Live updates: Mkutano wa CHADEMA viwanja vya Dr Slaa - Mbeya

Live updates: Mkutano wa CHADEMA viwanja vya Dr Slaa - Mbeya

Hebu wahi kumnongoneza hapo asisahau kuwaambia vijana kuwa yule kiongozi wa vijana waliomaliza JKT ametekwa kama Ulimboka na kusulubiwa kwa vile tuu anahamasisha wenzake wakaulize zile ajira walizo ahidiwa na serikali ya CCM ziko wapi? Ni vema wafahamu wote maana kuna wengine hawana taarifa hiyo. mohamed Mtoi
huu ni upumbavu chakaza unaoueneza. soma masharti ya kujiunga na JKT. narudia tena kukuambia huu ni upumbavu unaoeneza. tumia kichwa kufikiria.
 
Hivi huko Mbeya ameenda na Joyce Mukya ama na mama Liliani Mtei?
Nadhani atakuwa ameenda na Hot Lady. Si unajua tena wazee wa kisasa tunapenda vitu vya moto!:smile-big::smile-big:
 
Tatizo la CDM ni kwenye kulinda kura!
Wala hilo siyo tatizo. Wenyewe wanapita majukwaani kutangaza ushindi wakati wenzao CCM kwa kutumia mabalozi wao wanapita nyumba kwa nyumba kufanya sensa ya wapiga kura wanaowaunga mkono na kuwahamasisha kujiandikisha na kupiga kura.
 
chadema niliwadhara sana, kwa sasa nawakubali sana......
 
Hiyo ndiyo kazi makamanda....
Kidogokidogo ccm WANAANZA KUINGIA MITINI, Baada ya muda mfupi Ikulu itakuwa nyeupeee
 
Ccm wakiona hizi picha za makamanda wakiwa na raisi wao mtarajiwa Dr Slaa wanachanyikiwa kabisa.
 
Muda huu mwenyekiti wa chama Taifa anahutubia mkutano kwenye viwanja vya Dr Slaa hapa Mbeya mjini.

Ni mkutano wa hadhara baada ya kumaliza kikao cha ndani cha baraza la uongozi la kanda ya Nyanda za juu Kusini, kanda hii ina mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Mbeya. Makao makuu ya kanda hii yako hapa mjini Mbeya.

Yaliyojiri

- mbunge wa Mbeya mjini kamanda Joseph Mbilinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wana Mbeya kwa kuzidi kuonyesha imani kwake na Chadema, aliwashukuru wana Mbeya kwa kuipatia Chadema ushindi wa kishindo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya. Aliwaahidi utumishi uliotuka kutokana na upendo wa dhati wanao uonyesha kwake na Chadema.

- Mheshimiwa mbunge alitumia fursa hiyo kuwatangazia rasmi wakazi wa mjini wa Mbeya kuwa daraja la Iyela makaburini kata ya Iyela limezinduliwa rasmi baada ya serikali kukataa kiongozi wa kambi ya upinzani kulizindua daraja hilo ambalo limejengwa kwa mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi millioni 58, akasema "...daraja hilo lingejengwa na ccm wangesema limejengwa kwa zaidi ya millioni 400.

- Kamanda Mbowe aliwapokea makada wawili wa ccm walio hamia Chadema, makada hao ni Joseph Mlozi aliyekuwa katibu wa ccm wilaya ya Makete na ndugu Okoa Mwaitenga aliyekuwa katibu mwenyezi wa ccm wa kata ya Mwakibete. Aliwakaribisha Chadema huku akiwaasa waache tabia zote chafu walizotoka nazo ccm, alizitaja tabia hizo kuwa ni Rushwa, Wizi, Ufisadi na majungu. "... Tabia hizo ni kinyume na utamaduni wa Chadema..."

- Aliongelea kuhusu uimara wa UKAWA na mpango mkakati kuelekea uchaguzi wa Oktoba, aliwaambia wana Mbeya walio furika uwanjani hapo kuwa, "... UKAWA bado uko imara sana kwa ajili ya kuwakomboa watanzania, tegemeeni wagombea bora wa UKAWA wa udiwani, ubunge na hatimae mgombea urais atakaye patikana baada ya mchakato wa ndani ya UKAWA kukamilika..."

- Mh Mbowe alitumia fursa hiyo kumuonya Mzee (Jiji) Lubuva kulinda heshima yake ili asije kuingia Kwenye historia mbaya ya kuiingiza nchi kwenye machafuko kutokana na hila ambazo tume ya uchaguzi imesha anza kuzifanya kwenye mchakato wa kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura. Alielezea namna tume hiyo ilivyo vunja sheria ya mwaka 1985 kama ilivyo rejewa 2010 kifungu cha 15 (1) kwa kuto boresha daftari la wapiga kura kabla na baada ya uchaguzi. Tangu 2010 baada ya uchaguzi daftari hilo halikuwahi kuboreshwa.

- Alieleza pia kuwa wataalamu wa nje walio tumiwa na tume kwenye ushauri wa kitaalamu kuhusu mfumo wa BVR wamewaandikia tume ya Taifa ya uchaguzi ripoti ambayo imebainisha kuwa tume hiyo haina uwezo wala vifaa kumudu uandikishaji wa BVR, ripoti hiyo imeeleza changamoto mbalimbali ambazo tume haiwezi kukabiliana nazo na kimsingi ni kwamba zoezi hilo limesha anza kukwama na tume na serikali hawana uwezo wa kujinasua kutokana na ukosefu wa fedha.

Eee Mola wetu mwema sana, bariki ukombozi huu ukamilike vyema Oktoba mwaka huu, tuukomboe umma na taifa hili dhdi ya ukoloni wa mafirauni CCM na genge kuu la ujangili, ufisadi linaloangamiza rasilimali za umma, na sasa linachezea daftari la wapiga kura ili liendelee kujilinda madarakani kwa udhalimu na ushindi haramu! HAKI itashinda uovu huo wa CCM, itaanguka! Tunaomba mwenye nakala ya Ripoti hiyo ya udhaifu wa system za BVR aiwasilishe na wanasheria waiweke rasmi ktk adendum au droo zao rasmi kuandaa kesi pale BVR itakapovuruga kura! Tume hii ya uchaguzi ni mhimili wa uovu. Jaji LUBURA UTAKUWA adui namba moja wa HAKI kwa kukubali kutumika wakati akijua kila mwananchi ameshautambua ujanja na udhaifu wa BVR! Atakimbilia wapi? Labda ajiandae kuwahi ICC maana hatakuwa na pa kuhemea litakapomtokea kuvuruga kura.
 
Chadema jitahidini angalau mwaka 2025 mchukue kama mtakuwa hamjagawana mbao
 
Ungekuwa unajua kuoga angeenda na wewe, tatizo unanuka mikojo muda wote!

Nimecheka tu. Siyo kwamba nimependa, ila kwa sababu aliyeambiwa hajui uzito wa maneno haya na kesho atarudia, ndo dalili uchizi. Tumbo mwanaharamu kwa kweli
 
huu ni upumbavu chakaza unaoueneza. soma masharti ya kujiunga na JKT. narudia tena kukuambia huu ni upumbavu unaoeneza. tumia kichwa kufikiria.
Mkuu Abunuas masharti sio hoja lakini jee unajua ni ahadi gani walikuwa wanapewa hao vijana kabla ya kujiunga? Tatizo lenu kila kitu mnatumia siasa ya ulaghai ili kukifanikisha na mwisho mnaposhindwa mnasingizia masharti ambayo wakati mnawashawishi kujiunga na JKT hamkuwafafanulia kwa uwazi bali mlizingatia ulaghai wa ahadi ili mfanikiwe. Sasa imekula kwenu.
Niambie ni sababu gani inayowafanya muanze kuwakamata kwa siri viongozi wa hao vijana na kuwatesa? Kama hakukuwa na ahadi yeyote usiri wa nini katika kuwakamata? Mngeweza tuu kuwakamata na kuwashtaki kuwa wanafanya uchochezi wa kitu ambacho hakipo. Msitumie vijana masikini kama mtaji wenu wa kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
kwanza nikutoa wasiwasi mimi sio sehemu ya utawala uliopo au zilizopita na wala sifaidiki kwa chochote kwa maana ya kipato zaidi ya wao kuja kukata kodi kwenye mapato yangu.
binafsi sipendi ushabiki wa kijinga kama huu unaotaka kuueneza hapa, na hata kama mimi sio sehemu ya utawala siwezi kushabikia upuuzi kama huu. ukisoma kwenye taratibu za kwenda JKT hakuna inapotamkwa kuwa na mkataba wa kuajiriwa, ila ni kufundishwa uzalendo (ambao hata hivyo siuoni kwa akina lowasa na wengineo walioenda huko).
ninachokumbuka kwenye ahadi za kwenda JKT alichosema sifue (chief secretary) ni kuwa ikitokea kwenye kuajiriwa kuwa wanafanana kwa vigezo basi aliyeenda JKT itakua added advantage.
bado naendelea kukusisitiza kuandika ukweli hata kama una masilahi ya kichama. (binafsi sina chama ndo maana natwanga kote kote kwa kubaki kwenye ukweli daima na sio unafiki kama ulivyo wewe)
Taifa hili ni letu sote tukiliharibu hakuna taifa mbadala la kukimbilia zaidi ya kwenda kuwa wageni a.k.a wakimbizi.
tafakari, chukua hatua.

Nakushukuru kwa maelezo yako marefu. Nakushukuru pia kwa kuniona mpuuzi, na mshabiki wa kisiasa. Haina shida huo ni muono wako. Tulipokwenda JKT miaka hiyo ya 1980's kwa mujibu wa sheria tulikutana na vijana wengi waliokuwa wanaenda voluntary na wale wa wakati ule walikuwa wanaelezwa wazi kuwa wanakwenda kufundishwa uzalendo na jinsi ya kujitegemea baada ya kujifunza fani mbalimbali. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati ule na walifahamu hivyo.
Baadae mafunzo hayo yalifutwa kwa sababu ambazo serikali inazijua. Yaliporudi wale wa kujitolea wakawa hawapatikani na ndipo serikali ilipobuni mbinu ya kuwaambia watafikiriwa nafasi za ajira kwenye majeshi yetu ya ulinzi na usalama ili kufanikisha kupata vijana.
Kuhusu hizo taratibu na malengo yaliyoandikwa kwenye mkataba wa kujiunga na JKT, unataka kuniambia kijana wa kijijini aliyemaliza darasa la saba anao uwezo wa kuusoma huo mkataba na kuuelewa au ataelewa maneno yaliyotolewa na kiongozi bila kujua kuwa ni hadaa? Mbona unataka kuwaonea hao vijana kwa kuwapa mtihani mkubwa kuliko uwezo wao?
Nakuhakikishia kama taifa linachafuka sio kwa mimi kuhoji kwa nini watu wanateswa kwa kuuliza ahadi waliyopewa bali ni kwa ahadi za uongo zinazotolewa kwa vijana hao na wanasiasa uchwara kisha wakiulizwa wanakuja na mbinu za kimafia. Kweli taifa ni letu wote na tukitaka salama basi bora vile viashiria vya machafuko tuvikemee na sio kuvificha chini ya kapeti na kuimba wimbo wa amani. Vijana wakiwa na njaa ni hatari kuliko simba wa porini.
 
Anyway nisingependa sana malumbano na wewe kwenye hili ila nilikupa angalizo tu kwa mbegu unayopandikiza kwa watanzania.
lakini hata hizo ahadi labda kama ni zingine ambazo sikuzisikia lakini kama ni zile walizoahidi hata mimi nilizisikia. na ndo hicho nilichokueleza, kwa maana oppotunity ikitokea watapata. hata mimi nina majirani ambao watoto wao wamepata ajira ya upoliccm. lakini sio kwa huo uchochezi unaouleta.
labda nikuachie tafakuri ndogo tu. jiulize hao wote wanaomaliza JKT kila mwaka wanaweza kuajiriwa na serikali? kwa kazi ipi?
Kwa heri chakaza na jumapili nje,a.

Back
Top Bottom