Live updates: Mkutano wa Dr Slaa uwanja wa Kwaraa Babati

Live updates: Mkutano wa Dr Slaa uwanja wa Kwaraa Babati

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Wakuu.

Mtakumbuka kuwa leo Dr Slaa anafanya mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa Babati mjini.

Uwanja wa Kwaraa, Babati Mjini ndipo mahali ambapo Dkt. Slaa alimnyamazisha kbs aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba wakath wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010, pale alipomwambia kuwa endapo ataendelea tu kusema uongo wake, angefumua siri zake kwa nini alifukuzwa kazi ya ualimu mkuu kule Kigoma. Kuanzia hapo, Makamba hakuzungumza tena kabisa lolote kuhusu Dkt. Slaa na CHADEMA hadi kampeni zilipomalizika.

YANAYOJIRI

• Lawrence Tara, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi (kabla ya kuhamia CHADEMA mwaka huu), amemshangaa James Mbatia kubweteka na ubunge wa mezani, wakati ameshindwa kupigania ubunge halali ambao ulichakachuliwa na CCM hao hao mwaka 2010 Jimbo la Babati Vijijini (mgombea akiwa Tara). Amesema ameamua kuhamia kwa watu walio serious na mapambano ya kupigania haki na matumaini ya Watanzania.

• Pauline Gekul: nitaendelea kuwapigania wananchi na Watanzania wenzangu wa Babati Mjini katika nafasi yangu ya Viti Maalum, sasa tunawaonesha kuwa kuchakachua ubunge wetu mwaka 2010 hakukuwasaidia.

• Kazi ya mbunge ni kuisimamia na kuiagiza serikali. Kazi hiyo naifanya nanyi mnatambua jinsi ninavyowakaba koo kwenye ardhi yetu. Nawaomba Watanzania tuache mapenzi ya mshumaa kwa CCM, kuendelea kutumika kuimulikia huku sie tukiungua na kumalizika!

• Dkt. Slaa 'watu wa Babati mimi niliwaambia hapa kuwa Chambiri alifukuzwa kwao, akaja kugombea huku. Ninyi hamkuelewa. Simseng'enyi ni vibaya kumsema mtu kwa ubaya, lakini mbunge wenu namfahamu nimekaa naye bungeni. Wakati ule alikuwa anatokea Kenya kuja bungeni badala ya kutokea kwa wananchi wake Tarime. Si ajabu tena hata hapa haonekani.

• Dkt. 'Tanzania sasa ndiyo ina bunge, anamnukuu aliyekuwa Spika wa Bunge la Kenya Francis Ole Kapalo, ambaye alikuja wkt fulani Tz kuwafanyia wabunge semina na kusema Tz hakuna bunge, kuna mkusanyiko wa mashehe na wachungaji, hadi siku ngumi zitakapowaka bungeni kwa maslahi ya wtz ndiyo atajua kuna bunge'.

• Dkt. Slaa anasema wabunge wake kamwe hawatakaa kimya bungeni wkt twiga wanakunjwa wazima na kupandishwa ndege, tembo wanauwawa, maisha yanazidi kuwa magumu, ufisadi unaongezeka. Anasema ni unafiki kutetea amani, kuliko kuangalia rasilimali za Watanzia zikiibiwa mchana kweupe'.

• Anasema wawatukane na kuwabeza bungeni lakini mbele ya wananchi na Mungu wametimiza wajibu na wataendelea kutimiza wajibu huo bila kurudi nyuma.

• Anasema 'CCM waendelee kuchukua na kutumia sera zetu zile zile walizobeza mwaka 2010, sisi hatuna hiyana kwa sbb tunafurahi hatimaye ni Wtz wetu wananufaika. CCM watekeleze sera zetu, wasifikiri kuwa watatufilisi, mwaka 2015 tutakuja na akili mpya kabisa na tutawashangaza!

===================
Picha uwanjani hapo
===================

attachment.php

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.
 
HAM-D, dr. slaa hakulazimika kubaki padre kwa kuwa kuwa padre ni uamuzi wa mtu mwenyewe kwa hiyo hata makamba angeolea hilo wala isingekuwa shida. Pia kumbuka kuwa suala la Dr. Slaa siyo siri kwamba watu hawajui. Dr. Slaa alisema angefumua siri za Makamba za udhaifu alionesha wakati wa kutimiza wajibu wake kwa wananchi
 
Yani siku hizi CDM ni kama siafu waliokamata inzi. Zitto Tabora, Slaa Babati, Mbowe na makamanda wengine Arusha. Hadi raha...
umesahau Nddesamburo yuko Mwanza Ally Binanga yupo Iramba acha wachakarikaji wengine ambao taarifa hazijaingia jamvini moto unawake nchi nzima
 
Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuhasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.
Makamba alifukuzwa ualimu Kigoma baada ya kuwapa mimba wanafunzi shuleni. Haya na wewe lete santuri yako kuhusu Dr Slaa.
 
mkuu Mohamedi Mtoi wake picha kwani kuna akina Timaso wengi hapa jf.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuhasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.
Dr Slaa kuwa alikuwa Padri ni fact na kwamba aliacha upadri kwa taratibu zao ni fact kwa hiyo hakuasi kama unavyosema,Lakini Makamba kubaka mtoto wa shule na kukimbia mpaka kuacha ukuu wa shule kigoma ni fact anahitajika kufunguliwa kesi ya ubakaji
 
Kiukweli CCM hawana chao tena katika mkoa wa Manyara 2015. Taswira ya CCM hivi sasa katika jamii haina tofauti ya kibaka!
 
umesahau Nddesamburo yuko Mwanza Ally Binanga yupo Iramba acha wachakarikaji wengine ambao taarifa hazijaingia jamvini moto unawake nchi nzima
Yani ukimwangalia inzi wakati amenaswa na siafu utamhurumia. Mwingine anakamata mguu, mwingine bawa, mwingine tumbo.... Yaani CCM haitafurukuta mwka huu...
 
Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuhasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.

Mzee Makamba hana siasa za kishakunaku kama walivyo chadema wao huwa wanaangalia maisha binafsi wakati kuna mambo mengi maovu wanayafanya. Kanakambwa hawaoni uovu wao.
Hivi haujiulizi ni kwanini viongozi wengi wa Ccm hawamuataki mtu ktk maisha binafsi?
 
Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuhasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.

Utahangaika sana lakini nakuapia hutafanikiwa.Kuna wengi kama wewe walihangaika hivi hapa jamvini wakachemsha wenyewe.
 
Dr Slaa kuwa alikuwa Padri ni fact na kwamba aliacha upadri kwa taratibu zao ni fact kwa hiyo hakuasi kama unavyosema,Lakini Makamba kubaka mtoto wa shule na kukimbia mpaka kuacha ukuu wa shule kigoma ni fact anahitajika kufunguliwa kesi ya ubakaji

tupeni update za mkutano tafadhali..hizo rumaz za magamba tushazizoea
vipi muitikio wa watu ?Dr yupo na makamanda gani na wangapi?
ni m4c au na udiwani?
magamba kwa uzushi wanarikodi muvi ingine sasahivi kua LEMA na CHADEMA ndio walilipua kanisa.
ahahahhaaaaaa.....watakoma mwaka huu watu washaamka bhana!!!!!!!!
 
Mzee Makamba hana siasa za kishakunaku kama walivyo chadema wao huwa wanaangalia maisha binafsi wakati kuna mambo mengi maovu wanayafanya. Kanakambwa hawaoni uovu wao.
Hivi haujiulizi ni kwanini viongozi wengi wa Ccm hawamuataki mtu ktk maisha binafsi?

Kama unarepent zambi zako kwamba utaacha kuattack viongozi wa chadema na maisha yao basi ni uamuzi wa busara,leo hii NAPE na Kinana wanazunguka na Mtela na Shonza kwa sababu wanatukana viongozi wa chadema matusi ya nguoni,kama umeamua kubadirika tutakushangaa angalia posti zako,Makamba ndio mwalimu wa siasa za maji taka nchi hii hata Sitta alimsema makamba kuwa bingwa wa siasa za maji taka na CCM kwa ujumla
 
Dr Slaa kuwa alikuwa Padri ni fact na kwamba aliacha upadri kwa taratibu zao ni fact kwa hiyo hakuasi kama unavyosema,Lakini Makamba kubaka mtoto wa shule na kukimbia mpaka kuacha ukuu wa shule kigoma ni fact anahitajika kufunguliwa kesi ya ubakaji

Makambaaa! Ile mimba itakuwa ndio huyu Februari makamba!
 
Chadema hawana jipya kila wao ni kulalama tu! Utadhani mjane!
 
Ha!ha!Ha,

Kauli zako hizi zimekuwa Kama kiburudisho. Sasa nimeamini au ulna tatizo la ignorance, and seems you are untrainable material. Kwa Taarifa ya wale ambao hawajui utaratibu wa Kanisa Katoliki,
I) Padre wa Kanisa Katoliki ni kweli anaweza kuasi au anapewa Kibali maalum na Papa kinaitwa Decree of Laizization.
2) Padre aliyepewa Decree of Laizization anapewa katika instrument hiyo hiyo, mambo anayoweza kufanya na ambayo hawed kufanya na utaratibu wa kufanya ikiwa ni pamoja na Utaratibu wa Kufunga Ndoa.

3) Dr Slaa hakuasi Bali alipewa Decree of Laizization kwa utaratibu wa Kanisa Katoliki. Kama hufahamu utaratibu wa mambo ya watu waachie wanaoyajua,I vinginevyo utaonekana Pumbuani.

4) Waliomfanyia Sherehe ya Upadre Padre Slaa ni wananchi wa Karatu, na hao hao wanaojua history na Maisha ya Dr Slaa ndio waliomwomba awe Mbunge wao kwanza kwa ticket ya CCM ( na nikashinda kura ya maoni). Hao hao wananchi wa Karatu ndio waliomchagua kwa kura bila kuhonga Dr Slaa Mara 3 (tatu!). Wanaomjua Dr Slaa wanakushangaa. Endelea tu na kelele zako haina impact kwa yeyote, isipokuwa wale wa aina yako tu.

Wakati unahangaika na Dr Slaa, maelfu ya Wananchi Babati wamefurika uwanjani wakigombea kumsikiliza Dr. Slaa. endelea kuwa Katibu mwenezi wangu, kwani umaarufu wa mtu unajengwa kwa kumtangazia mema au mabaya. Tutapiga mguu kila kijiji hadi kieleweke.

Mzee Makamba mstaarabu tu, kama ningekuwa mimi kwenye nafasi hiyo hiyo ya Makamba, ningemwambia na mimi nitazitoa siri zake (Dr Slaa) zote za kuhasi upadre. Tuone nani ingemgharimu.
 
Back
Top Bottom