FT: Germany 2-1 Ivory Coast | World Cup 2026 | BMO Field | Juni 20, 2026

FT: Germany 2-1 Ivory Coast | World Cup 2026 | BMO Field | Juni 20, 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,911
Reaction score
6,502
Ujerumani na Ivory Coast zinaingia katika mchuano huu wa Kundi E huko Toronto zikijua kwamba ushindi utawahakikishia nafasi katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia zikiwa zimesalia na mechi moja mkononi.

Habari za Mechi na Fomu ya Sasa

Ujerumani ilifikisha ushindi wa kumi mfululizo baada ya kuichapa kwa mabao 7-1 timu ngeni ya Curaçao inayoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza siku ya Jumapili, na kuonyesha wazi kwamba wasichukuliwe poa katika mashindano haya yanayoendelea. Mabao hayo saba yaliwasaidia kumaliza siku hiyo ya mechi wakiwa ndio wafungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia (mabao 239).

Ivory Coast nao pia walifungua msimu wao kwa ushindi, ingawa ulikuwa wa kusuasua na usio wa kushawishi sana, kufuatia kuifunga Ecuador 1-0 na kujipatia ushindi wao wa nne mfululizo wa kimataifa.

Kukutana kwao kwa mara ya mwisho na pekee ilikuwa ni katika mechi ya kirafiki mnamo Novemba 2009 ambapo walitoka sare ya 2-2.
 
Kama kweli Ivory coast wakitumia vizuri winga zao Leo wanaweza kupata Magoli, naona Germany kama wameingia na back three ambayo ukiwa makini unaweza kushambulia Kwa Counter vizuri Sana...
 
Tatizo kubwa linalozikabili timu za Afrika ni kukosa umakini na kutojiamini hali inayofanya wacheze kwa kiwewe, kama isingekuwa hivyo wangeweza kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano makubwa kama haya.

Hali hiyo huwafanya wapoteze sana pasi wanapocheza.
 
Jamaa hawako serious kabisa, Mimi mwanzo nilidhani wameuza game but ndivyo walivyo, Germany wana timu ya kawaida Sana. Yaani unaona kabisa Ivory Coast ni Jambo la kukaza kidogo tu hii mechi wangeshinda, Ivory coast wakienda mbele unaona kabisa kama wengekuwa serious Magoli wangepata.... Germany Hadi walichanganyikiwa, Jamaa wanakuja Tu...Hatupo serious...asiposhinda mechi ijayo anatoka maana Ecuador hatacheka na yyte.....
 
Wameniudhi sana
 
Tatizo Ivorycoast ni kocha anaona wachezaji wamechoka anachelewa kufanya sub, wachezaji hawajitumi hata kuwapigia kelele na pia wachezaji wengine hawajielewi kama yule aliyepewa pasi na Pepe anajigongagonga tu badala ya kutupia nyavuni pia pasi back zimekuwa nyingi..
 
Back
Top Bottom