Live updates: Tanzania vs zimbabwe

Live updates: Tanzania vs zimbabwe

Rais nipo positive ila ushindi wa goli moja kweli kaka tusiweke siasa elewa kabisa wao wamekuja kutafuta draw ama kufungwa c zaidi ya moja na wamefanikiwa tupo pamoja ila safari n ndefu sanaa kaka malinzi,

Tuwe na mjadala mpana sana kuhusu soka letu bila hivyo hatutaenda popote pale itabakia ivi tuu
 
bwana malinzi hii ni timu ya taifa gani ? tanganyika au Tanzania?

nauliza maana nnaona wote wachezaji ni wa upande mmoja au timu za zanzibar hazina uwezo wa kutoa wachezaji kuwakilisha Taifa ?
 
Yaani Samatta na Ulimwengu tofauti yao imeonekana kabisaa kama wanacheza nje!! Nakumbuka kuna kipindi Ulimwengu tulikua tunamzomea pale Taifa ,lakini sasa hiv tunampigia magoti dah!!
Welldone Taifa Stars.
 
be positive mshazari,siku ile nilikwambia wao watakuwa 11 na sisi 11,Harare itakuwa ni hivyo hivyo,tutapambana.

Mkuu Malinzi, with due respect, tumekuwa "positive" tangu 1961! What do we have to show for all this time? Hata mimi niko pessimistic kidogo!

Again, with due respect, unaonaje mkiliangalia upya suala la sisi kung'ang'ania Uanachama wa "Shirikisho la Wachovu" (CECAFA), kuna sababu gani inayotuzuia sisi kujiunga na COSAFA ambako kuna ushindani zaidi? Hebu fikiria tukutane kila mwaka na A. Kusini, Zimbabwe, Malawi, Zambia, Botswana, angola, Malawi, Swaziland, n.k? Ninaamini tukihamia huko, baada ya vichapo kadhaa, tutapiga hatua kuliko kila mwaka kukutana na Timu kama Somalia, Eritrea, Burundi, n.k.

Kama ni vigumu sisi kujitoa CECAFA, basi angalau tuombe kualikwa mara moja moja. Kiwango cha Timu za COSAFA kiko juu kuliko cha CECAFA. Tunahitaji ushindani huo. Ninaamini wenzetu wa Nchi Jirani wangekuwa hapa kwetu ki-Jiografia wangekuwa tayari washatosa CECAFA kama walivyofanya Zambia, tena kwa manufaa makubwa baada ya Miaka kadhaa.

Ni mawazo yangu tu Mkuu! Asante!
 
Wenzetu wa Kenya walivoachana na siasa za Gor Mahia na AFC Leopards ndipo mpira ulianza kupanda kimataifa, leo wana wachezaji wanaocheza premier league England, Ufaransa, Italy, na mwaka huu mkenya mwenye uraia wa Ubelgiji atacheza kombe la dunia.

Uganda hali kadhalika hivyo hivyo baada ya Express na Villa kupotea wapo mbali sana, leo hii waganda wanacheza mpaka ligi daraja la kwanza Scotland etc. Na akina Okwi ndiyo hao tunapigana vikumbo.
 
Mara nyingi huwa nasema. Kuiwekea matumaini Taifa stars ni kama unaionea tuu.
Mtaendelea kuumia kila itakapocheza.
 
Najutia kiingilio changu,bora ngepiga zangu monde tu....!
 
Back
Top Bottom