Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Haya Magoli tunayataka afunge kwenye Mechi Muhimu sio asubiri Timu ambazo hazionekani hata kwenye ChatGPT ndiyo atambe! Anyway niliwahi kujiuliza how PSG watuuzie best player? Mbona kama kuna kitu hakipo sawa hivi.
Kweli kabisa dogo mechi muhimu EPL amekua sio kwa sasa. Kocha anamtetea ni mgeni pia hakuna na preseason nk nk hivyo tuwe na subira mazuri yanakuja , muda utasema kama mwalimu yupo sahihi. Hii hat trick itampa kujiamini zaidi.
Hilo la PSG kutuuzia mchezaji Bora sio kweli pale dogo hakua starter alikua bench warmer ama super sub na alivyoona Enrique anawapedelea Dembele, Khavicha na Desire akaanza kusaka timu ili angalau awe chaguo la kwanza, kimsingi Liverpool hapa wamejipigisha tu wenyewe walipe pesa nyingi 123m kwa huyu dogo japo kipaji sio kwa bei hio hivyo upo sahihi kuna kitu hakipo sawa pengine ndio maana Hughes akasepa zake na kuachia Ward nafasi.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…