Live updates: Mkutano wa CHADEMA viwanja vya Dr Slaa - Mbeya

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Muda huu mwenyekiti wa chama Taifa anahutubia mkutano kwenye viwanja vya Dr Slaa hapa Mbeya mjini.

Ni mkutano wa hadhara baada ya kumaliza kikao cha ndani cha baraza la uongozi la kanda ya Nyanda za juu Kusini, kanda hii ina mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Mbeya. Makao makuu ya kanda hii yako hapa mjini Mbeya.

Yaliyojiri

- mbunge wa Mbeya mjini kamanda Joseph Mbilinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wana Mbeya kwa kuzidi kuonyesha imani kwake na Chadema, aliwashukuru wana Mbeya kwa kuipatia Chadema ushindi wa kishindo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya. Aliwaahidi utumishi uliotuka kutokana na upendo wa dhati wanao uonyesha kwake na Chadema.

- Mheshimiwa mbunge alitumia fursa hiyo kuwatangazia rasmi wakazi wa mjini wa Mbeya kuwa daraja la Iyela makaburini kata ya Iyela limezinduliwa rasmi baada ya serikali kukataa kiongozi wa kambi ya upinzani kulizindua daraja hilo ambalo limejengwa kwa mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi millioni 58, akasema "...daraja hilo lingejengwa na ccm wangesema limejengwa kwa zaidi ya millioni 400.

- Kamanda Mbowe aliwapokea makada wawili wa ccm walio hamia Chadema, makada hao ni Joseph Mlozi aliyekuwa katibu wa ccm wilaya ya Makete na ndugu Okoa Mwaitenga aliyekuwa katibu mwenyezi wa ccm wa kata ya Mwakibete. Aliwakaribisha Chadema huku akiwaasa waache tabia zote chafu walizotoka nazo ccm, alizitaja tabia hizo kuwa ni Rushwa, Wizi, Ufisadi na majungu. "... Tabia hizo ni kinyume na utamaduni wa Chadema..."

- Aliongelea kuhusu uimara wa UKAWA na mpango mkakati kuelekea uchaguzi wa Oktoba, aliwaambia wana Mbeya walio furika uwanjani hapo kuwa, "... UKAWA bado uko imara sana kwa ajili ya kuwakomboa watanzania, tegemeeni wagombea bora wa UKAWA wa udiwani, ubunge na hatimae mgombea urais atakaye patikana baada ya mchakato wa ndani ya UKAWA kukamilika..."

- Mh Mbowe alitumia fursa hiyo kumuonya Mzee (Jiji) Lubuva kulinda heshima yake ili asije kuingia Kwenye historia mbaya ya kuiingiza nchi kwenye machafuko kutokana na hila ambazo tume ya uchaguzi imesha anza kuzifanya kwenye mchakato wa kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura. Alielezea namna tume hiyo ilivyo vunja sheria ya mwaka 1985 kama ilivyo rejewa 2010 kifungu cha 15 (1) kwa kuto boresha daftari la wapiga kura kabla na baada ya uchaguzi. Tangu 2010 baada ya uchaguzi daftari hilo halikuwahi kuboreshwa.

- Alieleza pia kuwa wataalamu wa nje walio tumiwa na tume kwenye ushauri wa kitaalamu kuhusu mfumo wa BVR wamewaandikia tume ya Taifa ya uchaguzi ripoti ambayo imebainisha kuwa tume hiyo haina uwezo wala vifaa kumudu uandikishaji wa BVR, ripoti hiyo imeeleza changamoto mbalimbali ambazo tume haiwezi kukabiliana nazo na kimsingi ni kwamba zoezi hilo limesha anza kukwama na tume na serikali hawana uwezo wa kujinasua kutokana na ukosefu wa fedha.
 

Attachments

  • 1424529181333.jpg
    1424529181333.jpg
    72.2 KB · Views: 11,479
  • 1424529216849.jpg
    1424529216849.jpg
    50.1 KB · Views: 10,324
  • 1424529231771.jpg
    1424529231771.jpg
    60.3 KB · Views: 7,600
  • 1424529248301.jpg
    1424529248301.jpg
    54.3 KB · Views: 4,043
  • 1424529268721.jpg
    1424529268721.jpg
    77.1 KB · Views: 8,809
  • 1424529284082.jpg
    1424529284082.jpg
    36.4 KB · Views: 9,757
Hana jipya huyo mzee, amekua katuni siku hizi ndio maana watoto wanajazana kumuona
 
Ni matumaini kaa hayo tunataka. Si ahadi hewa 1000000 bila hata moja kutimizwa. Bado watu hawajaipata ruhusa, je wakiruhusiwa itakuwaje? Fikiri kwanza, chukua hatua.
 
Hebu wahi kumnongoneza hapo asisahau kuwaambia vijana kuwa yule kiongozi wa vijana waliomaliza JKT ametekwa kama Ulimboka na kusulubiwa kwa vile tuu anahamasisha wenzake wakaulize zile ajira walizo ahidiwa na serikali ya CCM ziko wapi? Ni vema wafahamu wote maana kuna wengine hawana taarifa hiyo. mohamed Mtoi
 
Last edited by a moderator:
Mtoi habari hii imechelewa sana , hata hivyo tunakushukuru kwa ulipoanzia , siyo mbaya , japo next time jaribu kuleta updates mapema mjomba , cdm ni maisha jamani sasa mnapotuchelewesha kiasi hiki hamtutendei haki .
 
Back
Top Bottom