Mkuu Malinzi, with due respect, tumekuwa "positive" tangu 1961! What do we have to show for all this time? Hata mimi niko pessimistic kidogo!
Again, with due respect, unaonaje mkiliangalia upya suala la sisi kung'ang'ania Uanachama wa "Shirikisho la Wachovu" (CECAFA), kuna sababu gani inayotuzuia sisi kujiunga na COSAFA ambako kuna ushindani zaidi? Hebu fikiria tukutane kila mwaka na A. Kusini, Zimbabwe, Malawi, Zambia, Botswana, angola, Malawi, Swaziland, n.k? Ninaamini tukihamia huko, baada ya vichapo kadhaa, tutapiga hatua kuliko kila mwaka kukutana na Timu kama Somalia, Eritrea, Burundi, n.k.
Kama ni vigumu sisi kujitoa CECAFA, basi angalau tuombe kualikwa mara moja moja. Kiwango cha Timu za COSAFA kiko juu kuliko cha CECAFA. Tunahitaji ushindani huo. Ninaamini wenzetu wa Nchi Jirani wangekuwa hapa kwetu ki-Jiografia wangekuwa tayari washatosa CECAFA kama walivyofanya Zambia, tena kwa manufaa makubwa baada ya Miaka kadhaa.
Ni mawazo yangu tu Mkuu! Asante!