Live Updates: Tanzania Vs Ivory Coast – World Cup Qualification 2014, June 16, 2013

... Updates
===
Hatutakubali, Stars waapa!

KWA maneno rahisi sana ni hivi; Taifa Stars ikipata sare au kupoteza mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Ivory Coast biashara yetu itakuwa imekwisha.
Lakini, haiwezekani hawa Ivory Coast waliopigana mazoezini watuletee jeuri, tena nyumbani kwetu.
Watanzania tupo milioni 45, lakini ni watu 60,000 pekee ndio wataingia kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Yaani tuzidiwe ujanja na kikundi cha watu 80 kilichokuja kutoka Ivory Coast!
Stars imeunganisha nguvu ya nchi nzima kuhakikisha inashinda mechi zake zote mbili zilizosalia kwa kuanzia na hii ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Taifa huku ikiombea angalau Morocco itoke sare na Ivory Coastkwenye mechi ya mwisho.
Kama hesabu za Stars zikienda sawa, Stars ikaenda na Gambia Septemba 6 ikachukua pointi tatu itaongoza Kundi C na kuingia kwenye hatua nyingine itakayohusisha vinara kumi wa makundi yote ya Afrika ambako kutachezwa mechi mbili za mtoano nyumbani na ugenini kupata timu tano za kucheza Kombe la Dunia.
Kocha wa Stars, Kim Poulsen anaimani kubwa na kikosi chake na kupoteza mabao 2-1 kwenye mechi iliyopita nchini Morocco hakujamkatisha tamaa ndio maana amewaomba Watanzania wamuunge mkono na kujazana uwanjani kushangilia kwa nguvu mwanzo mwisho.
“Tunacheza na timu ngumu na bora kwa bara la Afrika. Lakini hatupaswi kuwaogopa ingawa tunatakiwa kucheza kwa uangalifu mkubwa kwa kushambulia pamoja na kujilindakikamilifu, tusiachie upenyo hatakidogo wala kupepesuka kimaamuzi,” alisisitiza kocha huyo anayeamini katika soka la vijana.
Kim alieleza kuwa wanatakiwa kuwa makini zaidi katika dakika za mwanzo kwani iwapo wataruhusu bao la mapema linaweza kuwachanganya vijana wake na kuwatoa mchezoni na kuongeza kuwa kukosekana kwawachezaji watatu; beki Aggrey Morris aliyelimwa kadi nyekundu mechi ya Morocco, Mrisho Ngassaanayemiliki kadi mbili za njano pamoja na John Bocco aliye majeruhi hakuwezi kuathiri timu wala mashabiki wasihofu chochote kwani atabadili staili yamchezo.
Katika mazoezi ya Stars, Kim amesisitiza matumizi ya mipira ya kona pamoja na faulo kwenyekufunga na amempa Mwinyi Kazimoto jukumu la kupiga mipira hiyo na kuwataka mabeki Nadir Haroub Cannavaro na Erasto Nyoni kuhakikisha wanatumia vizuri uzoefu wao kufunga mipira ya vichwa.
WACHEZAJI
Nahodha wa Stars na kipa mwenye heshima kubwa nchini, Juma Kaseja alisema; “Tumejifua vya kutosha, mchezo hautakuwa rahisi kwetu. Ivory Coast ni timu bora Afrika, ina wachezaji wengi wanaocheza soka Ulaya, mashabiki watusapoti tufanye kazi kwa vitendo. Tupo vizuri na mwalimu ametupa mbinu nyingi.Tunawaahidi tutapambana hadi tone la mwisho kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”
Kiraka Shomari Kapombe alisema: “Nafikiri tupo sawa kimwili na kiakili. Mwalimu ametupa mbinu nyingi namna yakuwamaliza Ivory Coast katika mazoezi. Nadhani kilichobaki ni kuzifanyia kazi, mashabiki wajitokeze kwa wingi, waje kufurahi. Tunawaahidi kuwa tutacheza vizuri pamoja na kuwapa furaha ya ushindi.”
Beki wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema: “Mchezo utakuwa mgumu ingawa tumejipanga kwa hilo. Kama wachezaji tumejidhatiti kwa hilo ingawa dua za Watanzania pia ni muhimu katika kufanikisha ushindi wetu.”
MSIMAMO
Stars yenye pointi sita inashika nafasi ya pili kwenye Kundi C ambalo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10 huku Morocco ikishika nafasi tatu na pointi zake tano, Gambia inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.
MAJERUHI NA KADI
John Bocco anayekipiga katika klabu ya Azam FC atakosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi ya goti na daktari wa Stars, Mwanandi Mwankemwa alithibitisha hilo wakati Mrisho Ngassa hawezi kucheza kutokanana kuwa na kadi mbili za njano. Kadi hizo alipata katika mechi ya kwanza dhidi ya Ivory Coast na yapili alipewa na Morocco, beki Aggrey Morris atakosa pambano hilo kutokana na kulimwa kadi nyekundu katika mchezo uliopitadhidi ya Morocco.
STARS
Kikosi cha Stars kitakachoanza: Kipa Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nadir Haroub,Kelvin Yondan, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakari, Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto na Mbwana Samatta.
TIKETI
Kiingilio cha chini ni Sh.5,000 wakati cha walionazo ni Sh.30,000. Vituo vya mauzo ya tiketi hizo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, sokoni Kariakoo, Mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha MafutaBuguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani. Vituo vyote vipo jijini Dar es Salaam.
Viingilio vitakuwa kama ifuatavyo; Sh.5,000 viti vya kijani, 7,000 rangi ya bluu, 10,000 viti vya machungwa, 15,000 VIP C, 20,000 VIP B wakati VIP A itakuwa 30,000
KOCHA IVORY COAST
Kocha Mfaransa, Sabri Lamouchi (41) alilalamika kwamba kwenye mechi dhidi ya Gambia waliyoshinda mabao 3-0 walifanya upuuzi na kwamba timu yake itacheza staili yake ya mchezo kwenye mechi dhidi ya Stars.
Kurejea kwa Gervinho wa Arsenalna Salomon Kalou waliomaliza adhabu zao kunampa kiburi kocha huyo: “Hawa wachezaji watabadili sana staili yetu ya uchezaji, itatusaidia sana kwenyemechi na Tanzania, wana uzoefu na wameizoea timu.”

By: MwanaSports
 
tiketi za bei ndogo zimekwisha, vijana toka morogoro waliokuja na viingilio vya chini wakitegemea kuona match wanalalamika na kuanza kupigiana simu, too bad, barabara kuu ya kuingia taifa, imefungwa kwa magari makubwa mawili kupunguza Jam ya kuingia uwanjani, watu wameshaaza kufika maeneo ya uwanja milango bado imefungwa, tusubiri mtanange uanze, kila la heri stars, poleni wahanga wa mabomu Arusha.
 
Point of correction,......sasa hivi tunashika nafasi ya tatu na sio ya pili,Ivory Coast ipo nafasi ya kwanza ikiwa na points 10,Morocco nafasi ya pili kwa point 8, na tanzania nafasi ya tatu ikiwa na point 6 huku Gambia wakiwa wa mwisho wakiwa na point 1.
 
Nina uhakika tunakandamizwa nyumbani. Kwenye mambo ya msingi wenzetu wapo serious zaidi..! Baadaye utasikia ya kuwa Cote d'voire yaondoka na ushind mwembamba..!
 
WAKUU,kwa mara nyingine tena leo Taifa Stars inaingia uwanjani kukabiliana na Tembo wa Ivory Cost,tunahitaji kuishangilia timu yetu ili kushinda mchezo huo,nawaalika wadau wote wa JF Sports tujumuike humu kuleta mpmbanao huo moja kw amoja kutoka uwanja wa Taifa,kwa wale watakaokuwepo uwanjani.

Mimi nitakuwepo,Makoye Matale,Idawa,na wengineo Mtakuwepooooooooooooooooo?!

sa9 unauhakika?
 
Mkuu sitakuwepo uwanjani niko nje ya nchi, nitafuatilia hapahapa JF.
 
haya ndo matatizo ya mtoto wa kiume kupumuliwa mgongoni, huna ata aibu ya utaifa wako

Mkuu una maanisha tiGO Chop? Huyu dogo umemtendea haki. Utaifa mbele makundi mengine ya siasa, udini, ukabila nyuma kabisa. I love Tanzania, I love Taifa Stars. Go go go boys!
 
tiketi za bei ndogo zimekwisha, vijana toka morogoro waliokuja na viingilio vya chini wakitegemea kuona match wanalalamika na kuanza kupigiana simu, too bad, barabara kuu ya kuingia taifa, imefungwa kwa magari makubwa mawili kupunguza Jam ya kuingia uwanjani, watu wameshaaza kufika maeneo ya uwanja milango bado imefungwa, tusubiri mtanange uanze, kila la heri stars, poleni wahanga wa mabomu Arusha.

huuu wote ni uzembe wa mipango mibovu ya serikari ya mijizi ya ccm
 
...wacheza wa Ivory Coast' wakizipiga wakati wa mazoezi...
1016513_294700124000963_328291954_n.jpg
 
WAKUU,kwa mara nyingine tena leo Taifa Stars inaingia uwanjani kukabiliana na Tembo wa Ivory Cost,tunahitaji kuishangilia timu yetu ili kushinda mchezo huo,nawaalika wadau wote wa JF Sports tujumuike humu kuleta mpmbanao huo moja kw amoja kutoka uwanja wa Taifa,kwa wale watakaokuwepo uwanjani.

Mimi nitakuwepo,Makoye Matale,Idawa,na wengineo Mtakuwepooooooooooooooooo?!

Yeah!!! All the best Taifa Stars!!!
 
Mdau wabhejasana ila nitakushukulu sana kama unafahamu links yoyote kwenye Internet nitaweza kuangalia hii mechi ya leo ukatujulisha au mdau yoyote anayefahamu tafadhari.
 
Kuna link ya wiziwig wataonyesha live kwa watakao penda kuangalia kwenye Internet kama mimi.
 
Back
Top Bottom