahi kulisikia.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimebuni mbinu mpya ya kudhibiti mamluki wanaochukua fomu za kugombea kupitia chama hicho kisha kutokomea nazo mitini.

Sasa watakaopitishwa na kupewa fomu za chama hicho kugombea ubunge au udiwani, watatakiwa kusaini fomu maalumu mbele ya mahakama ili wakitokomea bila kurejesha fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), wapandishwe mahakamani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Jijini Mwanza.

"Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa, wagombea wetu wote tutawasainisha mahakamani na wakishindwa kurudisha fomu, tutawashughulikia mahakamani," amesema Dk. Slaa na kuongeza;
 
Smart thread! Inabidi kama una plan ya kugombea jimbo uliloko mbali nale basi Nenda mapema wanamji wakujue vena. Inawezeka toka umalize Primary hujawahi kurudi kwenu na wapiga kura wako hata jina hawajawahi kulisikia.
Mkuu,
Ninakubaliana na ushauri wako.

Huwezi kuja Bariadi Kijijini kuomba tukupatie uongozi kwa kigezo cha kujulikana kwenye mitandao wakati uliondoka ukiwa unanyonya na hujawahi kurudi tena au kushiriki katika ujenzi wa jamii.
 
Daaaah, kwa hiyo ile slogan yetu ’TWENDE BUNGENI NA BEN SAANANE’ ndo imeishia ROMBO?? Aseee, naanza kuifananisha na ile ’SAFARI YA MATUMAINI’ iliyoishia DODOMA.Sasa kuhusu ile michango inakuwaje? Maana braza alikuwa anaichanga kwelikweli ili aende bungeni.
 
Asipopigwa ban kwa name calling naishtaki JF kwa kunisababishia usumbufu usio wa lazima
Mkuu,
Jamiiforums ina MOD's ambao wanaifahamu vizuri kazi yao.

Huhitaji kuwafundisha kazi yao, kama unataka kufahamu kama wanafahamu vizuri kazi yao, vunja taratibu na sheria!
 
Back
Top Bottom